Upasuaji wa urembo wazua gumzo mtandaoni

Upasuaji wa urembo wazua gumzo mtandaoni

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
115
Reaction score
176
Muonekano wa hivi karibuni wa rapa mkongwe wa Marekani Lil’ Kim umezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionyesha wasiwasi na wengine wakikosoa tabia ya wanawake kukataa miili yao na kutaka miili ama maumbo mengine ambayo huishia kuwaletea madhara.

Video na picha za Lil’ Kim kutoka katika tukio la hivi karibuni zilisambaa kwa kasi, na kusababisha maoni mengi kuhusu mabadiliko ya sura yake.

Cosmetic Surgery imekuwa habari ya mjini karibu ulimwengunu pote, wanawake wamekuwa wakifanya upasuaji wa urembo kutaka maumbo ambayo wanayaona yanawafanya waonekanane bora na wazuri.

Soma zaidi:Madaktari wa China wanawasaidia wagonjwa kupata nafuu kupitia upasuaji wa uvamizi mdogo

Lil’ Kim amekuwa akikabiliwa na mijadala kuhusu muonekano wake kwa miaka mingi. Mwaka 2013, mwakilishi wake alikosoa ripoti iliyoutaja uso wa rapa huyo kuwa umeharibika, akisema lugha hiyo ilikuwa ya kikatili na ya kukosa heshima.
images.jpg


Mjadala wa sasa, hata hivyo, umeibua suala pana zaidi kuhusu usalama wa taratibu za urembo. Upasuaji wa urembo na taratibu zisizo za upasuaji, ikiwemo sindano za kujaza ngozi, zinaweza kufanywa kwa usalama chini ya wataalamu wenye sifa, lakini hazikosi hatari.

Shirika la Chakula na Dawa la Marekani, FDA, linaonya kuwa sindano za kujaza ngozi zinaweza kusababisha maumivu, uvimbe, maambukizi, makovu, uvujaji wa dawa, vinundu na athari za tishu.

Katika matukio machache lakini makubwa, dawa inaweza kuingia katika mshipa wa damu na kusababisha kufa kwa tishu, kupoteza uwezo wa kuona au kiharusi.
 
Hizi cosmetic surgery hazifai
Miaka mbeleni lazima zitakuathiri
Huwezi shindana na nature

Ova
 
🙆‍♂️😫👦🙅‍♂️🙅‍♂️
 
Back
Top Bottom