Uongozi CHADEMA umeshindwa kusimamia chama

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,120
Reaction score
35,507
Wakuu,

Pamoja na lawama kwa huyo Nassari au hata Ndugai ambaye ametumia vyema sheria iliyowazi kabisa kwanini tusijiulize nafasi ya viongozi wa chama kwenye hili sakata?

Hivi kweli imefikia hatua Chadema hawafuatiliani tena mwenendo wa wabunge wao bungeni ikiwemo mahudhurio? Mbunge anakosa kuhudhuria vipindi vitatu vya bunge hadi anachukuliwa hatua na spika kabla nyie wenyewe hamjachukua hatua? What a shame!

Tukisema tatizo la Chadema ni zaidi ya CCM na dola kama kilivyo kilio cha kila siku hatueleweki! Kama kuna taasisi inayotimiza majukumu yake ya kawaida huu ujinga usingetokea.

Tumesema mara nyingi, Chadema ya sasa hakuna nidhamu, kila mtu anasharubu, kila mtu anaweza kuita press au kuandika chochote mtandaoni bila kujua kwanza party position.

Tatizo la nidhamu linakolezwa na dharau kwa katibu mkuu Mashinji. Katibu mkuu pamoja na uwezo wake mkubwa kimbinu lakini ameshindwa kusimamia chama hasa baada ya mpasuko wa 2015.

Katibu mkuu Mashinji si kiongozi mbovu bali anaongoza watu ambao wanapitia kipindi cha mpito ambacho kinaweza kuamua mustakali wa chama kama karata zisipochangwa vizuri na chama kilihitaji mtu anaweza kukemea yeyote na ikibidi hata kuchukua hatua kama ilivyowezekana ku manage crisis ya Zitto na kundi lake.

Wanachama na wapenda mabadiliko tuache kutetea ovyo uongozi uliopo kwa namna mambo yanavyoenda. Chadema ina vijana wengi walioiva ni vizuri kupewa vijiti tuanze upya. Bila mabadiliko hali hii haishushi tu morali ya wanachama bali inazidi kupenya hadi kwa viongozi waandamizi.

Tuache kauli za kutiana moyo ambazo sasa zimegeuka faraja hewa kuwa chama kitabaki hata kama viongozi wake waandamizi wakiondoka. Chama kinapoteza watu muhimu kwa namna inayohitaji tafakari na fikra huru kubaini tatizo.

Napenda kurudia rai yangu, wanaoikumbuka vizuri sana NCCR watakuwa wanaogopa hata unyasi kwa yanayoendelea Chadema. Chama kinaelekea ilipo NCCR kama mzaha! Chukueni hatua badala ya kupeana moyo hewa.

Walau Chadema zama hizi kuna mitandao kuipa uhai kidogo tofauti na enzi za Mkapa na jinsi NCCR ilivyopotezwa na kubakia jina la Mbatia kwa sasa.
 
Ni kweli kabisa ndio maana tunazuia mikutano ya ndani pamoja ya wazi, halafu viongozi wa upinzani tunawambakia kesi na kuwanyima dhamana ili wasipate muda kuongoza vyama vyao, ma tunasubiri uchaguzi uje tuibe kura tena na kupora ushindi maana viongozi wa upinzani wameshindwa kuongoza, uko sahihi kada mwenzagu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama kizima kilikuwa jela? Hivi mnafikiri ni awamu hii tu ndio mna makesi? Unajua awamu iliyopita kulikuwa hakuna kiongozi ambaye hana kesi?

Nakubali viongozi wana changamoto lakini ndio upinzani wenyewe wa kiafrika, hakuna siasa za upinzani rahisi. Lakini chama ni taasisi, ni zaidi ya Mbowe, Mashinji n.k, lazima mambo mengine yaendelee kiutawala.

Chadema wasipobadilika tunaenda kubaki na chama cha upinzani kikubwa kihistoria kama NCCR na CUF.

Katibu hajui kama mbunge wake anahudhuria vikao au lah then wanataka kuishika CCM uchawi hahahahahahah.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Inasikitisha sana. Wabunge hawahudhuri vikao vya bunge mtu analeta habari za mikutano ya ndani! Sijui nani kawaloga hawa! Inatia hasira kwelikweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahah wafuasi wa chadema ni ZERO KABISA.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Wakuu,

Pamoja na lawama kwa huyo Nassari au hata Ndugai ambaye ametumia vyema sheria iliyowazi kabisa kwanini tusijiulize nafasi ya viongozi wa chama kwenye hili sakata?

Hivi kweli imefikia hatua Chadema hawafuatiliani tena mwenendo wa wabunge wao bungeni ikiwemo mahudhurio? Mbunge anakosa kuhudhuria vipindi vitatu vya bunge hadi anachukuliwa hatua na spika kabla nyie wenyewe hamjachukua hatua? What a shame!

Tukisema tatizo la Chadema ni zaidi ya CCM na dola kama kilivyo kilio cha kila siku hatueleweki! Kama kuna taasisi inayotimiza majukumu yake ya kawaida huu ujinga usingetokea.

Tumesema mara nyingi, Chadema ya sasa hakuna nidhamu, kila mtu anasharubu, kila mtu anaweza kuita press au kuandika chochote mtandaoni bila kujua kwanza party position.

Tatizo la nidhamu linakolezwa na dharau kwa katibu mkuu Mashinji. Katibu mkuu pamoja na uwezo wake mkubwa kimbinu lakini ameshindwa kusimamia chama hasa baada ya mpasuko wa 2015.

Katibu mkuu Mashinji si kiongozi mbovu bali anaongoza watu ambao wanapitia kipindi cha mpito ambacho kinaweza kuamua mustakali wa chama kama karata zisipochangwa vizuri na chama kilihitaji mtu anaweza kukemea yeyote na ikibidi hata kuchukua hatua kama ilivyowezekana ku manage crisis ya Zitto na kundi lake.

Wanachama na wapenda mabadiliko tuache kutetea ovyo uongozi uliopo kwa namna mambo yanavyoenda. Chadema ina vijana wengi walioiva ni vizuri kupewa vijiti tuanze upya. Bila mabadiliko hali hii haishushi tu morali ya wanachama bali inazidi kupenya hadi kwa viongozi waandamizi.

Tuache kauli za kutiana moyo ambazo sasa zimegeuka faraja hewa kuwa chama kitabaki hata kama viongozi wake waandamizi wakiondoka. Chama kinapoteza watu muhimu kwa namna inayohitaji tafakari na fikra huru kubaini tatizo.

Napenda kurudia rai yangu, wanaoikumbuka vizuri sana NCCR watakuwa wanaogopa hata unyasi kwa yanayoendelea Chadema. Chama kinaelekea ilipo NCCR kama mzaha! Chukueni hatua badala ya kupeana moyo hewa.

Walau Chadema zama hizi kuna mitandao kuipa uhai kidogo tofauti na enzi za Mkapa na jinsi NCCR ilivyopotezwa na kubakia jina la Mbatia kwasasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa shida yako ni moja tu: Mahaba yaliyopitiliza kwa Wilbrod Slaa. Tangu Slaa aondoke CDM umekuwa mchungu sana. Huna jema hata moja kwa chadema. I cannot take you seriously; the same way I do to MM. Punguzeni mahaba, yanapofusha.
 
Brother hujawahi kukata tamaa kukishauri chama hiki ukipendacho kwa dhati ya moyo wako! Sema wanazi huwa hawakuelewi.

Una point ya msingi sana! Chadema kila mtu anasauti! Mashinji is just there as a toothless dog.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa shida yako ni moja tu: Mahaba yaliyopitiliza kwa Wilbrod Slaa. Tangu Slaa aondoke CDM umekuwa mchungu sana. Huna jema hata moja kwa chadema. I cannot take you seriously; the same way I do to MM. Punguzeni mahaba, yanapofusha.
Bro, nakuelewa sana ila naomba tusaidie kupaza sauti Chadema ijipange upya. Yanayoendelea ni makubwa kuliko misimamo yangu baada ya usaliti kwa Dr Slaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejaribu uanisha ya msingi lakini kuongea haya kwenye keyboard ni rahisi sana, tujaribu kufahamu hawa ndugu zetu wanapitia kipindi kigumu sana.

Tusikimbilie kulaumu kuna mmoja wa wabunge waandamizi alinieleza haya kwa kina, tusicheze na kitu kinachoitwa DOLA its WORSE.
Refer kauli ya "Wewe pambana nao huko ndani wakitoka Nje mimi ninao"
 
Mkuu hata kufatilia mwenendo wa wabunge ikiwemo mahudhurio tunaleta excuse kama hizi? Kesho ukisikia kuna ubadhirifu Chadema si bado tutakuja na ngonjera hizi? Tunahitaji kubadilika, lipo tatizo zito!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Pamoja na lawama kwa huyo Nassari au hata Ndugai ambaye ametumia vyema sheria iliyowazi kabisa kwanini tusijiulize nafasi ya viongozi wa chama kwenye hili sakata?

