Uongozi wa Simba SC tafadhali semeni tu Ukweli kuhusu Mchezaji Jonas Mkude kwani haumwi kama ambavyo mnatudanganya

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,037
Binafsi nimeshatonya nini kinaendelea dhidi yake na alifanya nini huko ( kule ) Niger ila nyie mnaficha na Kufanya Siri ili tu kutozua Taharuki kwa Mashabiki na Kuwagawa Wachezaji.

Kwa Kujiamini kabisa tena 100% GENTAMYCINE nasema Kiungo wa Simba SC Jonas Gerald Mkude haumwi kama ambavyo mnatudanganya Wiki hii ya Pili sasa bali ni tatizo la Kinidhamu na Kimaadili amelifanya.

Tafadhali tumeshamchoka japo binafsi nilimpenda na nampenda kutokana na Kipaji chake Kikubwa cha Kucheza Mpira ila sasa imetosha na Msimu huu ukimalizika tu achacheni nae na kama anataka kwenda Kucheza Yanga SC ambako tunayemjua tokea akiwa anacheza Kinondoni Biafra, Kawe, Simba B na hadi ya Wakubwa basi aende tu kwani ameshatukinai na Nidhamu yake mbovu na Maadili yake ni mabaya.

Kuna za chini chini ( ambazo si nzuri nimezipata ) hivyo nangoja kuona kama kuna JF Members wengine hapa Watu wa Mpira ( hasa Wapenzi wa Simba SC ) kama nao wamezipata.

Simba SC endeleeni tu Kutuficha sawa?
 
Ni kweli bhana, ile mechi ya Niger alikua jukwaani kwa kumuona tu sio mtu mgonjwa. Kuna shida wanaificha.
 
Pini ( Uchawi ) aliopigwa ni ule ule ambao alipigwa nao Kotei na Fraga na msitegemee tena Lwanga kurudi kuwa kama mwanzo. Dogo anapiga Pini ( Miba ) ya maana kutoka huko Kwao Milimani Uluguruni Mkoani Morogoro.
Hili ni kweli, ila Lwaga kapona,, nazani labda hapagwi sababu ya fitness tu.
 
Back
Top Bottom