Upanuzi wa barabara jijini Mwanza

Upanuzi wa barabara jijini Mwanza

Taeyong

Senior Member
Joined
Sep 29, 2019
Posts
169
Reaction score
218
Habari zenu wanaJF, natumaini nyote mnaendelea na pirika za kila siku kwa ajili ya familia na ujenzi wa taifa.

Twende kwenye hoja yangu direct! Swali langu ni kwamba "Ni lini serikali itapanua barabara hizi muhimu zinazounganisha Mwanza mjini na maeneo kuanzia Usagara hadi mjini kati na Kisesa hadi mjini kati ili ziwe na njia nne (mbili kwenda na mbili kurudi) ili kupunguza msongamano unaozidi kila siku?

Hili ni swali linalowakilisha hisia za wananchi wengi wanaotegemea barabara hizi kwa shughuli za kila siku, ikiwemo biashara, usafiri na huduma za kijamii.

Barabara hizi zimekuwa na ongezeko kubwa la magari na watu kutokana na ukuaji wa haraka wa mji wa Mwanza na maeneo ya pembezoni kama Igoma, Usagara na Kisesa. Hali hii imesababisha foleni kubwa kunapotokea ajali kidogo tu, ucheleweshaji wa safari na wakati mwingine hatari kwa watumiaji wa barabara, hasa waenda kwa miguu na waendesha bodaboda.

Upanuzi wa barabara hizi kuwa na njia nne (dual carriageway) utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano, kuongeza usalama wa barabarani na kurahisisha mzunguko wa shughuli za kiuchumi. Miundombinu bora ya barabara pia itaongeza thamani ya maeneo husika na kuchochea maendeleo ya haraka na kufanya kuwa jiji lenye hadhi.

Ni wazi kuwa uwekezaji katika miundombinu ya barabara si anasa bali ni hitaji la msingi linalokwenda sambamba na ukuaji wa miji. Serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa mipango ya upanuzi wa barabara inaendana na kasi ya ongezeko la watu na magari ili kuepuka changamoto zinazoshuhudiwa sasa.

Kwa hiyo, wananchi wanaendelea kuomba na kutarajia kuona mipango ya haraka ya kupanua barabara hizi muhimu kuwa za njia nne, ili kuleta usafiri salama, wa haraka na wenye ufanisi zaidi katika jiji la Mwanza na viunga vyake.
Nawasilisha👏
 
Da

ANgekuwepo na imani zingekuwa zimepanuliwa, ni aibu barabara kuu za kuingilia jijini mwanza kuwa na njia 1.
Siku nyingi tu! Maajabu alofanya kwenye daraja la busisi hakuna mtu angewaza huko hata siku moja!
 
Dual carriageway ya Usagara walishatangaza tender.

Hiyo ya Kisesa nadhani bado bila bila. Walipata vichenchi vya mafuriko wakapanua eneo la Mabatini tu.
 
Umaskini wa Mwanza unachochewa na kucheleweshwa kwq maendeleo

Ni aibu kwa jiji ETI la pili kwa ukubwa Tanzania
 
Siku nyingi tu! Maajabu alofanya kwenye daraja la busisi hakuna mtu angewaza huko hata siku moja!
Natumaini mamlaka wataliangalia hili kwa makini kwa maaana jiji la Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa na ukuaji nchini kwetu hivyo linapaswa kuwa na miundombinu bora.
 
WAtu wajiji wanapaswa jiuzulu

Mwanza ni kama hatulipagi kodi miaka ypte, ni kama wananchi hatupo vile
Maji, Barabara na umeme bado ni changamoto
Yaani ni ujingaujinga tu
2F91957F-980B-43A2-8D54-D983831AC5D9.jpeg
 
Natumaini mamlaka wataliangalia hili kwa makini kwa maaana jiji la Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa na ukuaji nchini kwetu hivyo linapaswa kuwa na miundombinu bora.
Huenda! Jiji linapanuka kwa kasi na wao hawaoni! Watashtukia tu tumezidiwa wakati huduma ziko palepale!
 
Dual carriageway ya Kisesa walishatangaza tender.

Hiyo ya Kisesa nadhani bado bila bila. Walipata vichenchi vya mafuriko wakapanua eneo la Mabatini tu.
Natumaini watapanua mpk kisesa itakua jambo kubwa sana maana barabara ni finyu sana sema kweli.
 
Back
Top Bottom