UPDATES: US midterm election results

UPDATES: US midterm election results

Wow! Just wow!

This a total repudiation of Trump.

Yaani miaka miwili tu baada ya kurudi madarakani kwa kujenga bonge moja la coalition, leo wapiga kura wa Marekani nao wameongea kwa kukataa kabisa sera za Trump.

Mtu unaahidi kuwa hutaanzisha vita. Baada ya mwaka unaanzisha vita ya kipumbavu inayovuruga uchumi wa dunia, unategemea nini?

Unaahidi utakamata na ku deport wahalifu. Unaingia madarakani unakamata na kuanza ku deport hadi raia! Unategemea nini?

Sidhani kama huu ni ushindi wa Democrats. Huku ni kukataliwa kwa namna Trump anavyoiendesha nchi.

Hivyo Democrats wasidhani kwamba wanakubalika kivile maana na wao walipewa fundisho na wapiga kura 2024 kwa kumchagua Trump.

Wow!
Mtizamo wangu ni kuwa 2024 Wamarekani walimkataa Kamala Harris na sio chama, Maana BIDEN alifanya vizuri kwenye uchumi na kama asingejitoa angeshinda tena, lakini Marekani bado haijawa tayari kwa Rais mwanamke.
Kingine BIDEN alionekana uwezo wake kiafya umeisha na Wamarekani hawakuwa na chaguo lingine. Trump alionekana bora kuliko Kamala, Historia ilionyesha kuwa Kamala amefika pale kwa sababu ya kubebwa na sio uwezo wake.
 
Si wana waiga nyie veggies, km ambavyo mmezoea wizi wa kura. Lol
Vyama havina matawi wala ofisi sehemu kubwa ya nchi halafu mnataka kushindana na CCM,matokeo yakitoka mnadai mmeibiwa, CCM ina wanachama hai 14m
 
Senate and House going blue
Wakipata Senate 67 wanamng’oa Trump
Democrats wana udhibiti wa Senate, lakini bado hawajafikia theluthi mbili inayohitajika kumwondoa Trump.
Kwa mtazamo wangu, ushindi huu ni pigo kubwa kwa Trump. Lakini hata wakifikisha viti 67, bado watahitaji House kupitisha mashtaka na Senate kumtia hatiani kwa theluthi mbili ya maseneta waliopo
 
Vyama havina matawi wala ofisi sehemu kubwa ya nchi halafu mnataka kushindana na CCM,matokeo yakitoka mnadai mmeibiwa, CCM ina wanachama hai 14m
CCM Ilipaswa kugawana na vyama majengo na mali zote zililichumwa na kujenga na Wananchi wakati wa chama kiomja ikiwemo maofisi na viwanja vya michezo, haikufanya hivyo lakini pia sheria ya vyama vingi ilikuwa na mapungufu kiasi cha kuipa nguvu kubwa CCM, Ilipaswa kutengeneza mazingira ya ushindani sawa, ni kama vile sera ya vyama vingi ni udanganyifu tu.
 
Back
Top Bottom