Uongozi Simba ni sikio la kufa halisikii dawa: Mazoezi bado ya wazi

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Jana usiku wamepost picha zao wenyewe kwa raha zao kuhusu mazoezi yao wakijandaa na geita gold kuna raia wamehudhuria na kwenye hizo picha kuna mmoja kabisa anarekodi.

Kabla wale wa comment za OYAA ACHA MAMBO YA KISHAMBA NA KIZAMANI hawajaanza embu soma alichowahi kuandika aliyekuwa katibu na msemaji wa simba Ezekiel kamwaga anazungumzia jinsi jamaa wa libolo ya angola alivyokuwa anahudhuria mazoezini kuchota mbinu zao.

"Simba imekosea kwenda Misri? Nasikia hizi hoia lakini nashangaa tu. Simba au timu yoyote ya Tz kwenda nje kuweka kambi ni hatua. Miaka nane tu iliyopita, Simba ilikuwa lazima ipige hodi kwa Marehemu Hans Poppe, Geofrey Nyange "Kaburu" au Mzee Ramesh Patel watoe hela za mafuta. Na mazoezi tunafanya kwa Mzee Kinesi au Sigara. Watu kibao wanajaa mazoezini. Hakuna siri za kimbinu wala faragha. Nakumbuka siku moia tulikuwa tunajiandaa na mechi dhidi ya Libolo ya Angola kumbe skauti wao, Alberto, alikuwa anakuja mazoezini kwetu kututazama kila siku. Anatuchota tu na kujua mbinu zote. Leo Simba ikienda Misri au kokote kwingine ughaibuni inaonekanaje ni kubaya?"

Simba kwa sasa kama hamna sabotage basi kuna mvurugano wa kichinichini na huu ujinga wenu mtavuna mnachokipanda sooon kwani mkichukua mabaunsa watano wa k4s security wafukuze watu inashindikana? au zungusheni makuti basi kama ile hela ya ukuta mlikula.

USHAURI WANGU KWA WAPINZANI WA SIMBA WANAOFUATA TUMENI WATU PALE WAPENI ILE MIWANI INAYOREKODI , SPY GLASSES WAPATE QUALITY NZURI KABISA TENA ILE INACHUKUA HADI AUDIO VIZURI MNOOO MAELEKEZO YA KIKOCHA KIZEE CHA KIZUNGU MTAYASIKIA VYEMA KABISA, MSISAHAU NA KUTUPIATUPIA YALE MAMBO YETU YA JADI MAANA SIMBA NI WAZUNGU HAWAJALI KABISA

mazoezingi3.jpg
mazoezi2.JPG
 
Kwenye mpira ni kama jeshi/vita tu. Siku zote kuna mazoezi ya wazi na mazoezi ya kimbinu. Mazoezi ya wazi ni ruksa mtu yoyote kuhudhuria lakini mazoezi ya mbinu si ruhusa watAzamaji kuona.

Iwapo viongozi wa Simba sasa hivi wanaruhusu watazamaji kwenye vyote yaaani mazoezi ya wazi na mazoezi ya mbinu basi wanakosea tena wanakosea sana.

Ni sawa na jeshini tu gwaride lao mtaliona watu wote pale kwa Mkapa lakini wakienda porini kujifunza mbinu za kivita raia hawaruhusiwi kusogea huko.

Kwenye mazoezi ya mbinu ndio huwa kuna zile "suprise" za kona, faulu, kuanza mpira haraka, n.k. ili upate goli la kumshangaza mpinzani wako.

Sasa mpinzani wako akituma mtu ambaye ni mtaalamu kwenye mazoezi ya timu yako basi lazima upate ushindi kwa shida sana kama sio kuambulia kichapo.
 
