Uchaguzi 2020 Uongozi wa CHADEMA ulikuwa sahihi "kuwatimua" TBC katika uzinduzi wa kampeni zake

Kati ya taasisi za kipuuzi kabisa kwa sasa, mojawapo ni TBC.

Rais Magufuli amekuwa anatukana watu hadharani, na TBC wakiwa mubashara. Lakini wapinzani hawajawahi kutoa tusi lolote. Wakiusema tu ukweli dhidi ya Magufuli, wanasema ni matusi!

Hivi mtu akisema kuwa Rais amejenga uwanja mkubwa wa ndege Chato wakati hakuna hata manispaa moja yenye uwanja mkubwa kama wa Chato, hilo ni tusi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
Nakubaliana na wewe kabisa. Hao jamaa walikuwa wanatafuta sababu tu ya beef na CDM liwe rasmi. Hiyo TV huwa inachefua sana na sidhani kama inatazamwa na watu wawanaojielewa
 
Hivi inawezekanaje TBC ndiyo ijifanye inafanya "censorship" ya matangazo wanayoyarusha na kukatakata matangazo, wakidai kuwa maudhui yake hayaendani na maudhui ya sheria ya vyombo vya habari?

Kinachokatazwa kwenye sheria hiyo ni matusi pekee

Hebu TBC muueleze Umma wa watanzania ni sehemu gani katika hotuba ya viongozi wa CHADEMA jana walitukana?

Hivi kwa viongozi wa CHADEMA kuishinikiza Tume ya Taifa ya uchaguzi kurejesha majina ya wagombea wa vyama vya upinzani, ambayo yamekatwa kihuni ndiyo kulisababisha TBC iyakate kate matangazo hayo?

Hivi nini kina maslahi kwa Taifa letu, Tume iyakate kihuni majina hayo au viongozi wa upinzani waishinikize Tume hiyo ili itende haki kwa kuwarejesha hao walioenguliwa kihuni?
Mnawaonea Watangazaji bur, wao huwa hawajui ukifanya nini unakosea....anayejua yupo huko juu hivyo wanachofanya wao ni kubahatisha tu kwamba hili ni kosa na hili ndio sahihi.
 
CDM wamewekewa mtego na sasa wameingia kichwa kichwa, hii inamaanisha hakuna mkutano wa CDM katika kampeni za 2020 utakaokuwa live tena, TBC walikuwa wanatafuta sababu tu na kweli mmewapatia justification.

Kwa Tz ni watu wangapi wana uwezo kuangalia mkutano wote kwa live streaming online, ukijumlisha na changamoto za ubora wa internet kwa streaming kwa maeneo mengi Tz, unapata jibu moja tu, CDM wameshawekwa kibra, kinachofuata kinajulikana.
Hakuna mtego hapo, kwanza tbccm haiangaliwi na watu wengi sana kama huna habari.
Wapuuzi sana, kodi zetu zitawatokea puani.
 
Mystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
Nami niliwaza hivyo ila nkasema ngoja muda utaamua
Kwa hyo hapo chadema mikutano yao ya kampeni haitawekwa live kwa sababu kuwa hawataki chombo cha habari cha taifa lakini wanahubiri "uhuru wa vyombo vya habari"?


Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
FB_IMG_1598629371317.jpg
 
Tutaona leo kama watakuwa wanakata matangazo ili kukidhi matakwa ya sheria ya maudhui

HAWATAKATA KWA KUWA WATAFUATA MAUDHUI YA UTANGAZAJI. FULL STOP.

MBONA JANA CDM HAWAJAPATA HATA REDIO STATION MBALI YA TV, KWA KUWA WENYE TV WALITOA MASHARTI YA KAMA WATAFUATA MAUDHUI YA UTANGAZAJI , WATAENDA, LKN HAWAKUONESHA KAMA KWELI WATAFUATA MASHARTI NDIO MAANA TV ZOTE ZILIJITOA. HATA TV YA UPANDE WA KWAO JANA ILIWATOLEA NJE. HAJUNA JANJA JANJA MWAKA HUU.
 
Watu mkitaka kila kitu muongee kishabiki ni kwamba ccm wataisapoti Tbc na wapinzani wataunga mkono ufukuzwaji wa watangazaji pale uwanjani...kwa sisi ambao hatuna vyama tunaona wote wamekosea pale na hakuna aliyefanya kitendo kizuri, TBC kukatakata matangazo hata mimi iliniuma sana, nilikuwa nasikiliza TbcTaifa mbowe alivyoanza kuongea uhuni wa kuenguliwa wabunge wa upinzani nikasikia mtangazaji anasema tusikilize kidogo wimbo wa uchaguzi, nikajikuta namtukana tu...then mbowe nae anakuja kusema Tbc watoke kisa wanakatakata matangazo.

Mambo ya Tbc mbowe angeyaacha tu yajiendeshe yenyewe kama watakavyo TBC wenyewe, hasira hizo hazina maana yoyote. Kwani kukatakata kwa matangazo ya Tbc kuna hasara gani kwa mkutano ule? Vyombo kibao vilikuwepo kuurusha live mkutano kwa hiyo Tbc ilivyokuwa inazingua watu tulihamia kwingine. Kuifukuza TBC uwanjani sio kitendo kizuri mngewaacha tu wafanye maovu yao na aibu ingewapata hata bila kuwafukuza.
 
