Uonavyo: Kati ya prof LIPUMBA na Dr SLAA ni nani zaidi?

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Watu hawa ni viongozi maarufu kutokea katika kambi ya upinzani. Wengi wetu tumekuwa na matarajio kuwa, upinzani ndio utaleta ukombozi wa kweli katika nchi hii. Je, kati ya majogoo hawa wawili, ni nani yuko juu zaidi ya mwenzake? Ni yupi anayeza kuthubutu kuwika mjini kwa sauti kuliko mwenzake? Ni yupi kati yao atakayeweza kuwaletea maendeleo watanzania haraka zaidi ya mwenzake? Je kwa upande wa CV zao, ni nani zaidi? Tusemezane kwa amani.
 
dk slaa yupo juu kisiasa kuliko prof lipumba kwa sababu mbalimbali ya moja mvuto wa slaa ktk jamii ,ujengaji wa hoja wake uko juu kuliko lipumba .kiusomi mmoja ni prof na mwingine nidr
 
Lipumba hatujamfaidi maana anakuaga mnafik mdamwingine. Hapendi kuona cdm ikubalikavyo! Slaa anaga izo. Yeye lengo kuu ni true changes in Tz.
 
Mkuu umepambanisha jiwe na kisiki!! Barcelona na Azam FC. Majibu unayo.

Dr. Slaa hapambanishwi na yeyote Bongo!! Labda tu chuki binafsi.
 
Dr. Slaa yuko juu. Angalia uchaguzi wa 2010 wa urais pamoja na kuchakachua Dr. Slaa alikuwa first runner up! Bila kuchakachua WINNER!!
 
Ni dhambi kubwa kumlinganisha Dr Slaa na Lipumba.Ni sawa na kichuguu na mlima Kilimanjaro.Hata kura za Urais walizopata mwaka juzi zinajieleza.Dr Slaa ni sawa na Real Madrid na Lipumba ni sawa na Lipuli
 
Kisiasa Dr. Slaa yupo juu sana. Si wa kulinganishwa na yeyote awaye kwa sasa ndani ya Bongo hii. Anajua Uongozi, mfano ni mafanikio ya Halmashauri zilizokuwa chini ya Chadema ukilinganisha na zile zilizo chini ya Magamba, wote tunajua ni juhudi na Ubunifu wa Dr. Slaa. Lipumba kisiasa, naona amechemsha, bora aendelee kuwa Mwanataaluma tu wa kipengele kimoja tu nacho ni Uchumi kwani maisha ni zaidi ya Uchumi.
 
Wewe umetumia kigezo cha usomi?wewe uwezi kuchekecha ubongo wako huo mdogo uliopewa??ukatoka na jibu?Lipumba ni sawa na Jahazi Slaa ni Meli ya Mizigo!Tazama utofauti uliopo.
 
Wewe umetumia kigezo cha usomi?wewe uwezi kuchekecha ubongo wako huo mdogo uliopewa??ukatoka na jibu?Lipumba ni sawa na Jahazi Slaa ni Meli ya Mizigo!Tazama utofauti uliopo.

Mkuu nimeweka hii baada ya kuona hawa watu wanasifiwa sana kila mtu kwa upande wake. Kutaka kujua nani zaidi kati ya hawa jamaa si kufikiri kwa ufinyu ila ni kwa mapana na marefu. Wote wawili wana umuhimu katika jamii yetu kutokana na michango yao. Sana nataka tupate nani zaidi ya mwenzake.
 
Lipumba bado hajaelimika japo amesoma,elimu si vyeti ni namna unavyoweza kuyatumia mazngira kuwa na faida na kuyatawala,je Lipumba ameshaifanyia nn Tz akumbukwe?usomi wake haunafaida Tz hanatofaut na Mongela,Migiro,nk.Maprof. wa ukwel ni Mwandosya na wengne anaofanana nao coz impacts zao zinaonekana kwa jamii.
 
mkuu au umeweka mada kutokana na mapokezi yake ya jpili, ni kweli ktk taaruma hasa vyeti vya uchumi yuko juu. Lkn uwezo wake kiuchumi ameutumia vipi kuinua uchumi wa nchi yetu? Niliwashaa watz wenzangu kumpokea pro Lipumba mapokez makubwa kuuliza sababu eti amesaidia kuinua uchum wa dunia na yuko 5bora kwa kuujua uchumi afrika, swali ni kiuchum wa tz tuko ngaz gani? Kisiasa Siraha anatisha kwa sasa bado hajapata mpinzani maana anajenga hoja za msingi majukwaani na sio misingi ya hoja kama wanasiasa wengne. Hongere Dr. SLAA uko juu.
 
mmeanzisha thread wenyewe mnachangia wenyewe.Tatizo imewauma sana mapokezi makubwa aliyoyapata mtaalamu wa uchumi duniani profesa lipumba.Si vibaya mkaendele kujifariji na 'msomi' wenu wa sheria za kanisani,
 
mmeanzisha thread wenyewe mnachangia wenyewe.Tatizo imewauma sana mapokezi makubwa aliyoyapata mtaalamu wa uchumi duniani profesa lipumba.Si vibaya mkaendele kujifariji na 'msomi' wenu wa sheria za kanisani,

Mkuu nani ni msomi wa sheria za kanisani?
 
Useless thread, hata kanumba akitaka kupokewa na umati Airport atapokewa ili mradi awe na pesa za kukodi mafuso, ukitaka kujuwa nani zaidi kati yao nenda tume ya uchaguzi au ingia mtandao wao anagalia matokeo ya Urais uchaguzi uliopita.

Thats it!
 
nchi kama US zina mambo fulani ambayo hupelekea kuwa mtu anayegombea uraisi ni lazima awe tajiri lakini kiukweli sio kuwa tajiri bali ni kuwa umefanikiwa kufutana na kazi ambayo mgombea (mtu) amekuwa akijishugulisha nayo kabla ya kutaka kuwania kuingia ofisi hiyo kubwa.

Ninachotaka kusema hapa ni mafanikio yanayoonekana kwa Dr. Slaa pamoja na mambo mengine ni katika uendeshaji (umiliki!??) wa hospitali/kituo ya CCBRT. Huyu mwenzake Prof. Lipumba nimjua siku zote kama mchumi aliyetukuka lakini sifahamu hasa kielelezo (visible/tangible) cha mafanikio yake kinachoweza kuonekana. Labda mwenye kujua atujuze hapa
 
Back
Top Bottom