Updates kutoka Manyara: Mary Nagu nusura achomwe Moto.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Mary Nagu nusura achomwe moto akigawa rushwa ya uchaguzi! Ilikuwa hivi, makamanda wa CHADEMA wakiongozwa na Mbunge wa Karatu, Israel Natse na Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul, walitonywa na askari wa miguu wa Kata ya Bashanet, kuwa CCM wako mahali wameita watu na kuwafungia ndani ya nyumba wakiwapatia rushwa ili wamchague mgombea wao.

Makamanda wa Ki-iraq wakapiga yowe kuita wenzao. Nyumba ikazingirwa, watu wakitaka kuichoma moto, ndani yake akiwemo Nagu na Jitu Soni. CCM wana hali mbaya sana katika kata hiyo ambapo CHADEMA na mgombea wake, Lawrence Tara, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, wanakubalika sana. Polisi kutoka Babati mjini na vijijini ndiyo wamefanikiwa kumwokoa Nagu alfajiri ya leo, baada ya kuzingirwa usiku kucha.

Muda huu ndiyo Kamanda wa Anga, Mbowe anaelekea kata hiyo ya Bashnet kwenda kufunga kazi, kisha atakwenda Dongobesh, Makuyuni, kisha Arusha mjini, Uwanja wa Soweto Kaloleni.

» Kamanda Mbowe amemaliza mkutano wa Bashnet sasa ngoma Dongobesh, Mbulu. Kama ilivyokuwa jana Muheza ambako mikutano ya CCM na CUF ilikufa kwa watu kwenda kusikiliza mikutano ya CHADEMA, leo pia mkutano wa CCM hapa Bashnet umekufa, watu wamekimbilia kumsikiliza Mbowe.

• Mwenyekiti ametoa kauli nzito hapa Bashnet akionya mchezo mchafu wanaofanya CCM Monduli wa kuanza kukodi vijana ili wakawafanyie fujo watu wa CHADEMA, amesema kama vijana wa CHADEMA nao watapewa amri ya kulipiza matendo ya CCM itakuwa ni songombingo ambayo itaharibu nchi.

• CHADEMA hawako tayari kuona damu ya Mtanzania yeyote ili mtu mmoja awe diwani, lakini kwa mambo ya CCM kuanza kufanya vurugu huku vijana hao wakilindwa na polisi, itafika mahali haitakubalika! Amesema ''vijana wa CCM nchi nzima ni 10% wakati wale wa CHADEMA ni 90%, amewataka waache mara moja.

• Nape amepita hapa nusu saa kabla Mkiti Mbowe hajatua, watu walimzomea. Walikuwa na wapambe na masare yao. Mbowe alipofika, wananchi wachache waliokuwepo kwenye mkutano wake wakaondoka kwenda CHADEMA.

» More update

• Tunatoka Kata ya Makuyuni, sehemu inaitwa Mbuyuni. On the way to A-City kwa ajili ya kata nne za mjini. Finalization. We are so hopeful here. Lowassa is so desperate than ever before. Ametafuta yale magari makubwa ya kubeba ng'ombe kwenda Dar, ili kusomba watu hadi kutoka Meru. Bado 'imebuma'. Ajiandae kwa goli la nne. Goli la kwanza: alimleta Batilda Buriani Arusha mjini, akapigwa, akamleta mkwe wake Sioi, Arumeru Mash., akapigwa, akamleta mtu wake pale Daraja Mbili, udiwani, akapigwa, kesho akipigwa ni goli la nne.

• Helkopta inarusha vipeperushi hapa mjini Makuyuni. Tunaitafuta Arusha. Dogo janja kakabidhiwa majukumu hapa. Anasema amekuwepo kwa wiki 2 sasa, makamanda wamefanya kampeni ya nyumba kwa nyumba, mtu kwa mtu. Mbowe amesema uchaguzi huu unakwenda kuwa kielelezo kingine cha Watanzania kukataa udhalimu wa watawala na kujiandaa kuwaondoa kabisa madarakani 2014-2015.

Updates combination Tumaini Makene (Man of the letters) na Mohamedi Mtoi.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Last edited by a moderator:
Hao wamebakiza kuanza kudondoka mmojammoja kwa stroke, jinsi mambo yao yanavyobuma!??
 
Natamani kujua huyo mama alijiteteaje baada ya kusurika,unafungiwa usiku kucha ndani hata sijui kwa mumewe aliaga anakwenda wapi......
 
Hao wamebakiza kuanza kudondoka mmojammoja kwa stroke, jinsi mambo yao yanavyobuma!??'
 
Kama nchi hii inamfumo wa vyama vingi, na hili swala limethibitishwa bado kuna uhalali gani wa CCM kupewa nafasi ya kugombea? bwana mwanya Tendwa anafanya kazi gani? Tatizo nchi imeisha kuwa kama ya vikatuni, hili ni swala zito lakini inakuwa kama ni kakichekesho kidogo, baada ya hapo Mary Nagu goes free ili sakawatukane wapinzani bungeni
 
Maji yamewafika shingoni.
Bila rushwa hakuna ccm.
Na sasa kama katiba mpya ikiamua viti maalum kuondolewa sijui watakula wapi.
Chonde chonde CDM tuwe makini kesho wasije kuomba uanachama tukawakubalia.
Huu ni uozo wa ccm acha wabaki nao.
Umekuwa mchezo wa watoto wa Kidali pooo walale nacho!
 
Hawa jamaa wa cdm vurugu zote wanafanyia arusha na kuua utalii ila moshi hawafanyi vurugu watu wa arusha tujitambue katika ili
 
Ni nani aliye msafi hapa bongo ndani ya ccm wa kukemea rushwa? Kinana jangiri au mwenyekiti wao? Hamna,nchi ishakuwa cha mwendawazimu.
 
Huyu Nagu anajisahau sana,kumbe alidhania ni uchaguzi wa ndani wa ccm du hata Sumaye alivyo lalamika kuhusu huyu mama kugawa rushwa ni kweli,makamanda wengemgeuza kitoweo people are serious na hii nchi yeye anagawa pesa ovyo wakati,hospital hatuna madawa,ovyo kweli.
 
Back
Top Bottom