Uongo wa vifurushi vya Intaneti vya Airtel Tanzania

Jawai

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
530
405
Kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi ya vifurushi vya Internet. Tarehe 01/08/2022, nilijiunga na kifurushi cha Tsh.1500 (Mb850) na niliamua kuanza kufuatilia na kujipimia matumizi ya vifushi vya Internet kwenye simu yangu kupitia Mobile data usage ambapo nilipata fursa ya kuweka ukomo wa matumizi ya kifushi nilichojiunga kwa siku nisizidishe Mb100.

Lakini cha ajabu niliweza kutumia Jumla ya Mb490 pekee na kuletewa ujumbe kuwa nimetumia kifurushi cha Internet kwa 100%.

Nilishangaa sana na kugundua kuwa kumbe hivi viwango wanavyotuandikia ni Uongo mtupu. Huu mtandao wanafanya utapeli mkubwa sana.

Pamoja na maelezo haya nimeambatanisha screenshot za manunuzi ya kifurushi na matumizi.

Kama kuna mtu anaweza fuatilia pia ajaribu atajionea mwenyewe.

Screenshot_20220804-222533_Messages.jpg
Screenshot_20220804-222324_Settings.jpg
Screenshot_20220804-222442_Messages.jpg
 
Kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi ya vifurushi vya Internet. Tarehe 01/08/2022, nilijiunga na kifurushi cha Tsh.1500 (Mb850) na niliamua kuanza kufuatilia na kujipimia matumizi ya vifushi vya Internet kwenye simu yangu kupitia Mobile data usage ambapo nilipata fursa ya kuweka ukomo wa matumizi ya kifushi nilichojiunga kwa siku nisizidishe Mb100.

Lakini cha ajabu niliweza kutumia Jumla ya Mb490 pekee na kuletewa ujumbe kuwa nimetumia kifurushi cha Internet kwa 100%.

Nilishangaa sana na kugundua kuwa kumbe hivi viwango wanavyotuandikia ni Uongo mtupu. Huu mtandao wanafanya utapeli mkubwa sana.

Pamoja na maelezo haya nimeambatanisha screenshot za manunuzi ya kifurushi na matumizi.

Kama kuna mtu anaweza fuatilia pia ajaribu atajionea mwenyewe.View attachment 2316699View attachment 2316700

View attachment 2316701
Hiki kitu nilishawaambiaga humu, unanunua 1GB ila kimsingi unaungwa na qouta ya O.6GB, kwa sisi wenye uelewa kidogo na system zinavyofanya kazi ni rahisi tu, una edit statement tu ya ku display ujumbe unaandika uongo.

Mfano:
if (qouta ==O.6) {
print = "Umefanikiwa kujiunga na kifurushi cha week cha 1GB toka Airtel";
}

Ambacho utaona wewe ni huo ujumbe wa 1GB ila system imekuachia O.6GB kiuhalisia so unakuwa umepigwa 4OOMB bila kujua.
 
Ushuhuda sababu ya kuacha kutumia Airtel kwa mitatu japo ulikuwa mtandao wangu pendwa;

Hawa jamaa niliwakubali sababu kipindi kile walikuwa wanatoa Ofa za uhakika kwenye UNi Ofa.

Kuna siku nilijiunga Mb 500 ile kuingia notifications za YouTube ,Insta na wasap nikatumia text nimetumia 70% nikacheki sijakaa Sawa pale pale nikaambiwa nimemaliza.Ikatokeasiku nyingine video chache tu nikaambiwa nimemaliza na wakaniudhi sana connection ikawa kuipata kwa shida na kukwamakwama.

Nikachukua maamuzi magumu kwa hasira nikapopi majina muhimu na kutupa chooni line na kujipiza kutotumia huo mtandao tena maishani na ninafuraha kubwa kutimiza mwaka wa tatu sasa ila naona bado hawajarekebisha changamoto zao watu wanazidi kulalamika mambo yale yale.
 
Voda hata mimi siwapingi hakuna kitu kizuri kama kutodanganya ndio maana wanakula hela zangu nimejinga bando la wiki Mb 850 nakaribia natimiza siku ya tatu leo.

Nimepima 1.8 za Vida zinadumu kwa muda mwingi kuliko 2.2Gb za Halotel
Uko sahihi, nmeunga 1000mb za voda siku ya nne leo. Airtel niliunga mb1000 zikakata siku hio. Hio.
 
Halotel naogopoga sana kuweka bando mara kibao nikicheki kwenye data usage nakupigia hesabu Mb nilizoziona nakuta nimepigwa kama mb 160 na kitu kwenye GB2 vilevile watu kibao wanalalamika linaisha kwa haraka.

Sasa nipo Voda sijutii kuwa huku kabisa coz bando linaisha kihalali
Halotel na tigo wana kamchezo ka kutikisa net ukiwa na mb nyingi. Halafu muda wa kuisha wanaachia full speed
 
Back
Top Bottom