Katibu wa Chadema Morogoro asimamishwa uongozi

Katibu wa Chadema Morogoro asimamishwa uongozi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,025
Reaction score
285,558
Hii ndio Taarifa ya sasa kutoka Kanda ya Kati

Inadaiwa Katibu huyo huku akijua utaratibu wa CHAMA chake ameamua kuvunja Sheria makusudi na kujiropokea uongo

Natoa Onyo kwa Mamluki wengine waliohongwa Kwamba, wakiendelea n.a. Usaliti wao tutaendelea kuwafyeka kwenye CHAMA bila huruma yoyote

Mungu Ibariki Chadema
Safi sna.
 
Aisee...
CHADEMA katika kipindi wanapaswa kuwa makini, uvumilivu na maamuzi magumu ni hiki kipindi.

Wahuni hawalali, CHADEMA imekuwa threat kwao kwenye kila nyanja, hii vita ni vita ya kutaka kuifanya CHADEMA iwe CCM B..

CHADEMA inabidi wapambane kwa jasho na damu.

Fyekeni wasaliti wote, fyekeni mamluki bila huruma..

CHADEMA wakishinda hii battle watakuwa katika nafasi nzuri sana.
 
Naam
 
Hii ndio Taarifa ya sasa kutoka Kanda ya Kati

Inadaiwa Katibu huyo huku akijua utaratibu wa CHAMA chake ameamua kuvunja Sheria makusudi na kujiropokea uongo

Natoa Onyo kwa Mamluki wengine waliohongwa Kwamba, wakiendelea n.a. Usaliti wao tutaendelea kuwafyeka kwenye CHAMA bila huruma yoyote

Mungu Ibariki Chadema
Kipindi hiki ni kigumu sana, ni wazi Lumumba wapo nyuma ya hizi drama tunazo ziona kila kukicha.

Ila Mungu yupo kwa akili ya watanzania wote
 
Ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kati imemsimamisha uongozi rasmi Katibu wake Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola, kwa kosa la kukiuka maadili na kutoa shutuma nzito hadharani dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Wegesa Heche.

Soma pia Katibu CHADEMA Morogoro: Mamlaka za Chama ziingilie kati tuhuma zinazomhusisha Makamu Mwenyekiti kuhusu michango

Taarifa rasmi iliyotolewa leo Alhamisi, Julai 9, 2026, na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Mashaka Masoud imeeleza kuwa hatua hiyo ya dharura imechukuliwa ili kulinda nidhamu ya taasisi hiyo baada ya Okola kuitisha mkutano wa waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo na kushusha makombora dhidi ya Heche kinyume cha kanuni za chama.

“Maamuzi haya yamechukuliwa kutokana na kitendo cha ndugu Barnabas Okola kukiuka sheria za maadili ya kiuongozi wa CHADEMA ya katiba ya chama ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2019 kwa kuita mkutano wa waandishi wa habari na kutoa matamko na shutuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mh. John Wegesa Heche kinyume na kanuni za maadili ya viongozi wa CHADEMA kanuni ya 10.1 (ix) na 10.1(x)”, imesomeka taarifa rasmi ya Ashura Mashaka Masoud.

Kanda ya Kati imempa Okola masharti ikimtaka kuwasilisha uthibitisho wa tuhuma zote alizozitoa dhidi ya Heche ndani ya siku 14, huku akipigwa marufuku kujihusisha na shughuli yoyote ya kichama kama kiongozi katika kipindi hiki.

Chanzo: Jambo TV
 
Pelekeni moto hasaa wahuni wote mpaka watubu
Pitisha fagio la chuma hakuna kumuonea kima huruma
 
Back
Top Bottom