Kwenye mpira ni kama jeshi/vita tu. Siku zote kuna mazoezi ya wazi na mazoezi ya kimbinu. Mazoezi ya wazi ni ruksa mtu yoyote kuhudhuria lakini mazoezi ya mbinu si ruhusa watAzamaji kuona...
Ndiyo maana niliweka quotation ya Ezekiel kamwaga hapo akizungumzia scout wa Libolo ya angola aitwaye Alberto alivyokuwa akienda Tcc sigara kuchota mbinu za mazoezi yao

Hapo lazima free kicks zinavypigwa,kona,mpiga penalty anayepewa mara kwa mara,hata kujua atadaka nani,kocha anagawanya vipi kikosi chake rahisi kujua first 11

Mbaya zaidi hata watu wakirekodi kwa simu simba hawajali ndiyo maana nashauri wapinzani wajao wa simba watume watu na hizi spy glasses , simba wazungu sana hawajali issues ndogondogo kaa hizo

Simba mazoezi yao siku zote hapo bunju ni ya wazi, yawe ya mbinu au la..kenge hasikii hadi atoke damu

spy glasses.JPG
 
mtani wangu GENTA kapotelea wapi??au kajitoa makolokoloni???maana yupo kimyaa sanaaa tangu ijumaa kapoteaa!!hahahah GENTA njoo bana tuendeleze utani wa jadi!!
GENTA akipandisha uzi hapa Mashabiki wenzake wa Simba wajiandae atamwaga shombo la tuhuma ile mbaya. Ila si kawaida yake kuwa kimya namna hii!!!
 
Mbona man united wanafanya mazoezi carrington complex hakuna paparazi wala mashabiki na vichapo vikuu vinaendelea tu hebu kuja na hoja ya kueleweka
kwa nini utolee mfano man utd, unataka simba ielekee kuoza kama man utd?mashabiki wa man utd walitaka kuchoma nyumba ya Maguire ,vipi tuwaige na hilo? anyway yatakuja tu automatic hayo mnayoyataka
 
kwa nini utolee mfano man utd, unataka simba ielekee kuoza kama man utd?mashabiki wa man utd walitaka kuchoma nyumba ya Maguire ,vipi tuwaige na hilo? anyway yatakuja tu automatic hayo mnayoyataka
Kwan si ulikuja na uzi humi wa mashabiki wagomee kuangalia mechi za simba hapo lupaso?
Hata mjifungie ndani kufungwa ni kufungwa tu chamsingi angalia uliteleza wapi inuka pambana kiume
 
Kwan si ulikuja na uzi humi wa mashabiki wagomee kuangalia mechi za simba hapo lupaso?
Hata mjifungie ndani kufungwa ni kufungwa tu chamsingi angalia uliteleza wapi inuka pambana kiume
Lile likuwa wazo langu lakini ipo siku automatic haitahitaji hata mtu kuandika uwanja utakuwa empty automatic tu
hii hali siyo ya kawaida hii ni zaidi ya sabotage, ule ukuta tulioambiwa utatumia milion 150 zilizochangwa kwenye mchango ule wa azam uko wapi?
maana tuliambiwa utajengwa immediately ili kuwe na faragha baada ya wachezaji kulalamika
 
Kwani hakuna walinzi hapo bunju arena ambao watasaidia kutoa hao waangaliaji wa mazoezi?
 
Kwani hakuna walinzi hapo bunju arena ambao watasaidia kutoa hao waangaliaji wa mazoezi?
si ndicho nilichouliza? si wana ubia na 4ks security? tunavyolalamika hivi ni kwamba wengine tunakerwa na mambo kama haya
Uongozi wenyewe ulisema Boko alienda kulalamika kukosekana kwa faragha kwenye mazoezi wakasema ujenzi wa ukuta utaanza fasta, kimya hadi leo kwa nini tusiamini milions 150 zimeliwa
 
"OYAA ACHA MAMBO YA KISHAMBA NA KIZAMANI"

Nimenukuu tu baadhi ya maelezo yako hapo juu. Hivyo usinielewe tofauti.
 
GENTA akipandisha uzi hapa Mashabiki wenzake wa Simba wajiandae atamwaga shombo la tuhuma ile mbaya. Ila si kawaida yake kuwa kimya namna hii!!!
Kama hajapigwa ban sijui binafsi nimeshangazwa sana.Ni muda sasa hajajitokeza.
 
Back
Top Bottom