Unyonyaji na unyanyasaji ndani ya chuo kikuu Bugando

Wakatoliki chuo chenu kinaaibisha ukristo nina mashaka na uhalali wa kanisa katoliki kujiita kanisa la kikristo. Povu ruksa
Waizi wametamalaki kila mahali mkuu, kwenye zile kanzu kuna watu wanapepea na sadaka
 
Halaaaa!!! Nimekupa mfano huo ili kukuonesha kwamba maamuzi yakishatoka huwa hayatenguliwi...na kanisa halijaribiwi....
Nakwambia hivi..kanisa haliwezi kukandamiza haki za watu alaf likaogopwa...ni ujinga...bima ni sh 50,400/= wao wanawakata 200,000/= alaf ww unaleta habar za ajabu hapa..
 
pole kwa wasomi wa CUHAS, ni vyema kuwauliza waliotangulia walipitaje na kama ni unyonyaji mpya hakuna kufumba macho mpaka kieleweke, japo kuna kupoteza muda wa masomo, kufukuzwa chuo na mengine mengi
 
kuna ulazima kusoma hapo tu...????? nazani kuna kile kipengele kuwa ada itapanda hata bila wanafunzi kupewa dhamana ya kujadiri na uongozi... na hili ni kwa vyuo vyote... na vingine wanasema kuwa pesa utakayo lipa kwa ada na application hazirudishwi...

yani hivi vyote pia wavielewe wanafunzi... Serikali pia ilisema haita ingilia shule binafsi ktk kupanga ada... nazani ndio mpaka chuo ili wanafunzi muende vyuo vya serikali... hivyo sizani kama utasikia tamko hapa ila kutakuwa na kicheko kutoka kwa mamlaka...

wakitaka na mkitaka serikali hiingilie kati nazani... ni kuundwa na mamlaka au sheria ya ku regulate hizo malipo ya vyuo na mashule na ruzuku watoe pia... kwa taasisi zote za serikali na binafsi ili ziweze jiendesha vizuri kama ilivyo katika taasisi za kiafya...
Kuandika tu hujui. Waste material!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
- Ubadhirifu wa fedha za wanafunzi masikini unaokadiriwa kuwa Zaidi ya billion 2.
- Wanafunzi hulipishwa Tsh 200,000/= ya matibabu ya Bima ya NHIF huku gharama za bima ni Tsh 50,400/=
- Ada hupandishwa kiholela, TCU na wizara kimya
- Uwakilishi wa wanafunzi wapigwa stop na utawala wa chuo
- Wanafunzi watozwa michango ya nyongeza Tsh 100,000 kila muhula
- Viongozi wa wanafunzi na wanafunzi hatarini kufukuzwa chuo

Huku hali ya sintofahamu ikiendelea kutawala ndani ya chuo kikuu cha UDSM kwa serikali ya wanafunzi,kwingineko ndani ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba CUHAS –BUGANDO yanaenddelea mambo ya kusikitisha sana katika taaluma ya Eimu ya Juu na Afya kwa ujumla. Kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vilivyoweza kuthibitishwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho walioonekana kukerwa na tabia ya uongozi wa chuo kukandamiza haki zao na kujipatia pesa kwa njia za magumashi walieleza kwa undani masaibu wanayoyapata.

Imeelezwa kuwa kwa kipindi chote wamekuwa na “KERO ZA KUDUMU” walizozitaja kama Upandishwaji wa ada kiholela, Utozaji wa pesa za matibabu ya NHIF Zaidi ya ile inayohitajika, Ukosefu wa uwakilishi wa wanafunzi katika vikao vya maamuzi, na Tabia ya utawala wa chuo kuwakandamiza wawakilishi wa wanafunzi.

Wakieleza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walisema kwa kawaida kila mwanafunzi anayesoma chuo chochote huchangia pesa ya matibabu kwenye mfuko wa taifa wa bima NHIF ambayo kwa mwaka ni Tsh 50,400 na mchangiaji hupewa bima ambayo hugharamia matibabu yote kwa mwaka mmoja. Kinyume na hilo chuo kwa muda wote kimekuwa kikitoza Tsh 200,000/= ambapo mwanafunzi hupewa bima ya NHIF na pesa ambayo hubaki yaani 149,600/= haieleweki hufanya kazi gani. Kila wanafunzi wanapo uhoji uongozi wa chuo kupitia serikali za wanafunzi hujibiwa kuwa hiyo ni sera ya muda mrefu ya chuo ambayo haiwezi kubadilika (Long standing policy).

Kwenye suala la ada ,kabla mfumo wa serikali kubadilika kutoka kwenye utaratibu wa wanafunzi kupangiwa na serikali kwenda Vyuoni kupitia TCU kwenda utaratibu wa kuomba wenyewe chuoni, TCU ilitoa ada elekezi ambayo kwa mwaka mara ya mwisho ada elekezi ya Bugando inaonesha kuwa ni shilingi 3,700,000/= lakini chuo kimekuwa kikitoza kati ya shilingi 4,150,000/= hadi 4,300,000/= . Kwa ujumla chuo kimejiongezea pesa taslimu shilingi 600,000 ambayo ni karibia na nusu ya ada ya chuo cha muhimbili.

Kwenye mfumo wa bodi ya mikopo kuna utaratibu unaoonesha kwamba kila mnufaika wa bodi ya mikopo huwa anapewa fedha za kujikimu pamoja na fedha ya mahitaji maalumu ya kitivo ambapo kwa BUGANDO kila mwanafunzi hupewa Tsh 150,000/= na bodi ya mikopo.Pesa hiyo ambayo kawaida anapaswa kupewa mwanafunzi chuo kinachukua pesa hii kwa matumizi ya chuo na ilhali wanafunzi hupewa vifaa ambavyo wenyewe wanadai havina thamani sawa na kiasi cha pesa wanacho gharamiwa na bodi ya mikopo.

Pia kwenye utaratibu wa utawala wa Chuo cha BUGANDO mwanafunzi anapochelewa kulipa ada kwa wiki moja ya kufungua chuo semester ya kwanza ya masomo hutozwa kiasi cha ziada kama faini ya takribani Tsh 100,000/= hata kama amelipa ada lakini hajamaliza. Ikumbukwe kuwa mchango mkubwa wa da hutoka bodi ya mikopo kwahyo hata pale bodi ya mikopo inapokuwa imetoa kiasi cha pesa anachopewa mwanafunzi lakini bado mwanafunzi anatozwa faini hiyo ya laki moja. Utaratibu huu wa chuo kuwalipisha wanafunzi pesa ya faini wanapochelewa kulipa ada hujirudia pia semester ya pili ambapo mwanafunzi hulipishwa tena 100,000/= .Kwa mantiki hii kwa wale watoto wa masikini ambao ndio wengi hujikuta kila mwaka wanapata faini ya shilingi 200,000/=

Katika hatua za kufuatilia hizi kero wanafunzi kupitia serikali za wanafunzi miaka yote wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo lakini walikuwa wakijibiwa kuwa hamna kinachoweza kubadilika kwani maamuzi haya hufanyika kwenye University Council isiyo na uwakilishi wa wanafunzi hali iliyofanya wapeleke malalamiko yao Serikalini na mpaka naandika uzi huu chanzo chetu kimetaarifu kuwa serikali kupitia vyombo husika bado iko kimya.

Ili kutatua changamoto hizi ,mwaka huu wanafunzi walifanya baraza la chuo ambapo waliamua kwa pamoja kumtaka makamu mkuu wa chuo apelike malamiko yao kwenye Baraza kuu la Chuo (University council). Katika kikao hicho wanafunzi walitoa dukuduku zao na makamu mkuu wa chuo kuzipeleka kwenye Council na pia kumtaka asisitizie kuhusu suala la uwakilishi wa wanafunzi katika University council.

Baada ya kikao cha Baraza la chuo maamuzi yaliyotolewa ni kuwapunguzia wanafunzi hela ya matibabu kutoka 200,000/= hadi 100,000= na kuwa na mwakilishi mmoja wa wanafunzi katika baraza la chuo. Lakini pia wale viongozi wawakilishi wa wanafunzi kupitia serikali ya wanafunzi walipewa mashitaka wakituhumiwa kuwashawishi wanafunzi kudai madai yao ambapo mpaka hivi naandika uzi huu viongozi wa wanafunzi BUGANDO wako hatarini kufukuzwa chuo.

