Usaliti kwa Mkewe wamponza, akosa mchepuko na utajiri

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari za wakati huu wapendwa

Tafuta pesa kwa nguvu zote ila nimeanza kuamini ule msemo wa wahenga kwamba kipato huleta majivuno.

Sio simulizi imetokea kweli kabisa kwa baba mmoja ambaye ni dereva wa taxi (UBER) kwa sasa ambaye ni jirani yangu na nimefahamiana naye kitambo sana.

Jamaa alioa mke kutoka Tanga pisi kali kali kweli kweli lakini hawakubahatikaga kupata mtoto licha ya kusema mwanamke ndio mwenye tatizo lakini mimi siamini maana huyo jamaa anamichepuko ya kutosha na bado hajapata mtoto hata wa kusingiziwa.

Baada ya kufunga ndoa na kuishi wote maisha ya shida chumba kimoja mwananyamala miaka ya 90 dada wa jamaa akampeleka wifi yake kwa mganga wakapata mtoto mmoja ila akaambiwa kabla mtoto hajatembea aende akapewe dawa ili azae moja kwa moja akapuuza hakwenda wakabaki na mtoto mmoja tu hadi leo ni huyo huyo.

Kisa chenyewe ni kwamba baada ya kuhangaika muda mrefu bila ya kuwa na kazi ya uhakika mke wa jamaa akaamua aende kwao Tanga na mtoto na aliporudi mambo yakaanza kuwanyookea.

Jamaa akapata kazi kwenye mgahawa mmoja maeneo ya manazi mmoja kidogo akajenga nyumba kubwa ya vyumba 6 hajakaa sawa akajenga nyingine mara akanunua daladala akanunua na shamba kama heka 10 hadi mwaka 2010 jamaa alikuwa anamigahawa yake 3 kwenye maofisi makubwa ya kiserikali vibali vyote akawa anachukua tenda ya kupika kwenye shughuli mbali mbali na kipato kizuri tu.

Kipato huleta majivuno jamaa baada ya kupata hela akamroga mke wake amsikilize yeye tu hata kwenda sokoni huyo mwanamke hawezi kwenda peke yake yani.

Jamaa akamuajiri ndugu yake mmoja sasa huyo ndugu yake akawa anatoa umbea kazini analeta kwa mkewe kuhusu jamaa kuwa na mchepuko ameupangia na chumba kabisa mtoto wa kichaga. Mwanamke akatoa kauli moja tu achana na huyo mwanamke akanyamaza.

Jamaa akaleta ubishi mkewe akampa sharti moja tu kama anataka kumuoa huyo mwanamke basi yeye amfungulie duka tu jamaa si kiburi akamjengea fremu akamfungulia duka kubwa tu.

Mwanamke akawa anamcheki tu basi mkewe akaanza kuuza duka lake kawaida tu nao mawifi wanachagiza aoe mke wa pili apate watoto.

Yule mkewe alipoona mambo yamekuwa mazito akamuachia mwanae aendeshe duka mwanamke akaenda kwao Tanga aliporudi ndio Sekeseke likaanza sasa

Kwanza ule mchepuko wenyewe ukamwambia jamaa mimi sitaki ndoa na wewe tuachane tu sitaki matatizo na wewe hapo jamaa alishapeleka hadi barua ya uchumba yani.

Pili akapata ajali gari yake ikaharibika sana akashimdwa kuitengeneza akaiuza Tandale kwa wale wanaonunua magari mabovu.

Tatu migahawa yake yote ikaanza kufilisika mara serikali haimlipi akaamua kufunga akarudisha vitu nyumbani akapumzika.

Akapata tenda ya kupika kwenye chuo kimoja Dar akauza daladala ili afanye mtaji akafanya biashara kama mwaka mmoja hivi pakamshinda akaacha.

Akarudi nyumbani anamtazama mkewe tu ikabidi mkewe atoe hela kwenye duka lake amnunulie gari ndio awe dereva wa UBER ila nyumba yake kubwa ya vyumba 6 akapangisha vyumba vitano maisha yakawa yanaendelea.

