Uongozi CHADEMA umeshindwa kusimamia chama

Uongozi CHADEMA umeshindwa kusimamia chama

Kipindi katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru anafuatilia wabunge wa CCM watoro bungeni tulichukulia juhudi hizi kishabiki na hata walioitwa kuhojiwa tukageuza kisiasa zaidi.

Tunahitaji kubadilika sana kimtizamo ili kuweza kujenga vyama vya upinzani imara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi binafsi awamu hii nina pesa kutokana na ccm ndio maana Kuna mambo sichangii kuhusu upinzani

Kufa kwa chadema ni bora na kheri kwa Sisi ambao awamu hii tunakula, Uwepo wa ccm bila bughuza ni msaada kwangu

Mimi nashangaa Sana watu kutetea chadema, Sisi wengine wazazi wamepata ulaji awamu hii na wanasafiri nje

Wewe Kama upo chadema huna maslahi Kaa kimya, Sisi wenye maslahi ccm tutatetea chadema itoweke,
 
Kama kuna chochote ulihoji kuhusu huo uhuni ni kabla ya Magufuli kuingia madarakani. Baada ya hapo uhuni wowote waliofanyiwa wapinzani uliona ni stahiki kisa walimpokea Lowassa.
Mzee Mwanakijiji tangu aingie ngosha mwenzie yote mema kwake lakini pia alikua muumini wa mzee Slaa
 
Ni kweli kabisa ndio maana tunazuia mikutano ya ndani pamoja ya wazi, halafu viongozi wa upinzani tunawambakia kesi na kuwanyima dhamana ili wasipate muda kuongoza vyama vyao, ma tunasubiri uchaguzi uje tuibe kura tena na kupora ushindi maana viongozi wa upinzani wameshindwa kuongoza, uko sahihi kada mwenzagu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni mda wakujenga nchi na sio kufanya kampeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Pamoja na lawama kwa huyo Nassari au hata Ndugai ambaye ametumia vyema sheria iliyowazi kabisa kwanini tusijiulize nafasi ya viongozi wa chama kwenye hili sakata?

Hivi kweli imefikia hatua Chadema hawafuatiliani tena mwenendo wa wabunge wao bungeni ikiwemo mahudhurio? Mbunge anakosa kuhudhuria vipindi vitatu vya bunge hadi anachukuliwa hatua na spika kabla nyie wenyewe hamjachukua hatua? What a shame!

Tukisema tatizo la Chadema ni zaidi ya CCM na dola kama kilivyo kilio cha kila siku hatueleweki! Kama kuna taasisi inayotimiza majukumu yake ya kawaida huu ujinga usingetokea.

Tumesema mara nyingi, Chadema ya sasa hakuna nidhamu, kila mtu anasharubu, kila mtu anaweza kuita press au kuandika chochote mtandaoni bila kujua kwanza party position.

Tatizo la nidhamu linakolezwa na dharau kwa katibu mkuu Mashinji. Katibu mkuu pamoja na uwezo wake mkubwa kimbinu lakini ameshindwa kusimamia chama hasa baada ya mpasuko wa 2015.

Katibu mkuu Mashinji si kiongozi mbovu bali anaongoza watu ambao wanapitia kipindi cha mpito ambacho kinaweza kuamua mustakali wa chama kama karata zisipochangwa vizuri na chama kilihitaji mtu anaweza kukemea yeyote na ikibidi hata kuchukua hatua kama ilivyowezekana ku manage crisis ya Zitto na kundi lake.

Wanachama na wapenda mabadiliko tuache kutetea ovyo uongozi uliopo kwa namna mambo yanavyoenda. Chadema ina vijana wengi walioiva ni vizuri kupewa vijiti tuanze upya. Bila mabadiliko hali hii haishushi tu morali ya wanachama bali inazidi kupenya hadi kwa viongozi waandamizi.

Tuache kauli za kutiana moyo ambazo sasa zimegeuka faraja hewa kuwa chama kitabaki hata kama viongozi wake waandamizi wakiondoka. Chama kinapoteza watu muhimu kwa namna inayohitaji tafakari na fikra huru kubaini tatizo.

Napenda kurudia rai yangu, wanaoikumbuka vizuri sana NCCR watakuwa wanaogopa hata unyasi kwa yanayoendelea Chadema. Chama kinaelekea ilipo NCCR kama mzaha! Chukueni hatua badala ya kupeana moyo hewa.

Walau Chadema zama hizi kuna mitandao kuipa uhai kidogo tofauti na enzi za Mkapa na jinsi NCCR ilivyopotezwa na kubakia jina la Mbatia kwa sasa.
Mashinji anapwaya Jacob Meya wa ubungo achukue nafasi yake
 
Ukiona hivyo ujue mgao umepita.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mgao mkuu,unafiki alikua anamwona Dkt.Slaa ndio CDM,ukweli ni kwamba chama hiki kimo mioyoni mwa sisi vijana kwa wingi wetu hata Mbowe akiunga juhudi tupo imara na nikuhakikishie tupo vijana ambao tumeanza under ground movement na tumeplant vijana wengi ndani ya CCM mda utasema just wait.
 
Ukisoma hii taarifa mtaelewa kwanini tunasema kuna uzembe si kwa mbunge tu bali hadi chama. Mbaya zaidi ukichukua maelezo haya ya John Mrema ukaongeza utetezi aliotoa Nassari msibani majuzi kuwa alikuwa Marekani kutafuta wafadhili bado mnataka kudanganywa? Soma hii taarifa,

Mbunge wa Viti Maalum CCM, Amina Mollel amedai tangu Joshua Nassari alipochaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema, ametokomea kusikojulikana na hajui shida za wananchi waliomchagua.

Mollel ametoa madai hayo leo Jumapili Desemba 2, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na maji taka katika jimbo la Arumeru Mashariki uliofanywa na Rais Magufuli.

"Naamini walifanya makosa na hawatarudia tena 2020 na mimi niko hapa kwa ajili ya kuwasemea ili kuhakikisha shida zao zinatatuliwa," amesema Mollel. Katika uzinduzi huo Nassari hakuwepo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema Nassari yupo na wananchi wake na anafanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo katika sekta ya elimu na afya.

“Kuna kipindi Nasari alikuwa anasoma ila kwa sasa amemaliza na anaendelea na shughuli zake za Kibunge, Amina si msemaji wa wananchi wa Arumeru kazi hiyo ni ya wananchi wa Arumeru na kama alitaka kushitaki angewashitaki kwa Rais, mawaziri waliotajwa kutohudhuria vikao vya Bunge.

Kwa upande wake mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amemuomba Rais kuwasaidia kuondokana na shida ya maji kwa sababu wananchi wake wana hali mbaya.

Amesema hata akipewa nafasi kadhaa za kutoa maombi yake ili aweze kusaidiwa katika utekelezaji mara zote angetaja maji.

"Kama ulivyowakumbuka wenzetu wa Arumeru, tunaomba na sisi utukumbuke katika ufalme wako kwa sababu tuna shida kubwa ya maji," amesema Kalanga.

Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Ole Mollel amesema atahakikisha viongozi wa upinzani wanaopiga kelele wananyamazishwa ili chama tawala kiendelee kujenga na kuboresha uchumi.

"Tuhakikisha wote wananyamazishwa waache kupiga kelele hasa pale mambo mazuri yanapofanyika huku wao wakijaribu kuwapeleka wananchi katika mada zisizojulikana," amesema Mollel.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom