Uongozi CHADEMA umeshindwa kusimamia chama

Uongozi CHADEMA umeshindwa kusimamia chama

Wakuu,

Pamoja na lawama kwa huyo Nassari au hata Ndugai ambaye ametumia vyema sheria iliyowazi kabisa kwanini tusijiulize nafasi ya viongozi wa chama kwenye hili sakata?

Hivi kweli imefikia hatua Chadema hawafuatiliani tena mwenendo wa wabunge wao bungeni ikiwemo mahudhurio? Mbunge anakosa kuhudhuria vipindi vitatu vya bunge hadi anachukuliwa hatua na spika kabla nyie wenyewe hamjachukua hatua? What a shame!

Tukisema tatizo la Chadema ni zaidi ya CCM na dola kama kilivyo kilio cha kila siku hatueleweki! Kama kuna taasisi inayotimiza majukumu yake ya kawaida huu ujinga usingetokea.

Tumesema mara nyingi, Chadema ya sasa hakuna nidhamu, kila mtu anasharubu, kila mtu anaweza kuita press au kuandika chochote mtandaoni bila kujua kwanza party position.

Tatizo la nidhamu linakolezwa na dharau kwa katibu mkuu Mashinji. Katibu mkuu pamoja na uwezo wake mkubwa kimbinu lakini ameshindwa kusimamia chama hasa baada ya mpasuko wa 2015.

Katibu mkuu Mashinji si kiongozi mbovu bali anaongoza watu ambao wanapitia kipindi cha mpito ambacho kinaweza kuamua mustakali wa chama kama karata zisipochangwa vizuri na chama kilihitaji mtu anaweza kukemea yeyote na ikibidi hata kuchukua hatua kama ilivyowezekana ku manage crisis ya Zitto na kundi lake.

Wanachama na wapenda mabadiliko tuache kutetea ovyo uongozi uliopo kwa namna mambo yanavyoenda. Chadema ina vijana wengi walioiva ni vizuri kupewa vijiti tuanze upya. Bila mabadiliko hali hii haishushi tu morali ya wanachama bali inazidi kupenya hadi kwa viongozi waandamizi.

Tuache kauli za kutiana moyo ambazo sasa zimegeuka faraja hewa kuwa chama kitabaki hata kama viongozi wake waandamizi wakiondoka. Chama kinapoteza watu muhimu kwa namna inayohitaji tafakari na fikra huru kubaini tatizo.

Napenda kurudia rai yangu, wanaoikumbuka vizuri sana NCCR watakuwa wanaogopa hata unyasi kwa yanayoendelea Chadema. Chama kinaelekea ilipo NCCR kama mzaha! Chukueni hatua badala ya kupeana moyo hewa.

Walau Chadema zama hizi kuna mitandao kuipa uhai kidogo tofauti na enzi za Mkapa na jinsi NCCR ilivyopotezwa na kubakia jina la Mbatia kwa sasa.
Wewe unajuwaje kuwa hakuchukuliwa hatua?Mbona unadandia gari kwa mbele?
 
Chama hakioni mbali,hakina mbinu za kijijenga kinakuwa kwa kutegemea matukio au Makosa ya Chama Tawala, hakina vision Mtu akihama badala ya kusikitika wanasema alikuwa Mzigo, wajipange.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyeshiriki kumfukuza zito kwa usaliti na kutangaza kugombea uenyekiti bila kufuata taratibu za chama ndio huyo kajitangaza kuwa 2020 anagombea

Ha haaaaaaaaaaa.......kama utani ila ndio ukweli wenyewe!
 
Kabla ya kuilamu CHADEMA na uongozi wake tujikumbushe wanayopitia viongozi na wabunge wake katika zama hizi za utawala wa awamu ya tano ya CCM.

Mnadhimu mkuu wa CHADEMA kamanda Tundu Lissu yupo ktk matibabu baada ya kushambuliwa na watu wanaosemekana hawajulikani.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa rumande kwa miezi kadhaa. Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji, Wabunge wengi wa CHADEMA na madiwani wao wamefunguliwa kesi nyingi mahakamani na kutakiwa kuripoti Polisi mara kwa mara.

