Uoga wa Ku-Take Risk – Tofauti Kati ya Wazungu (Westerners) na Waasia/Mashariki (Easterners)

Uoga wa Ku-Take Risk – Tofauti Kati ya Wazungu (Westerners) na Waasia/Mashariki (Easterners)

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,990
Reaction score
12,019
Uoga wa kuchukua risk ni sumu kwa maendeleo. Hili ni tatizo kubwa sana kwa jamii nyingi za Kiafrika, na lina mizizi katika malezi, mfumo wa elimu, dini, na hofu ya kushindwa. Watu wengi wanajikuta wakiwa na ndoto kubwa lakini wanaziua taratibu kwa sababu ya uoga. Kwa nini?

Tuangalie mifano hai kutoka tamaduni mbili kubwa: Westerners (Wazungu) na Easterners (Waasia wa Mashariki).

1. Westerners (Mfano: Marekani, Uingereza, Australia)

  • Mfano: Elon Musk
    Aliuza kampuni ya PayPal akachukua mabilioni aliyoyapata na kuyahamishia kwenye SpaceX, Tesla na SolarCity – kampuni ambazo hazikuwa na uhakika wakati huo. Leo, ni miongoni mwa matajiri wakubwa duniani.
  • Mfano: Mwanafunzi wa Marekani
    Baada ya chuo, anaweza kuamua kuanzisha startup hata akiwa na mkopo wa elimu ya juu kama sie hapa Mkopo wa HESLB. Kwao, kushindwa ni sehemu ya safari, si mwisho wa ndoto.
  • Ukweli: Katika jamii hizi, mtu anaweza kushindwa mara kadhaa lakini bado akapata ufadhili wa mamilioni kwa idea nyingine mpya.

2. Easterners (Mfano: China, Japan, Korea Kusini)

  • Mfano: Jack Ma (China)
    Alikataliwa kazi zaidi ya mara 30, akakata tamaa? Hapana. Akaja na Alibaba, ambayo leo ni mojawapo ya makampuni makubwa duniani.
  • Mfano: Samsung (Korea)
    Ilianza kama kampuni ndogo ya kuuza vyakula. Leo ni empire ya teknolojia. Walichukua risk kuingia kwenye masoko yasiyojulikana wakiamini watajifunza wakiwa ndani ya vita.
  • Ukweli: Waasia wa mashariki wana nidhamu kali, wanafuata mfumo, lakini wanachukua risk kwa mpango – wanachanganya calculated risk na uvumilivu wa muda mrefu.

3. Sisi Je? (Wengi wetu hapa Afrika)

  • Tuna ndoto nzuri, lakini tunangojea “uhakika.”
  • Tunaogopa kuanza biashara kwa sababu “nani atanunua?”
  • Tunaogopa kuandika kitabu, kuanzisha podcast, kuomba kazi kubwa, kujaribu kitu kipya…
  • Tunaamini ukishindwa, umekuwa aibu ya familia, hii ni sababu hata uwezo wetu wa lugha za kigeni ni mdogo kwa sababu tunaogopa kujifunza, eti! tutachekwa tukipiga broken.
  • Sie mtu akichukua risk tunamcheka.
  • Dini imetufubaza kwa namna fulani tunadhani kwamba maisha ya duniani si lazima yawe bora, so tunaishi ili tutafute kula na kulala!

Je, Tutafikaje Mbali Bila Kuchukua Risk?

Hakuna mafanikio pasipo na hatari.
Kushindwa ni somo, si laana.
Risk sio ujinga, bali ni hatua ya kupima uwezekano na kuamua kufuata njia ambayo wengi hawawezi kufuata.

Tujiulize

  • Ni mara ngapi umezuia ndoto yako kwa sababu tu ya woga?
  • Ni kitu gani kingewezekana kama ungesema: "Nitajaribu tu"?
  • Kwa nini mtu kutoka Tokyo au Berlin awe jasiri kuliko wewe aliyezaliwa Mwanza, Morogoro au Mbeya?
Tufunguke. Tujaribu. Tushinde au tujifunze.
Risk is the price we pay for progress. Bila hivyo, tutaishia kuwa watazamaji wa mafanikio ya wengine kwenye YouTube na Netflix.
 
Unaongea jambo ambalo haulifahamu na kulijua hapa Tanzania ukiwa na wazo zuri ukiliwasilisha linaibiwa na hautopata vibali na mwisho hilo wazo lako utakuta amelichukua mwanasiasa Fulani anapiga hela.

Waulize Diaspora watakuambia.

Ndo maana unakuta watu tumeamua kufungua frame na kujibanza katika ajira za kimasikini Kama ualimu kwakuwa the house is leak.

Mimi huwa naamini idea is money MTU akiwa na wazo bora anabidi akalikopee pesa na Serikali impatie tax exempted.

Yaani ni bora kuwa na matajiri wachache ambao wata create ajira nyingi kuliko kuwa na watu wengi wenye hali za kawaida ambao wanaunga unga
 
Kikubwa maisha hayatabiriki,wapo walio take risk waka pass . Wengine wengi wali take risk ikawakatilia mbali.
Mfano kuna watu wamejiua kwa sababu mikopo nk
 
Oyaaaa,natarajia huu uzi uwe na wachangiaji wengi sana,unatuhusu sisi tulio wengi na roho za uoga
 
Na wakati huo viongoz wanatake risk kula kodi alf wanarudi kuongeza kua tukatwe tena na vocha 🥵🥵🥵🥵tunafanya sana tu hatuogopi ilaaaa🤯🤯🤯🤯🤯
 
Back
Top Bottom