Kwa haraka mpaka sasa ukijumlisha pesa inayofanyiwa ubadhirifu na watawala wa chuo hicho kwa wastani ni Zaidi ya 1,000,000/= kwa mwanafunzi mmoja na ukizidisha idadi ya wanafunzi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2500 hela hiyo inafikia zaid ya billion 2 kwa mwaka (yaani 600,000/= kama ongezeko la ada, 149,600/= ongezeko la pesa ya matibabu, 200,000 ya pesa ya faini pamoja na 150,000/=kama pesa maalumu ya vitivo).

Ufisadi huu unatisha sana ukizingatia hali duni ya maisha ya sasa hivi na ni aibu kubwa kwa serikali kufumbia macho suala hili linalowaacha watoto wetu wakiteseka. Ikumbukwe kuwa hawa ndio wataalamu wa afya wanaoandaliwa kwa ajili ya Taifa la kesho kwahiyo wanaponyanyaswa kwa namna yoyote ile baadaye tunakuja kupata wataalamu wa afya wasio wazalendo.

NAWASILISHA.

=======

UPDATES:

Viongozi wa wanafunzi wa Chuo wafukuzwa. Zaidi soma=>News Alert: - Viongozi wa Serikali ya Wanachuo na Wanachuo wa Chuo Kikuu Bugando Wafukuzwa Chuo!
Haki kwa watoto wa maskini iko wapi?
 
nasubili waraka povu ruksaaaa
hebu tuambieni kwA KIREFU yamefikaje hayo ya fukuzafukuza? sidhani kama chuo kinaweza fukuza mwanafunzi wake kirahisirahisi hivyo! Ukisikia mtoto alimuomba baba mkate, baba akamkata kichwa itabidi utafakari sana juu ya sababu halisi za maamuzi ya baba!
 
Nakwambia hivi..kanisa haliwezi kukandamiza haki za watu alaf likaogopwa...ni ujinga...bima ni sh 50,400/= wao wanawakata 200,000/= alaf ww unaleta habar za ajabu hapa..
Hao ambao wamekuwa na uthubutu na pia hawana woga(Students Govnr)...wako wapiii...???
 
Hivi hujui mwenyekiti wa TCU ni Mwalimu hapo? Prof Mutabaji
 
Kanisa Katoliki halijaribiwi na migomo na mobilization ya aina yotote.......

Elimu kwao ni huduma na sio biashara....Wanauwezo wa kufunga hicho chuo na kukigeuza kituo kikubwa cha kulea watoto yatima...
Usiwe blinded na udini kwa vitu simple to comprehend kama hiki. Sababu za vijana kufukuzwa ni kuhoji kwa nini kwenye medical capitation wanakuwa overcharged na hata kama uko tayari kwenye system ya bima bado unalazimishwa kulipa!! Does it bring sense? Kingine pale unapokuwa hujakamilisha ada hata kama ni laki mbili pungufu wanakataa kukusajili na ikipita week hujasajiliwa wanakupenalize Tsh. 100,000! Yaani wanakataa kukusajili ili waje wakupenalize baadaye!
Leo viongozi wenu wanafiki wameishia kuandika nyaraka kuelezea hali ya mambo nchini na wakati mwingine directly au indirectly huiokosoa serikali wakati kwenye taasisi zao kumejaa ufisadi na wao wakiwa front line, au ndio kusema nyani halioni kundule?
 
hebu tuambieni kwA KIREFU yamefikaje hayo ya fukuzafukuza? sidhani kama chuo kinaweza fukuza mwanafunzi wake kirahisirahisi hivyo! Ukisikia mtoto alimuomba baba mkate, baba akamkata kichwa itabidi utafakari sana juu ya sababu halisi za maamuzi ya baba!
Sidhan kama wao ni baba aisee hivi unaujua uchungu wa baba
 
Back
Top Bottom