Wakuu salam.
Niliwahi kuja humu mara kwa mara kujibu hoja za watu kuhusu swala la
Ruhazwe JR na zawadi za miss chitchat 2012 na nikaahidi kuleta mrejesho hapa mara baada ya kurudi na kuwasiliana na muhusika. Sasa basi kuhusu swala la mkuu
Ruhazwe JR kutokupatikana mara baada ya mshidi kupatikana ni kweli kwamba aliugua an kulazwa hospitalini kwa hiyo alipotea ghafla humu jamvini.
Kwa sasa hali yake ni nzuri kiafya japokuwa hakuweza kurejea tena ghafla kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wake nazo ni matatizo ya kifamilia ambayo yamesababisha yeye kwenda huko mkoani ili ku respond matatizo hayo na mimi niliporejea nyumbani nilikuta hali hiyo bado ipo hivyo inabidi niungane naye kwenda mkoa ni kwa sababu hiyo.
Kuhusu Zawadi.
Kuhusu zawadi za Miss Chit chat niliwasiliana naye na kwakuwa sasa hivi ninaungana naye kurespond hiyo issue naahidi baada ya hili swala kuisha nitarejea Dar es Salaam na nitawasiliana na
charminglady ili nimpe Zawadi zilizokuwa zimeahidwa na yeye mwenyewe
Ruhazwe JR na mimi nilizoahidi kwa wadau wengine wailoahidi naomba wampe
charminglady pia. Nitarejea tar 30 mwezi huu
Naomba radhi kwa wadau wa white party kwa hiyo tarehe sitahudhuria kama nilivyokuwa ninapenda iwe.
kama kuna mwenye Swali aulize hapa hapa jamvini
Copy to
charminglady Mtambuzi Madame B Remmy figganigga Arushaone washindi wote wa Miss Chit Chat na wadau wengine wote.