Hivi kweli imefikia hatua Chadema hawafuatiliani tena mwenendo wa wabunge wao bungeni ikiwemo mahudhurio? Mbunge anakosa kuhudhuria vipindi vitatu vya bunge hadi anachukuliwa hatua na spika kabla nyie wenyewe hamjachukua hatua? What a shame!

Tukisema tatizo la Chadema ni zaidi ya CCM na dola kama kilivyo kilio cha kila siku hatueleweki! Kama kuna taasisi inayotimiza majukumu yake ya kawaida huu ujinga usingetokea.

Tumesema mara nyingi, Chadema ya sasa hakuna nidhamu, kila mtu anasharubu, kila mtu anaweza kuita press au kuandika chochote mtandaoni bila kujua kwanza party position.

Tatizo la nidhamu linakolezwa na dharau kwa katibu mkuu Mashinji. Katibu mkuu pamoja na uwezo wake mkubwa kimbinu lakini ameshindwa kusimamia chama hasa baada ya mpasuko wa 2015.

Katibu mkuu Mashinji si kiongozi mbovu bali anaongoza watu ambao wanapitia kipindi cha mpito ambacho kinaweza kuamua mustakali wa chama kama karata zisipochangwa vizuri na chama kilihitaji mtu anaweza kukemea yeyote na ikibidi hata kuchukua hatua kama ilivyowezekana ku manage crisis ya Zitto na kundi lake.

Wanachama na wapenda mabadiliko tuache kutetea ovyo uongozi uliopo kwa namna mambo yanavyoenda. Chadema ina vijana wengi walioiva ni vizuri kupewa vijiti tuanze upya. Bila mabadiliko hali hii haishushi tu morali ya wanachama bali inazidi kupenya hadi kwa viongozi waandamizi.

Tuache kauli za kutiana moyo ambazo sasa zimegeuka faraja hewa kuwa chama kitabaki hata kama viongozi wake waandamizi wakiondoka. Chama kinapoteza watu muhimu kwa namna inayohitaji tafakari na fikra huru kubaini tatizo.

Napenda kurudia rai yangu, wanaoikumbuka vizuri sana NCCR watakuwa wanaogopa hata unyasi kwa yanayoendelea Chadema. Chama kinaelekea ilipo NCCR kama mzaha! Chukueni hatua badala ya kupeana moyo hewa.

Walau Chadema zama hizi kuna mitandao kuipa uhai kidogo tofauti na enzi za Mkapa na jinsi NCCR ilivyopotezwa na kubakia jina la Mbatia kwasasa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Haa ...watakuambia hawajawahi kuwa na spika dhaifu kama huyo , na bunge nalo ni dhaifu tuone nani dhaifu hapo
 
Ni kweli kabisa ndio maana tunazuia mikutano ya ndani pamoja ya wazi, halafu viongozi wa upinzani tunawambakia kesi na kuwanyima dhamana ili wasipate muda kuongoza vyama vyao, ma tunasubiri uchaguzi uje tuibe kura tena na kupora ushindi maana viongozi wa upinzani wameshindwa kuongoza, uko sahihi kada mwenzagu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ester Matiko katumwa Rwanda na Spika lakini Kafutiwa dhamana bunge na spika wako kimya waafutie wabunge wote wa upinzani wakitaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The Chief Whip is responsible foradministering the whipping system that ensures that members of the party attend and vote in Parliament as the party leadership desires. Whips are MPs or Lords appointed by each party in Parliament to help organise their party's contribution to parliamentary business.

Kabla ya kuilamu CHADEMA na uongozi wake tujikumbushe wanayopitia viongozi na wabunge wake katika zama hizi za utawala wa awamu ya tano ya CCM.
Mnadhimu mkuu wa CHADEMA kamanda Tundu Lissu yupo ktk matibabu baada ya kushambuliwa na watu wanaosemekana hawajulikani.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa rumande kwa miezi kadhaa. Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji, Wabunge wengi wa CHADEMA na madiwani wao wamefunguliwa kesi nyingi mahakamani na kutakiwa kuripoti Polisi mara kwa mara.

Edward Lowassa aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha CHADEMA pia alikuwa ameandamwa kwa kesi nyingi kabla ya kukimbilia CCM.

