Stan Mashamba
JF-Expert Member
- Apr 22, 2020
- 3,184
- 2,471
Tuone kama leo wata kataka matangazo ya CCM kama viongozi wa CCM watasema vibaya wapinzani. Kwa kweli kitendo cha TBC jana kukatakata hotuba za viongozi wa CDM kilikuwa kinawaudhi sana wasikilizaji. Nilishukuru sana kutimuliwa.Nianze mada yangu kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 18(1) nayo inasema hivi "Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi na pia uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na mtu yeyote" mwisho wa kunukuu.
Hebu sasa tutazame nini kilitokea kule Zakheim Mbagala katika ufunguzi wa kampeni zake chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA.
Watangazaji wa TBC walifika "kwa shingo upande" katika uwanja huo kwa nia ya kuonyesha LIVE matangazo hayo.
Nini kilitokea katika urushaji matangazo hayo?
Wasikilizaji wa TBC walibaini kukatwa katwa kwa matangazo kwa matangazo hayo.
Ndipo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa alipoamuru watangazaji hao "wafungashe virago" vyao na waondoke uwanjani hapo katika muda wa dakika 15!
Wapo wananchi wanawalaumu viongozi wa CHADEMA kuwa eti kitendo chao hicho kilikuwa si cha kiungwana!
Hapo hapo TBC wakatoa taarifa ya kulaani kitendo cha kufukuzwa "kinyama" watangazaji wake kwenye ufunguzi wa kampeni hizo.
Hebu turejee katika utangazaji wa TBC katika kipindi chote hiki cha utawala wa serikali ya awamu ya 5, bila shaka hata mtoto mdogo anayesoma chekechea atakuwa anajua kuwa TBC imejigeuza kuwa kama televisheni ya CCM, kwa kutangaza "sifa na mapambio" kwa serikali hii ya CCM, chini ya kiongozi wake Rais John Magufuli.
Hata hivyo TBC ni chombo cha Umma na hakipaswi "kuhodhiwa" na chama chochote cha siasa na kinapaswa kitoe "airtime" iliyo sawa kwa vyama vyovyote vya siasa nchini, bila kufanya upendeleo wowote, kwa kuwa sisi wananchi walipa kodi, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tunaoiendesha TBC
Nini kilitokea jana?
Ni dhahiri kuwa hao TBC walifika pale uwanjani Zakheim kwa maelekezo maalum ya wakubwa wao ili waje "wauhujumu" ufunguzi huo wa kampeni.
Nimesikiliza tamko lao TBC la kulaani "kutimuliwa" pale uwanjani, wakihalalisha ukatajikataji wao wa matangazo, wakidai wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2020, ya maudhui ya vyombo vya habari!
Niwaukize TBC hivi mnajua kuwa sheria mama, nikimaanisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiyo "supreme" ya sheria zote nchini?
Kwa kuweka ibara ya sheria iliyoko kwenye Katiba, hamuoni kuwa nyinyi TBC ndiyo mmeivunja Katiba ya nchi kwa kutotaka wananchi waisikie hotuba ya viongozi wakuu wa ChADEMA kwa kisingizio cha sheria yenu kandamizi ya vyombo vya habari, ambayo "inajicontradict" na sheria mama, ambayo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatoa Uhuru huo wa habari haupaswi uingiliwe kati na chombo chochote hapa nchini?