Upagani na wapagani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,652
729,707
Kwa vyovyote unaposikia neno pagan unapata picha ya watu fulani wenye roho mbaya waabudu shetani na watu wenye Rohombaya sana.

Lakini kiasili na kiuhalisia upagani ni imani kubwa ndani ya mwamvuli wenye imani ndogo ndogo nyingi zisizoamini katika Mungu mmoja huku wakiamini katika miungu na dini za asili.

Ndani ya hizo imani kuna baadhi huchanganywa na satanism na freemason, ambapo ndani yake hufanya ibada za kafara.

Leo ningependa kuzungumzia upagani wenye utu kwakuwa nimeishi nao kwa miaka mitatu mfululizo...hii ni aina ya imani ya kipagani isiyo na mafungamano na ule upagani wenye misimamo mikali ni upagani wenye kujali utu na kujituma zaidi kwenye ustawi wa jamii na self cultivation kwenye ulimwengu wa kiroho kwa tafsiri ya kipagani.

Huu ni upagani wenye kujali elimu maarifa ugunduzi na uvumbuzi mpya kwa manufaa ya jamii na dunia kwa ujumla huku wakijiepusha kwa mbali kabisa na malumbano juu ya uwepo wa Mungu mmoja.

Imani hii ya kipagan ni watu wakimya wataratibu wenye tafakuri kwenye kila jambo hawakurupuki na hata mnapofanya jambo la pamoja na ikafika mahali hakuna ufumbuzi hukuuliza wewe mwamini uongee na Mungu wako.

Kupitia kwao niliweza kujifunza mengi ya manufaa...hapa jamvini tuna wapagani wengi je ni wapagani wa sect ipi mojawapo?
 
Hiki kinachoitwa morden paganism si chochote si lolote bali ibada na matambiko vyenye muungano wa moja kwa moja na satanism na imani za giza zenye viapo na maagano
1454777320794.jpg
1454777328743.jpg
1454777335103.jpg
1454777339994.jpg
1454777346283.jpg
 
Naomba kuuliza , ninaishi na mtoto wa dada angu ambaye alipotea miaka mingi hatujui kama yuko hai ama alikufa, ila mwanae anatabia mbaya sanaaaaa anamiaka 16 binti ila anapenda wanaume kupita kiasi. Nimchonganishi kuliko chochote, hakuna anaemtaka wala kumuitaji, baba ake bibi zake pandembili wala majirani sababu tuu ya tabia zake. Yaaani kifupi kuishi nae nikujitwika jukum moja kubwa sanaaa. Point ni kwamba nilitaka kwenda kwa mganga nimuulizie tatizo ninini mbona yupo hivyo?. Je! Ntakua nimejiingiza katika ushilikina? Coz sijawahi fanya kituhicho nina 30 na nimeolewa , msaada wako mshana pleasss
 
Kwanza kupotea kwa mamaake kuna mahusiano makubwa na tabia zake za sasa...na hilo swala la ngono ni pepo mahaba limemuingia na pepo la uchonganishi pia. ..
Sikushauri sana uende huko mpaka uwe na hakika ya mtu unayemwendea kwakuwa kuna wapigaji kila kona siku hizi
Ishu kubwa hapo ni kujua mwisho wa mamaake ulikuwaje. ..kuna mengi mno kwenye hii ishu lakini chanzo kiko kwa mzazi
 
Naomba kuuliza , ninaishi na mtoto wa dada angu ambaye alipotea miaka mingi hatujui kama yuko hai ama alikufa, ila mwanae anatabia mbaya sanaaaaa anamiaka 16 binti ila anapenda wanaume kupita kiasi. Nimchonganishi kuliko chochote, hakuna anaemtaka wala kumuitaji, baba ake bibi zake pandembili wala majirani sababu tuu ya tabia zake. Yaaani kifupi kuishi nae nikujitwika jukum moja kubwa sanaaa. Point ni kwamba nilitaka kwenda kwa mganga nimuulizie tatizo ninini mbona yupo hivyo?. Je! Ntakua nimejiingiza katika ushilikina? Coz sijawahi fanya kituhicho nina 30 na nimeolewa , msaada wako mshana pleasss
Ndio Mi nnavyo faham sister ukijihusisha tu na mambo ya waganga tayari we ni mshirikina.
 
