&lt;br /&gt;<br /><br />
&lt;br /&gt;<br /><br />
Mkuu tafadhali usichanganye madesa. Jf ni pamoja na mimi na wewe, sasa kama mimi ninaunga mkono chadema Jf inageukaje kuwa ya chadema? Hapa Jf kuna watu wa chadema,kuna watu wa magamba,kuna watu wa cuf,kuna watu wa nccr,kuna watu wa serikali na kuna wasio na vyama vya siasa. Tatizo linawezakuwa ni kwamba wale wa vyama vingine hawaleti habari za vyama vyao hapa na wanapozileta zinakuwa hazina mashiko ama mvuto hivyo kukosa wachangiaji. Na pengine jambo kubwa kuliko yote ni hata pale wanapoanzisha thread na kisha wanakimbia mjadala. Sisi wa chadema tukianzisha thread hatuzikimbii,tunakuwepo kujibu hoja zinazojitokeza, huenda kwa hali hii tunaonekana kufunika jukwaa la siasa hapa Jf hali inayopelekea baadhi ya watu kuona kwamba Jf ni ya chadema.