Halafu wanatokea watanzania wasaulifu kushindwa kubaini, kutambua na kuona njama zote hizo hapo juu kuififisha CHADEMA kisiasa, kwa Chama cha CCM kutumia njia haramu.
Jaji Sam Rumanyika si tu amewaachia huru Mbowe na Matiko, bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti polisi kila wiki,” amesema Zitto ambaye pia ni mbunge huyo wa Kigoma Mjini.
Zitto ampongeza Jaji Rumanyika na kueleza Tanzania bado ina majaji kwa hakika na akamuombea mola ampe maisha marefu. Nderemo, vifijo Mbowe kuachiwa kwa dhamana

Itakuwa ni aibu kina ' MTAZAMO ' kuja na hoja dhaifu kuielekezea kidole CHADEMA kuwa ni taasisi dhaifu wakati ilitakiwa wao kina MTAZAMO kukemea kwa kupaza sauti tabia ya CCM kutumia kila njia haramu kuvidhoofisha vyama vya CHADEMA na CUF.
Lugora apiga marufuku mikutano ya ndani:

Hali hii ya CCM na serikali yake kuvisakama vyama vingine vya siasa Tanzania siyo nzuri kwa taifa letu lenye katiba ya kidemokrasia na hamu ya kuwa na nchi ya amani na utulivu.
 
Wakuu,

Pamoja na lawama kwa huyo Nassari au hata Ndugai ambaye ametumia vyema sheria iliyowazi kabisa kwanini tusijiulize nafasi ya viongozi wa chama kwenye hili sakata?

Hivi kweli imefikia hatua Chadema hawafuatiliani tena mwenendo wa wabunge wao bungeni ikiwemo mahudhurio? Mbunge anakosa kuhudhuria vipindi vitatu vya bunge hadi anachukuliwa hatua na spika kabla nyie wenyewe hamjachukua hatua? What a shame!

Tukisema tatizo la Chadema ni zaidi ya CCM na dola kama kilivyo kilio cha kila siku hatueleweki! Kama kuna taasisi inayotimiza majukumu yake ya kawaida huu ujinga usingetokea.

Tumesema mara nyingi, Chadema ya sasa hakuna nidhamu, kila mtu anasharubu, kila mtu anaweza kuita press au kuandika chochote mtandaoni bila kujua kwanza party position.

Tatizo la nidhamu linakolezwa na dharau kwa katibu mkuu Mashinji. Katibu mkuu pamoja na uwezo wake mkubwa kimbinu lakini ameshindwa kusimamia chama hasa baada ya mpasuko wa 2015.

Katibu mkuu Mashinji si kiongozi mbovu bali anaongoza watu ambao wanapitia kipindi cha mpito ambacho kinaweza kuamua mustakali wa chama kama karata zisipochangwa vizuri na chama kilihitaji mtu anaweza kukemea yeyote na ikibidi hata kuchukua hatua kama ilivyowezekana ku manage crisis ya Zitto na kundi lake.

Wanachama na wapenda mabadiliko tuache kutetea ovyo uongozi uliopo kwa namna mambo yanavyoenda. Chadema ina vijana wengi walioiva ni vizuri kupewa vijiti tuanze upya. Bila mabadiliko hali hii haishushi tu morali ya wanachama bali inazidi kupenya hadi kwa viongozi waandamizi.

Tuache kauli za kutiana moyo ambazo sasa zimegeuka faraja hewa kuwa chama kitabaki hata kama viongozi wake waandamizi wakiondoka. Chama kinapoteza watu muhimu kwa namna inayohitaji tafakari na fikra huru kubaini tatizo.

Napenda kurudia rai yangu, wanaoikumbuka vizuri sana NCCR watakuwa wanaogopa hata unyasi kwa yanayoendelea Chadema. Chama kinaelekea ilipo NCCR kama mzaha! Chukueni hatua badala ya kupeana moyo hewa.

Walau Chadema zama hizi kuna mitandao kuipa uhai kidogo tofauti na enzi za Mkapa na jinsi NCCR ilivyopotezwa na kubakia jina la Mbatia kwasasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu
Nasari alirudi CCM toka mwaka jana,akaogopa nguvu ya UMMA!
Ndiyo wakapanga na CCM asiende tena Bungeni hadi atakapo fukuzwa
 
Kama chama cha siasa makini kinapaswa kulinda uwajibikaji wa mbunge wake si tu kuhudhuria vikao hata uwajibikaji kwa wananchi wake.

Hayo yamekuwa mapungufu makubwa kwa CHADEMA na inawezekana walikuwa wanajua shida iliyopo lakini muda umezungumza.

Hata swali la Lissu hatuoni chama kulichukulia hatua ili Mbunge wake taarifa za kiofisi kufika kwa Ofisi ya Spika ili kuweka uzania na ushahidi kama haki zitavunjwa.

Mwisho wa siku tutasikia naye kavuliwa Ubunge ndipo wajitokeze na kuanza kulalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom