Updates: Mkutano wa Zitto Kabwe Lindi

Updates: Mkutano wa Zitto Kabwe Lindi

Mike zimekubali na mjumbe wa kamati kuu MAMA TERRY anongea....mike zimezingua tena
kidogo anajua kuamasisha anachangamsha kidogo

Anashukuru watu kihudhiria

Huyo si ndiyo alikuwa anaimbisha kipindi cha watoto pale radio moja?
 
Anasema kansa ya nchi ni ufisadi

Anasema inabidi kuwe na sheria Kali na miiko ya viongozi

Kwenye azimio la tabora Luna miiko ya viongozi

Hakuna kuchanganya uongoz wa uma na biashara

Anasema watangaza nia wa ccm wote ni wala rushwa na kila mmoja

Anasema lowassa ajieleze kihusu Richmond

Mwandosya aliharibu pia

Magufil amekula ela ua mabehewa

Membe aeleze juu ya ela za gadafi

Mbona hawajataja walioficha pesa uswis?
 
Ndg zzk anapanda jikwaani

Anasema ni Mara ya kwanza kifanya Mkutano Lindi

Anasema ameitetea sana Lindi na mtwara bungeni

Ansema mikoa hii iko nyuma kimaendeleo

Anasema mungu ametupa utajiri wa gesi ila kuna watu wanawanyonya watu wa Lindi na mtwara

Anasema mtwara ipi ya kuilinganisha na kigoma?
 
Mambo ya kushambuliana kwa vyama vya upinzani sio mazuri na hayatajenga upinzani madhubuti. Zitto na chama chake wanajaribu kuja na aina mpya ya siasa za hoja na sio kelele au maandamano. Watu walio na hoja moja ya ufisadi kila mwaka bila kuwa na mpango au kupendekeza mfumo wa kuondokana na ufisadi ndio wanapiga kelele kwakuwa hawana cha kuwaambia watanzania.

ACT imejifunza kutokana na makosa ya vyama vingine kwa kutokuja na mfumo wa kukifanya kiwe chama cha matukio yaani kusubiri mzee wa nyoka ya makengeza apige ndio wapate cha kuongea.

Umeenda chaka
 
Lindi 26.06.2015

Mwaka 2015 ni mwaka muhimu katika nchi yetu.

Kama ilivyokuwa mwaka 2005 na mwaka 1995 na mwaka 1985 tutakuwa tunapata awamu Mpya ya uongozi. Chama chetu cha ACT Wazalendo kitakuwa kinashiriki uchaguzi kwa mara ya kwanza na tutapenda kuwa na wagombea wenye mwono Mpya kuhusu nchi yetu. Tunataka kutengeneza kada ya wanasiasa wenye mwono chanya kuhusu nchi yetu na wenye kuweza kupambana na ufisadi.

Tumekuwa tukisema siku zote kuwa mwarobaini wa ufisadi kwenye kada ya wanasiasa ni Miiko ya Viongozi. Miiko itamke wazi kwamba kila kiongozi wa umma ni lazima atangaze Mali, Madeni na maslahi yake ya kibiashara akiingia kwenye uongozi na akiwa anatoka. Pia Miiko imzuie Kiongozi kuendesha biashara zake akiwa katika nafasi ya uongozi. Kwa njia hii uongozi wa umma utakuwa ni kwa wale tu wanaotaka kutumikia umma na tutazuia watu wanaotaka kujilimbikizia Mali.

Kutangaza Mali, Madeni na Maslahi pia ni lazima kuendane na uchunguzi wa kuthibitisha matangazo hayo kama ni ya kweli. Hivyo Tume ya maadili ya viongozi lazima iwe na nguvu ya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa umma watakaosema uwongo au hata kuficha maslahi mbali mbali ambayo umma unapaswa kujua.

Kwa mfano kipindi hiki watu wanatangaza kugombea nafasi ya juu kabisa ya nchi yetu tungeweza kwenda kwenye rekodi za wanaotangaza nia na kutazama maslahi yao ili kujua watu hawa watalinda maslahi gani.

Kumekuwa na minong'ono ya dhahiri na ya chini chini dhidi ya watu wanaogombea Urais ambayo lazima wahusika waitolee Maelezo ili wananchi waweze kupembua pumba na Mchele.

Mifano michache;

1) Edward Lowasa hana budi kuwaeleza Watanzania kwa ufasaha kuhusu tuhuma zake katika mchakato wa manunuzi ya kampuni ya kufua Umeme ya Richmond. Mradi huu wa dola 172 milioni ndio uliopelekea yeye kujiuzulu Uwaziri Mkuu. Ndio anasema aliwajibika kwa makosa ya waliochini yake lakini anataka nafasi kubwa sana na yenye nguvu kubwa. Hivyo bila kuelezea uhusika wake katika suala hili wananchi wa Tanzania hawatatendewa haki kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Pia ametamka kuwa yeye ni tajiri na anachukia umasikini lakini hajaeleza utajiri huo ameupataje, ana miliki Mali kiasi gani na ana hisa kwenye kampuni zipi za kibiashara. Habari za chini chini zinasema pia yeye ndiye alikuwa na zabuni ya kusambaza mabomba kwenye mradi wa maji wa Ziwa Victoria kwenda mji wa Kahama akiwa Waziri wa Maji na Mifugo. Edward Lowasa hana budi kuyaweka haya wazi umma ujue.

2) Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali. Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International. Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.

3) John Pombe Magufuli anasifika katika uchapa kazi ingawa hajawahi kuonekana waziwazi kwenye mapambano dhidi ya rushwa. Kwenye kashfa nyingi zilizopata kutokea nchini msimamo wa Magufuli haujulikani alisimama upande upi. Wananchi wana haki ya kupata majibu kutoka kwa Bwana Magufuli kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali. Uporaji mkubwa zaidi wa Mali za nchi kuwahi kutokea katika nchi yetu ni uuzwaji wa nyumba za Serikali. Waziri Magufuli alituhumiwa kwa kuuza nyumba kifisadi kiasi cha hata wadogo zake na watu wengine wasio watumishi wa umma. Wananchi lazima wapate majibu ya mambo haya.

4) Benard Camilius Membe amekuwa akijaribu kuzungumzia ufisadi na nia yake ya kupambana na ufisadi kila apatapo nafasi ya kuzungumza. Hata hivyo anapaswa kuelezea tuhuma dhidi yake kuhusu fedha zaidi ya dola za marekani 20 milioni za mkopo uliorekebishwa kutoka Libya. Suala hili limekuwa likisemwa chini chini na hivyo membe mwenyewe kulipotezea lakini ni jambo lenye kuhitaji Maelezo ya kina kabisa. Msaada huu ulikuwa uwekezwe kwenye kiwanda cha Simenti mkoani lindi ili kuongeza uzalishaji wa simenti nchini na kuongeza ajira kwa Watanzania. Je kiwanda kimejengwa? Je ndugu Membe anahusika vipi na tuhuma hizi kuhusu fedha za Libya? Kwenye nchi zenye misingi thabiti ya uwajibikaji Waziri Membe alipaswa kuwekwa kikaangoni na Bunge kueleza jambo hili. Kwa kuwa anagombea Urais ni muhimu alisemee.

Mifano hii ya wagombea 4 wa CCM inaonyesha dhahiri kwamba nchi yetu inahitaji kuelekeza vita dhidi ya ufisadi kwa kujenga taasisi imara na madhubuti za uwajibikaji. Vinginevyo vita dhidi ya rushwa na ufisadi inakua ni porojo tu za wanasiasa. Wote tuliowainisha hapo juu wamesema katika hotuba zao za kutia nia kuwa watambana na rushwa. Hakuna aliyesema atapambana vipi na rushwa na ufisadi.

Hakuna aliyethubutu kutamka neno Miiko ya Viongozi.Hakuna aliyethubutu kusema ataweka wazi Mali,Madeni na Maslahi yake.

Hata wagombea wa kambi ya upinzani wanatamka kupambana na rushwa lakini hawatamki namna gani watambana na rushwa. Nao pia wanaona aibu kuzungumzia Miiko ya Viongozi. Sisi ACT Wazalendo lazima tuwe tofauti kwa kuteua mgombea Urais ambaye ataweka ajenda ya Miiko kama ajenda kuu na tuseme hivyo waziwazi bila kumung'unya maneno. Hii ndio itakuwa tofauti yetu na vyama vikongwe. Ufisadi hauondolewi kwa maneno matupu. Siasa Mpya ni siasa za uwazi na uwajibikaji. Ni siasa za Miiko ya Viongozi kama ilivyoainishwa kwenye Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha.

Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo
 
Yaan ni ya kizalendo mpaka raha, mtu mmoja asubuh kaja na udaku wake eti ZZK hamsemi Lowasa ksbb ni mfadhili wake-nani anaweza kuja na ushahid hapa kuwa Mbowe na Slaha amewah kuwasikia wanamsema Lowasa? Northern Agenda haiwaruhusu kugombana-wao ni masilahi ya Urais na Rais lazima atoke kaskazin fullstop.
 
Chadema nijanga hutuba makini kabisa ooh eti zitto anatumika mbona kamchana huyo Lowasa hapa bavicha Siasa zenu zachuki hazitowafikisha popote
 
quote_icon.png
By Mtimbo
nyie watu mna matatizo sana na zitto! umeshakili hilo gazeti ni la team lowasa na lipo hapo kimkakati kwa nini usihisi labda sehemu aliyolipuliwa lowasa haikuwekwa hapo,!? hivi unategemea kabisa lowasa asemwe vibaya halafu mhariri wa gazeti hilo aiweke!? kushindwa kwako kuyaona mapungufu haya yote si bure ni dhahiri umesukumwa na chuki zako dhidi ya zitto!

Pia kuna gazeti la majira limemwandika hata Lowassa katika ile orodha, ila wasiwasi wangu nimeona jinsi alivyoandikwa Lowassa inadhihirisha Zitto hamutupii makombora kama anavyofanya kwa wengine, hapa anasema tu auambie umma yaliyojiri kwa kashfa ya Richmond kuwa akanushe kutohusika kwake kisha watendaji wa chini ndo walihusika na si yeye - hii inashiria pengine kuna harufu ya uhusiano kati ya Lowassa na Zitto japo kuna mbinu za kisayansi zinachezwa.

Ni mtizamo wangu.
 
Mod ;
Unganisha picha hizo kwenye habari; mbona ukawa ; Huwa unaunganisha
.
 
Back
Top Bottom