Updates kutoka Manyara: Mary Nagu nusura achomwe Moto.

Huyu bibi amebobea kwa rushwa kumbe Sumeye alimtuhumu ukweli kua kagawa mahela kupata ujumbe wa nec ya ccm
Mary Nagu nusura
achomwe moto akigawa rushwa ya uchaguzi! Ilikuwa hivi, makamanda wa
CHADEMA wakiongozwa na Mbunge wa Karatu, Israel Natse na Mbunge wa Viti
Maalum, Pauline Gekul, walitonywa na askari wa miguu wa Kata ya
Bashanet, kuwa CCM wako mahali wameita watu na kuwafungia ndani ya
nyumba wakiwapatia rushwa ili wamchague mgombea wao.

Makamanda wa Ki-iraq wakapiga yowe kuita wenzao. Nyumba ikazingirwa,
watu wakitaka kuichoma moto, ndani yake akiwemo Nagu na Jitu Soni. CCM
wana hali mbaya sana katika kata hiyo ambapo CHADEMA na mgombea wake,
Lawrence Tara, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, wanakubalika
sana. Polisi kutoka Babati mjini na vijijini ndiyo wamefanikiwa
kumwokoa Nagu alfajiri ya leo, baada ya kuzingirwa usiku kucha.

Muda huu ndiyo Kamanda wa Anga, Mbowe anaelekea kata hiyo ya Bashnet
kwenda kufunga kazi, kisha atakwenda Dongobesh, Makuyuni, kisha Arusha
mjini, Uwanja wa Soweto Kaloleni.

Updates combination Tumaini Makene (Man of the
letters) na Mohamedi Mtoi.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Last edited by a moderator:
RUSHWA ipo kwenye ilani ya CCM,
hivyo kila mwanachama sharti atekeleze ndipo aendelee na ahadi zingine alizoahidi.
 
Huyu bibi amebobea kwa rushwa kumbe Sumeye alimtuhumu ukweli kua kagawa mahela kupata ujumbe wa nec ya ccm

Sumaye na uwanaume wake hakulia bure, alilia akijua alichofanyiwa, akajua atamfanyia kila mtu namna alivyo fanya.

Hawahawa wakipanda majukwaani husema rushwa adui wa haki. very pathetic!
 
Natamani kujua huyo mama alijiteteaje baada ya kusurika,unafungiwa usiku kucha ndani hata sijui kwa mumewe aliaga anakwenda wapi......

Mimama sampuli hii inakuwaga na ndoa za kichina. Vidoleni pete kibao nyumbani kila mtu na chumba chake
 
du hivi takukuru ipo kweli? au ndo inawaza kuhusu rasimu mpya? rushwa ni adui wa maendeleo, watu wa dongobesh msikubali kununuliwa mtajuta.
 
RUSHWA ipo kwenye ilani ya CCM,
hivyo kila mwanachama sharti atekeleze ndipo aendelee na ahadi zingine alizoahidi.
Tena kwenye ilani yao kuna hadi rushwa ya ngono. Ndio maana wanapinga kutolewa kwa VITU maalum kwenye katiba
 
Duh.Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa.Nassary kawakurupusha CCM wanagawa kitu kidogo.HECHE naye kawakurupusha wakigawa kitu kidogo.Leo sangara mkubwa anusurika kuchomwa moto akigawa kitu kidogo.Sasa ni kitu gani kimebaki kama Nagu mwenyewe ambae yuko kwenye chungu cha mkuu wa kaya anafanya hivyo.Hii ni ishara ya mkuu wa kaya kuwa na yeye yuko hivyo.
 
Kama wamemuacha Mary Nagu bila kumchanja hata chale moja kwenye makalio yake watakuwa hawajamtendea haki kabisa. Watoa rushwa huko ccm wanazidi kuongezeka na ili kuwakomesha na kuikomesha rushwa inabidi wawe wanashughulikiwa hapo hapo wanapokamatwa kwakuwa Takukuru wame-prove failure katika kukabiliana na rushwa.
 
Huyu Mama ana uzoefu wa kugawa rushwa muulizeni Fedrick Tluway Sumaye alikoma ubishi.
 
sera za CCM hivi sasa haziuziki mbele ya wananchi, rushwa na vyombo vya dola ndio mkombozi wa CCM wakati wa uchaguzi.
tukumbuke pia huyu Mama Nagu alilalamikiwa na Rose Kamili kucheza rafu wakati wa uchaguzi jimbo la Hanang mwaka 2010.

na huyu ndio miongoni mwa mawaziri wanaomsaidia rais!
 
Back
Top Bottom