Hakuna mtego hapo,kwanza tbccm haiangaliwi na watu wengi sana kama huna habari.

Wapuuzi sana, kodi zetu zitawatokea puani
Hivi hawa TBC watajisikiaje hapo Oktoba 28, watakapoona Mheshimiwa Tundu Lissu ndiye katangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu?

Hivi hawataona aibu na watapiga U-Turn na kuanza kumtangaza kwa kuwa tayari keshakuwa Rais?
 
Mimi nimeshangaa kwamba kumbe TBC inafuatiliwa Sana kiasi kwamba wana CDM walilalamikia kwamba matangazo yalikua yanakatakata.
Nikawaza Kama yanakatakata TBC si nikuangalia kupitia njia nyingine na kuwaacha TBC ili kila mmoja atumie uhuru wake.

Wanaosema huwa hawaangalii TBC unawakuta ndio wnaolalamika ilikua inakatakata.

Makosa ya TBC hayakusahihishwa kwa hekima na kutumiwa vyema na CDM zaidi waliharibu zaidi na kiki ikahamia kwa TBC sio kwa uzinduzi wa kampeni.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimeshangaa kwamba kumbe TBC inafuatiliwa Sana kiasi kwamba wana CDM walilalamikia kwamba matangazo yalikua yanakatakata.
Nikawaza Kama yanakatakata TBC si nikuangalia kupitia njia nyingine na kuwaacha TBC ili kila mmoja atumie uhuru wake.

Wanaosema huwa hawaangalii TBC unawakuta ndio wnaolalamika ilikua inakatakata.

Makosa ya TBC hayakusahihishwa kwa hekima na kutumiwa vyema na CDM zaidi waliharibu zaidi na kiki ikahamia kwa TBC sio kwa uzinduzi wa kampeni.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Suala ni kuwa hiko chombo cha habari cha TBC kinaendeshwa kwa kodi zetu sote wana-ccm na wana Chadema, sasa swali la kujiuliza ni kwa vipi wao wajifanye kama chombo cha habari cha chama kimoja tu cha CCM?
 
Nianze mada yangu kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 18(1) nayo inasema hivi "Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi na pia uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na mtu yeyote" mwisho wa kunukuu.

Hebu sasa tutazame nini kilitokea kule Zakheim Mbagala katika ufunguzi wa kampeni zake chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA.

Watangazaji wa TBC walifika "kwa shingo upande" katika uwanja huo kwa nia ya kuonyesha LIVE matangazo hayo.

Nini kilitokea katika urushaji matangazo hayo?

Wasikilizaji wa TBC walibaini kukatwa katwa kwa matangazo kwa matangazo hayo.

Ndipo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa alipoamuru watangazaji hao "wafungashe virago" vyao na waondoke uwanjani hapo katika muda wa dakika 15!

Wapo wananchi wanawalaumu viongozi wa CHADEMA kuwa eti kitendo chao hicho kilikuwa si cha kiungwana!

Hapo hapo TBC wakatoa taarifa ya kulaani kitendo cha kufukuzwa "kinyama" watangazaji wake kwenye ufunguzi wa kampeni hizo.

Hebu turejee katika utangazaji wa TBC katika kipindi chote hiki cha utawala wa serikali ya awamu ya 5, bila shaka hata mtoto mdogo anayesoma chekechea atakuwa anajua kuwa TBC imejigeuza kuwa kama televisheni ya CCM, kwa kutangaza "sifa na mapambio" kwa serikali hii ya CCM, chini ya kiongozi wake Rais John Magufuli.

Hata hivyo TBC ni chombo cha Umma na hakipaswi "kuhodhiwa" na chama chochote cha siasa na kinapaswa kitoe "airtime" iliyo sawa kwa vyama vyovyote vya siasa nchini, bila kufanya upendeleo wowote, kwa kuwa sisi wananchi walipa kodi, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tunaoiendesha TBC

Nini kilitokea jana?

Ni dhahiri kuwa hao TBC walifika pale uwanjani Zakheim kwa maelekezo maalum ya wakubwa wao ili waje "wauhujumu" ufunguzi huo wa kampeni.

Nimesikiliza tamko lao TBC la kulaani "kutimuliwa" pale uwanjani, wakihalalisha ukatajikataji wao wa matangazo, wakidai wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2020, ya maudhui ya vyombo vya habari!

Niwaukize TBC hivi mnajua kuwa sheria mama, nikimaanisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiyo "supreme" ya sheria zote nchini?

Kwa kuweka ibara ya sheria iliyoko kwenye Katiba, hamuoni kuwa nyinyi TBC ndiyo mmeivunja Katiba ya nchi kwa kutotaka wananchi waisikie hotuba ya viongozi wakuu wa ChADEMA kwa kisingizio cha sheria yenu kandamizi ya vyombo vya habari, ambayo "inajicontradict" na sheria mama, ambayo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatoa Uhuru huo wa habari haupaswi uingiliwe kati na chombo chochote hapa nchini?
TBC ni hovyo kabisa na inaudhi!
 
Back
Top Bottom