Edward Lowassa aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha CHADEMA pia alikuwa ameandamwa kwa kesi nyingi kabla ya kukimbilia CCM.

Halafu wanatokea watanzania wasaulifu kushindwa kubaini, kutambua na kuona njama zote hizo hapo juu kuififisha CHADEMA kisiasa, kwa Chama cha CCM kutumia njia haramu.

Itakuwa ni aibu kina ' MTAZAMO ' kuja na hoja dhaifu kuielekezea kidole CHADEMA kuwa ni taasisi dhaifu wakati ilitakiwa wao kina MTAZAMO kukemea kwa kupaza sauti tabia ya CCM kutumia kila njia haramu kuvidhoofisha vyama vya CHADEMA na CUF.
Lugora apiga marufuku mikutano ya ndani:

Hali hii ya CCM na serikali yake kuvisakama vyama vingine vya siasa Tanzania siyo nzuri kwa taifa letu lenye katiba ya kidemokrasia na hamu ya kuwa na nchi ya amani na utulivu.

Kuna tatizo lingine la msingi ambalo wanachama, wapenzi na wafuasi wa CHADEMA wanaona aibu kulisema hadharani, ni ATTITUDE mbovu ya viongozi na wabunge wengi wa chama hicho. Chukulia mfano wa mbunge Joseph Haule a.k.a profesa Jay, unadhani mtu kama yule ni lini atazongwa zongwa na makesi kama ya Lijuakali? Sio kwamba haongei, sio kwamba hafanyi mikutano na wananchi wake na wala sio kwamba hakosoi serikali na watawala lakini kinachomtofautisha na wenzake ni attitude yake tu. Kama kuna siku Profesa Jay atakamatwa na kupata kesi kama za hao wengine basi nitaamini kweli wapinzani wanaonewa. Tofauti na hapo CHADEMA rekebisheni mienendo yenu mibovu.
 
Watu wamechoshwa na uongozi wa CCM ila hawana mbadala.

Hii ilikuwa fursa nzuri ya viongozi wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani kujionesha kwamba wao ni mbadala.

Wananchi si wajinga wasijue ipi mali ipi garasa. Ila wakiona yote magarasa wanaona waache.

Uchaguzi ujao utaonesha. Wengi hawatapiga kura. Hao wote wangepiga kura upinzani kama mara hii wangewekeza kwenye kujiimarisha na ingekuwa na nguvu zaidi katikati ya shurba hizi.

Fursa tumewapa, lakini mnakatisha tamaa jamii iliyowaamini.

Kutwa mnatengeneza mtetewe na wazungu. Right Mbowe na wengineo wangekuwa bora kwa wananchi wao kelele zingesikika kwamba wanaonewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda hatua ni kumfukuza mapema lkn isingesaidia kitu sana sana angerudi tena Bungeni kupitia CCM
Lakini angeitwa kuhojiwa na taarifa kuwekwa kwa kumbukumbu ingeonesha walau umakini kidogo kama alivyofanya Dr Bashiru. Lazima Chadema kama taasisi ioneshe namna inavyosimamia wale iliyowapa dhamana kupeperusha bendera ya chama kupitia nafasi tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu za Edward Lowassa na wengine kurudi CCM :
Hali ya vitisho kwa wanasiasa na misalaba mizito vyawakimbiza wanasiasa
 
Ni kweli kabisa ndio maana tunazuia mikutano ya ndani pamoja ya wazi, halafu viongozi wa upinzani tunawambakia kesi na kuwanyima dhamana ili wasipate muda kuongoza vyama vyao, ma tunasubiri uchaguzi uje tuibe kura tena na kupora ushindi maana viongozi wa upinzani wameshindwa kuongoza, uko sahihi kada mwenzagu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maelezo ya kijinga kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom