Upendo unaweza kuisha ghafla kiasi hiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upendo unaweza kuisha ghafla kiasi hiki?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Blaki Womani, Apr 4, 2011.

 1. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Habari ya J3 wana JF
  Jana jumapili nilikwenda kwa jirani yangu kumsalimia nilipofika nilimkuta yeye na dereva wake wa kazini wote wanalia kuuliza kulikoni jirani yangu akaniambia dereva wake amefiwa na mkewe mie na jirani yangu tukawa tunamfariji huyo dereva kwa msiba alioupata.
  Ilibidi niulize ilikuwa vipi, jirani yangu akanieleza walikuwa njiani kutoka kazini simu ikapigwa kwamba mkewe amepata ajali Moshi wamempeleka hospital, dereva akaamua kumpeleka kwanza boss wake nyumbani ili aweze kufanya utaratibu mwingine alipofika nyumbani kwa boss wake akapigiwa simu mkewe amefariki. mwishowe yule dereva akaondoka kurudi nyumbani kwake.
  Leo asubuhi nimekwenda pale kwa jirani yangu kujua maandalizi yanakwendaje tuweze kushirikishana cha ajabu nikamkuta yule dereva amekuja kumchukua boss wake kumpeleka kazini.
  Nikajiuliza amepata wapi nguvu ya kuweza kufanya kazi leo baada ya msiba mkubwa kama huo kutokea?

  Ninajiuliza je huyo Dereva alikuwa hampendi mkewe au baada ya kufa upendo unatoweka ghafla hata kabla ya maziko?
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa waache wafu wazikwe na wafu wao.

  Labda jamaa ameamua kulinda kibarua na wkt huo akiendelea na hatua za kuomba ruhusa kazi za watu bana we acha.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  BW kulia sana haina maana ndo mtu alipenda sana!
  Kila mtu ana namna yake ya kudeal na mambo kama hayo....kuna wale wapia mayowe....wanaolia kimya kimya vichwa vimeinamishwa mpaka ainuke ndo unajua amelia....kuna wale nje anaonekana yuko ngangari au hajali ila akifika sehemu yenye usiri analia kama mtoto...na kuna wale ambao hua wanakusanya huzuni zao mpaka siku zitakapowalemea ndo wanaziachia.
  Inawezekana anaumia sana ila hana jinsi....si ajabu anaendelea na kazi ili asikose pesa ya kufanikisha mazishi.Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla hujasema ''fulani hajali kabisa....kafiwa juzi leo yuko bar anakunywa!''
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Si dhani kama hana upendo,
  Mazishi yanahitaji maandalizi, na kusafiri kunahitaji maandalizi.
  Dereva kama mfanyakazi kunataratibu za kuaga kazini na kukama ikiwezekana akapata chochote cha kumsaidia kwa msiba.

  Fikilia +
   
 5. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mshangao - No comment
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  labda ndo alikuwa anaenda kazini kuchukua ruhusa ajikate mazikoni. asiyekuwepo machoni na moyoni hayupo.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Si kuna mama kafiwa na mmewe wake mtaani kwetu baada ya msiba kuisha na watu kutawanyika ameolewa na jamaa mwingine hata mwezi haujaisha anaendelea kula maisha kama kawa tena nimepewa kadi ha harusi ipo kibindoni nitanunua ndizi zangu na pilipili nawahi kula mpunga.
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa msiba umetokea Jumapili, ofisini kwake kulikuwa kumefungwa. Kiuratibu huyo dereva kama mtumishi anapaswa kwenda kazini leo ili aombe ruhusa na kukabidhi gari; maana madeva wa taasisi nyingi ni kwaida kuwa magari yako chini yao muda wote. Ina maana akienda asubuhi atatoa rasmi taarifa ya msiba na kuomba ruhusa; na ofisi nyingine anaweza kupewa hata usafiri na watu/mtu wa kumsindikiza kwenye msiba.
   
 9. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Ni sawa unavyosema lakini nilikuwa nafikiria kama ni mie ningeweza kufanya hivyo
  msiba unapotokea inakuwa umechanganyikiwa ndio maana watu wengine wanakuwa karibu nawe na kukusaidia
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Najaribu kufikiria mara mbili, saa zingine kuna hali inakutokea hata kulia mtu unaacha unakuwa katika hali ya kawaida sasa kwa situation ya huyu dereva nashindwa kuelewa either kama ndio hivyo mapenzi yamekwisha au vipi ni vigumu kuja na conclusion kwenye ishu kama hii
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndo maana nikasema kila mtu anadeal na mambo tofauti na wewe au mimi.Kama watu wanapofunamiana na kuna watakaoleta fujo...wengine hata hawataangalia nyuma wanaondoka tu.It's all about personal strength!!
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha nilienda kwenye msiba mmoja yule mfiwa alifiwa na mtu wake wa karibu cha ajabu ni kwamba wala alikuwa hatoi machozi hata tone watu wakawa wanashangaa au is that possible kumbe ni mshtuko aliopata kiasi kwamba hata kulia ilikuwa hamna zaidi ya kuwa ni mtu wa kushangaa tu.
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Nilipoona vile ilinitia uchungu sana maana nilikumbuka vile dadangu alifiwa na mumewe mwezi uliopita ambavyo alichanganyikiwa hakuweza kwenda kutoa taarifa kazini sisi tulikwenda kutoa taarifa ndio nikasema au vile wanawake wanakuwa na roho ndogo kuliko mwanaume
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuna faida gani kwenda kuzika afu akarudi kulia njaa na kazi hana?
  Labda boss wake kamnyima ruhusa afanyeje? hasa kama kazi yenyewe aliipata kwa mbinde kweli!

  Cha muhimu ni kwamba mke wake kaondoka,apige kazi huku anaangalia utaratibu wa kazi ingine (kama boss wake hatoi ruhusa) akipata kabla ya kuanza akatembelee kaburi la mkewe!

  Ni maisha tu,sio kila mtu akifiwa anaweza kuruka na ndege kwenda kuangalia mwili wa aliye ondoka,...
   
 15. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hizo feelings sio global feelings,wengine wanaweza vumilia kwa kila jambo na sio kila kitu unalegea tu hadi ubebwe na wewe kama umekua maiti sasa
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Well ukute huyo kaka/baba ana watoto....inabidi yeye kama baba ndo awe jasiri kwaajili ya watoto.Hawezi kujifungia ndani akilia huku watoto nao wanalia.Aliefariki ni mke wake....inawezekana kabisa kwamba bado hajaaccept kwamba mkewe ndo ameshamtoka....yani kuna vitu vingi sana ambavyo vinawafanya watu wareact wanavyoreact in certain situations!!

  BTW ....pole kwa dada!!!
   
 17. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Speaker
  sio kwamba mpaka ulie kiasi hicho ni ile hali ya machungu
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ahh watu bwana....tushazoea yale mayowe hata mengine ya kinafki basi wale watu wa kimya kimya wanaonekana wa ajabu.Ni bora mtu asielia huku anaumia ndani kwa ndani kuliko wanaojifanya kulia sana kumbe ni ilia waonekane tu kwamba na wao walikuwepo!
   
 19. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Asante
  Niliwaona wapo watoto 2 wadogo
  inawezekana hayo unayosema ni kweli
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hayo maandishi ulikuwa unawaandikia sisimizi ndio wasome au binadamu?
   
Loading...