Sifahamu takwimu hizi wanazi toa wapi au mbinu zilizo tumiwa kufikia taarifa hizo lakini dawa ambazo zinatoka MSD kwenda kwenye hospitali za serikali hazi toshi kwa namna ya idadi na namna ya kutibu magonjwa tofauti tofauti.
Matibabu ya watoto chini ya miaka mitano, wazee waliozidi miaka 60 na wenye presha na kisukari huwa ni bure lakini ukiangalia dawa zilizopo kwa wagonjwa hawa na ulinganishe na wanaotibiwa kwa bima ya afya (NHIF), utagundua kwamba tofauti ipo kubwa sana.
Siamini kwamba afya inaweza kuwa bure kwa wananchi wote. Bima ya afya iboreshwe na wananchi wawezeshwe kuwa na bima.