Dunia ina mengi mpagan naye atakushangaa kwa kile unachoamini
Kiongozi duh nitakuua mwaka huu samahani natoka kidogo ktk mada ila inauhusiano na haya ya upagani.kuna mtu siku moja ktk maongezi alisema alienda india kwa duka la sonara akataka peta ya dhahabu yule kuhindi akamuuliza siku na mwezi wa kuzaliwa alipomtajia akamkataza maisha yake yote kuvaa dhahabu badala yake akamshauri kuvaa silver . Alipomuuliza akamwambia watu hawajui lakini si vzr kuvaa vito usivyojua kama vinakuletea mkosi kwako au baraka.wengine huvaa cheni zenye mawe au madini kumve huvaa mikosi. Kila mtu ana kitu ambacho kwake ni baraka na vingine mikosi.
Speaking of that nikaanza kusearch for that particular knowledge ila nimepata ugumu hivyo vito vina majina magumu n mostly havijulikani ikiwa unayo chart inayoonesha au hata link ktk akiba yako library utueleweshe kipi ni laana na mkosi kwa nani tubadilishane mawazo juku na kimi nikiendelea kutafutatafuta.
Toka siku hiyo nikawa muoga sana kuvaa madude ovyo. Umeona cheni imewekewa urembo au nawe ya rangirangi nitaitazama na kuiacha hapohapo.
 
Katika hizo imani za kipagan kuna
1.za kuzaliwa nazo
2. Za kuja kubadilika ukubwani
3. Za kuiga na kufuata mkumbo
4.kutokana na mazingira
5.maslahi kama utajiri ndoa elimu na vyeo

Mkuu ongezea nyama kwenye hayo makundi!

Inawezekana vipi mtu kazaliwa na upagani ?
Hayo mengine yanawezekana lakini hili la kuzaliwa nao umeniacha njia panda!
Unataka kusema hata Uchawi wengine ni wakuzaliwa nao?
 
Kiongozi duh nitakuua mwaka huu samahani natoka kidogo ktk mada ila inauhusiano na haya ya upagani.kuna mtu siku moja ktk maongezi alisema alienda india kwa duka la sonara akataka peta ya dhahabu yule kuhindi akamuuliza siku na mwezi wa kuzaliwa alipomtajia akamkataza maisha yake yote kuvaa dhahabu badala yake akamshauri kuvaa silver . Alipomuuliza akamwambia watu hawajui lakini si vzr kuvaa vito usivyojua kama vinakuletea mkosi kwako au baraka.wengine huvaa cheni zenye mawe au madini kumve huvaa mikosi. Kila mtu ana kitu ambacho kwake ni baraka na vingine mikosi.
Speaking of that nikaanza kusearch for that particular knowledge ila nimepata ugumu hivyo vito vina majina magumu n mostly havijulikani ikiwa unayo chart inayoonesha au hata link ktk akiba yako library utueleweshe kipi ni laana na mkosi kwa nani tubadilishane mawazo juku na kimi nikiendelea kutafutatafuta.
Toka siku hiyo nikawa muoga sana kuvaa madude ovyo. Umeona cheni imewekewa urembo au nawe ya rangirangi nitaitazama na kuiacha hapohapo.
Iron Lady haya mambo mengine ni mapokeo tamaduni mila na desturi.. Kwa imani yako ya sasa angalia kitu fulani inasemaje... Wahindi ni waabudu miungu kwahiyo wana hayo mambo kwa Sana tuu....
Kwa wanaomuamini Mungu mmoja dhahabu sio kitu kibaya bali epuka kuvaa Pete na vidani vyenye nembo majina na rangi za ajabu ajabu
 
Mkuu ongezea nyama kwenye hayo makundi!

Inawezekana vipi mtu kazaliwa na upagani ?
Hayo mengine yanawezekana lakini hili la kuzaliwa nao umeniacha njia panda!
Unataka kusema hata Uchawi wengine ni wakuzaliwa nao?
Ndio kuna baadhi ni wapagani tangu kuzaliwa hajui chochote kuhusu kanisa wala msikiti wala Mungu mkuu
Kwenye Uchawi kuna watoto wa kichawi tangu kutungwa kwa mimba
 
Back
Top Bottom