Kuna tatizo lingine la msingi ambalo wanachama, wapenzi na wafuasi wa CHADEMA wanaona aibu kulisema hadharani, ni ATTITUDE mbovu ya viongozi na wabunge wengi wa chama hicho. Chukulia mfano wa mbunge Joseph Haule a.k.a profesa Jay, unadhani mtu kama yule ni lini atazongwa zongwa na makesi kama ya Lijuakali? Sio kwamba haongei, sio kwamba hafanyi mikutano na wananchi wake na wala sio kwamba hakosoi serikali na watawala lakini kinachomtofautisha na wenzake ni attitude yake tu. Kama kuna siku Profesa Jay atakamatwa na kupata kesi kama za hao wengine basi nitaamini kweli wapinzani wanaonewa. Tofauti na hapo CHADEMA rekebisheni mienendo yenu mibovu.
Tatizo kubwa la Chadema wamezoe siasa za hisia ,wanaamini kwenye kutukana au kufarakana na kubishana Zaidi kama njia ya kuwapatia umaarufu, sikatai lakini siasa hubadilika kulingana na mazingira na wakati, mfano;
1. Kuna haja gani ya Lijuakali kila siku yuko mahakamani? utagundua kama ulivyosema altitude.
2. Kuna haja gani ukiwa kwenye media lazima utukane? freedom of speech sio kutukana tu, chadema wengi ni wapenzi wa siasa za Kenya, je wanaweza hata wakatupatia video moja ya Raila /kalonzo /Mudavadi/akimtukana uhuru? , kuna tofauti kubwa kati ya kukosoa na kutukana, kukosoa ni kuielekeza serikali au Rais kuwa kwa hili ur wrong fanya hivi maana yake unatoa na solution.
3. Hadithi za kununuliwa, asilimia kubwa ya wabunge wao pia hawakubaliani na misimamo ya chadema, watu wanataka maendeleo wew unasema usishirikiane na serikali iliyopo a the end wananchi utawaambia nini maendeleo yakichelewa, ndio maana utaona wabunge wengi wa upinzani wanakimbia, chadema kwa kulijua hilo wanakuja na ngojera wamenunuliwa, tupe evidence hakuna.
4. Msimamo wa chadema sio maendeleo,kama mmegundua toka Magufuli aingie madarakani tumejua picha halisi ya upinzani wa Tanzania, hawako kwa ajiri ya maendeleo na kushika dola kwa miaka ijayo, wao maslahi yao ni Maisha yao. Mimi nilifikiria katika wakati huu washikamane na serikali kuleta maendeleo kama walivyo kuwa wanahubiri enzi zile ,leo wamekuwa ni watu wanapigania bunge live, wanapigania waongee kwenye tv waonekane, hivi kweli bunge live linaweza kukwamisha jitihada zako za kuwaletea wananchi maendeleo?
5. Mimi nilitoa ushauri kuwa wajitathimini kwanza wao wenyewe, wapate maoni direct ya kutoka kwa wananchi ,wawaulize kuwa hivi tukitukana, tukipigana na serikali nyie huku mnatungumzia vipi? VS tukishiriakiana na serikali katika maendeleo, tukafuata utaratibu wa kawaida wa mikutano, je wananchi watasema nin, wakipata maoni yote, watajua nini cha kufanya, lasivyo watu watakuwa wana tafuta visa kama nasari anazuga hahudhurii bunge au chochote ili wafukuzwe, maana anaona hakuna dira.