Kama huamini uchawi na ushirikina ni wewe tu jamaa akaenda kwa mganga mganga ndio akawa anamwambia sasa kwamba
~kwamba jamaa alianza kupata mafanikio kupitia mgongo wa yule mkewe na alipomkera mkewe kaamua aharibu kila kitu ili wakose wote maana jamaa alikuwa na kiburi cha pesa.
*Hapo kufanikiwa kupitia mwanamke ni kwamba mwanamke alipoenda kwao kumpeleka mtoto ndio alipewa hizo dawa na masharti yani wabaki na mtoto huyo huyo kama wanataka mali na masharti mengine ambayo jamaa hajayasema.

~Mkewe alipoenda Tanga baada ya jamaa kuleta mchepuko ndio akaambiwa sasa kwamba jamaa kamfunga pia anakiburi sababu ya kupata pesa ndio mwanamke akataka kumkomesha mumewe na mchepuko ili wakose wote ambapo mchepuko wenyewe ukasalimu amri na jamaa akaanza kufilisika.

Hapo lipo kubwa sana la kujifunza kupitia kwa huyo rafiki yangu
~Acha majivuno pale unapopata kipato.
~Heshimu mkeo wa ndoa hata kama anakasoro za kuvumilika kikubwa kama mlichuma mali pamoja.

Ni hayo tu
 
Unapoamini jambo lolote imani yako inakuunganisha na jambo hilo na muda huo huo unaanza kuona matokeo yake. Imani inamsha na kuaksi mazingira, hali halisi na mipango yote inayoshabihiana na imani yako. Yote yanatokea kwa kadri au ukubwa wa imini yako kwani unashughulika na roho.

Hii ni karakana yako ambapo ulimwengu wako utauona katika mwelekeo wa imani uliyonayo na kila kitu kitatokea kama unavyoamini.

Watu wawili wanaweza kwenda kwa Mungu, mganga au mchawi wakafanikiwa au mmoja asifanikiwe wingine akafanikiwa. Kwanini? IMANI......kubwa au ndogo.

Ukiamini uchawi utauona, ukiamini Mungu utamwona. Ukipanda bangi utaotesha na kuvuna bangi wakati huo huo ukipanda mahindi eneo hilo hilo utaotesha na kuvuna mahindi.

Uchaguzi ni wako
 
Chai Mbovu Hii
Nani anakitafunio hapo.

Mtoto amekua fasta kama ka broiler mpaka akaachiwa duka auze.

Vitafunwa unaleta au tuinywe kavu kavu?

Huyo mtoto anaeachiwa duka auze ndo huyu alozaliwa au??
Chai iko wapi?

1. Baada ya kufunga ndoa na kuishi wote maisha ya shida chumba kimoja mwananyamala miaka ya 90

2. Jamaa akapata kazi kwenye mgahawa mmoja maeneo ya manazi mmoja kidogo akajenga nyumba kubwa ya vyumba 6 hajakaa sawa akajenga nyingine mara akanunua daladala akanunua na shamba kama heka 10 hadi mwaka 2010

Hapo mtoto ana miaka 20.👆👆👆👆


3. Jamaa akaleta ubishi mkewe akampa sharti moja tu kama anataka kumuoa huyo mwanamke basi yeye amfungulie duka tu jamaa si kiburi akamjengea fremu akamfungulia duka kubwa tu.

4. Yule mkewe alipoona mambo yamekuwa mazito akamuachia mwanae aendeshe duka mwanamke akaenda kwao Tanga aliporudi ndio Sekeseke likaanza sasa

Sasa nyie wadau mnaosema ni CHAI...

KWAMBA HUKO KWENU MTOTO WA MIAKA 20 HAWEZI KUACHIWA BIASHARA?

Hiyo chai iko wapi ?? 😳😳😳

Au huko kwenu vijana ni mandezi kwamba miaka 20 HAWEZI KUACHIWA duka mpaka wafike 30

Waambie vijana wenu waamke.

JUMAPILI NJEMA.
YESU NI BWANA.

#YNWA
 
Back
Top Bottom