timu yenu ni nzuri ila ina tatizo moja kama kocha atakuwa amelitatua kwenye safari ya uturuki huenda mkafanya vizuri, kama huna macho ya kishabiki na ulikuwa unaangalia vizuri timu yenu ilikuwa na tatizo la kiungo mkabaji pamoja na beki wa kati hata beki wa kushoto naye hakuwa mzuri sana pamoja na kwamba alikuwa anajitahidi kupanda na kupiga krosi nyingi lakini huwa anafanya makosa mengi sana na huwa anachelewa kurudi kusaidia wakati mnaposhambuliwa hasa inapotokea counter attack, na kama hilo tatizo halijatatuliwa itakuwa ngumu sana kuzuia kufungwa mkikutana na timu yenye uchu wa magoli na kwa sababu washambuliaji wenu ni wazuri basi itakuwa kuwahiana atakayewahi kuwa na magoli mengi hadi dakika 90 basi ndo mshindi.
Nikiangalia naona timu zote tatu zina nafasi ya kuchukua ubingwa, ningeweka nne lakini mbeya city nafasi ya wao kuchukua ubingwa ni finyu ukilinganisha na azam, simba na yanga.