Hafla ya Ugawaji wa Tuzo za Ballon d’Or 2023

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,125
Usiku wa leo, kuanzia saa 3:00 usiku kutakuwa na hafla ya ugawaji wa Tuzo za Ballon d'Or pale katika ukumbi wa Theatre du Chatelet jijini Paris.

Katika hafla hiyo, kutakuwa na mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanaume na upande wa wanawake.

Vilevile, kutakuwa na tuzo ya golikipa bora wa mwaka, mshambuliaji bora wa mwaka na tuzo ya mchezaji bora chipukizi chini ya miaka 21.

Gumzo kuu ni kati ya vinara wawili ambao ni Lionel Messi ambaye ametwaa Kombe la Dunia pamoja na Erling Haaland ambaye ametwaa mataji makubwa matatu (treble).

Pia kutakuwa na tuzo ya timu bora ya mwaka. Hafla hiyo itakuwa mubashara kupitia DStv. Tutakuwa mubashara.
 
Mbappe kwenye red carpet
IMG_8581.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom