India kushirikiana na Tanzania katika upatikanaji wa dawa za bei nafuu

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
Serikali ya India na Tanzania zimekubaliana kushirikiana katika upatikanaji wa dawa za gharama nafuu ili kuwezesha wananchi kumudu na kupata dawa hizo kwa gharama nafuu zaidi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kukutana na kufanya kikao na Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa India Mansukh Mandaviya Jijini New Delhi India.

Katika kikao chao kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa Sekta ya Afya Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora ni agenda muhimu kwenye ziara yake ambapo Viongozi hao wamejadili kwa kina fursa za uwekezaji nchini Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za dawa ndani ya Tanzania hasa kwa kuwa asilimia 60 ya dawa na bidhaa za afya nchini Tanzania zinanunuliwa kutoka India, huku pia soko la dawa linagusa hadi nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Afika Mashariki na Nchi za SADC, unafuu wa bei za dawa utasaidia kufikia watu wengi zaidi na hivyo kuwawezesha kupata tiba.

“Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano zaidi katika maeneo mbalimbali na Serikali na Wadau wa Sekta ya Afya kutoka India kwenye utoaji wa huduma za ubingwa bobezi kufuatia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya Afya ambapo tumeshuhudia kuanza kutolewa kwa huduma za kibingwa ikiwemo upandikizaji wa Uloto (Bone marrow transplant), Upandikizaji Figo (Kidney transplant), upandikizaji wa vifaa vya usikivu ( Cochlea Implants), upasuaji wa moyo na mishipa ya fahamu” amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy ameiomba Serikali ya India kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia programu ya kubadilishana ujuzi na kutoa mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya muda mrefu ili kuongeza wataalam wa ubingwa ubobezi nchini Tanzania, matumizi ya TEHAMA katika huduma za afya, usafi wa mazingira na masuala ya ulaji wa vyakula bora ili kukabiliana ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa upande wake Waziri Mansukh Mandaviya ameshukuru kutembelewa na Waziri Ummy Mwalimu na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika kuboresha Sekta ya Afya kuanzia kwenye uzalishaji, upatikanaji wa dawa bora kwa bei nafuu kwa ajili ya manufaa ya nchi zote mbili.

Waziri Ummy Mwalimu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku 5 nchini India kufuatia Mwaliko wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa India Mhe. Mansukh Mandaviya. Akiwa India Waziri Ummy anatarajiwa kukutana na kufanya vikao mbalimbali na Wadau wa Sekta ya Afya na kuvutia ushirikiano baina ya Tanzania na wawekezaji hao wa kimataifa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya nchini Tanzania.
IMG-20230726-WA0001.jpg
IMG-20230726-WA0005.jpg
IMG-20230726-WA0001.jpg
IMG-20230726-WA0000.jpg
IMG-20230726-WA0003.jpg
IMG-20230726-WA0004.jpg
 
Serikali ya India na Tanzania zimekubaliana kushirikiana katika upatikanaji wa dawa za gharama nafuu ili kuwezesha wananchi kumudu na kupata dawa hizo kwa gharama nafuu zaidi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kukutana na kufanya kikao na Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa India Mhe. Mansukh Mandaviya Jijini New Delhi India.

Katika kikao chao kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa Sekta ya Afya Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora ni agenda muhimu kwenye ziara yake ambapo Viongozi hao wamejadili kwa kina fursa za uwekezaji nchini Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za dawa ndani ya Tanzania hasa kwa kuwa asilimia 60 ya dawa na bidhaa za afya nchini Tanzania zinanunuliwa kutoka India, huku pia soko la dawa linagusa hadi nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Afika Mashariki na Nchi za SADC, unafuu wa bei za dawa utasaidia kufikia watu wengi zaidi na hivyo kuwawezesha kupata tiba.

“Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano zaidi katika maeneo mbalimbali na Serikali na Wadau wa Sekta ya Afya kutoka India kwenye utoaji wa huduma za ubingwa bobezi kufuatia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya Afya ambapo tumeshuhudia kuanza kutolewa kwa huduma za kibingwa ikiwemo upandikizaji wa Uloto (Bone marrow transplant), Upandikizaji Figo (Kidney transplant), upandikizaji wa vifaa vya usikivu ( Cochlea Implants), upasuaji wa moyo na mishipa ya fahamu” amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy ameiomba Serikali ya India kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia programu ya kubadilishana ujuzi na kutoa mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya muda mrefu ili kuongeza wataalam wa ubingwa ubobezi nchini Tanzania, matumizi ya TEHAMA katika huduma za afya, usafi wa mazingira na masuala ya ulaji wa vyakula bora ili kukabiliana ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa upande wake Waziri Mansukh Mandaviya ameshukuru kutembelewa na Waziri Ummy Mwalimu na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika kuboresha Sekta ya Afya kuanzia kwenye uzalishaji, upatikanaji wa dawa bora kwa bei nafuu kwa ajili ya manufaa ya nchi zote mbili.

Waziri Ummy Mwalimu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku 5 nchini India kufuatia Mwaliko wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa India Mhe. Mansukh Mandaviya. Akiwa India Waziri Ummy anatarajiwa kukutana na kufanya vikao mbalimbali na Wadau wa Sekta ya Afya na kuvutia ushirikiano baina ya Tanzania na wawekezaji hao wa kimataifa kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya nchini Tanzania.View attachment 2699304View attachment 2699305View attachment 2699306View attachment 2699308View attachment 2699309View attachment 2699307
Wake kujenga viwanda badala ya kuongea porojo.Tuliqmbiw apolo hospital itajeng kampasi Dar Hadi Leo kimya.
 
Back
Top Bottom