Unyonyaji na unyanyasaji ndani ya chuo kikuu Bugando

Kanisa Katoliki halijaribiwi na migomo na mobilization ya aina yotote.......

Elimu kwao ni huduma na sio biashara....Wanauwezo wa kufunga hicho chuo na kukigeuza kituo kikubwa cha kulea watoto yatima...
Elimu hudumaa unayoisemea ni kama motto tu ila kiukwel wanafanyaa biasharaa.Afu sidhan kam watu kudai haki zao ni majaribuu
 
Kanisa Katoliki halijaribiwi na migomo na mobilization ya aina yotote.......

Elimu kwao ni huduma na sio biashara....Wanauwezo wa kufunga hicho chuo na kukigeuza kituo kikubwa cha kulea watoto yatima...
JE KAA NIWAFISADI WAKUBWA HAO WAKATOLIKI NA WANAKUWA WALAGAI HATA KUYAYASA WATOTO WA MASIKINI NI WATOTO YATIMA WATAWEZA, naona wewe una akili ndogo sana kwa hili wazo wako,pls elewa mambo kabla ya kucomment, have a great day
 
- Ubadhirifu wa fedha za wanafunzi masikini unaokadiriwa kuwa Zaidi ya billion 2.
- Wanafunzi hulipishwa Tsh 200,000/= ya matibabu ya Bima ya NHIF huku gharama za bima ni Tsh 50,400/=
- Ada hupandishwa kiholela, TCU na wizara kimya
- Uwakilishi wa wanafunzi wapigwa stop na utawala wa chuo
- Wanafunzi watozwa michango ya nyongeza Tsh 100,000 kila muhula
- Viongozi wa wanafunzi na wanafunzi hatarini kufukuzwa chuo

Huku hali ya sintofahamu ikiendelea kutawala ndani ya chuo kikuu cha UDSM kwa serikali ya wanafunzi,kwingineko ndani ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba CUHAS –BUGANDO yanaenddelea mambo ya kusikitisha sana katika taaluma ya Eimu ya Juu na Afya kwa ujumla. Kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vilivyoweza kuthibitishwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho walioonekana kukerwa na tabia ya uongozi wa chuo kukandamiza haki zao na kujipatia pesa kwa njia za magumashi walieleza kwa undani masaibu wanayoyapata.

Imeelezwa kuwa kwa kipindi chote wamekuwa na “KERO ZA KUDUMU” walizozitaja kama Upandishwaji wa ada kiholela, Utozaji wa pesa za matibabu ya NHIF Zaidi ya ile inayohitajika, Ukosefu wa uwakilishi wa wanafunzi katika vikao vya maamuzi, na Tabia ya utawala wa chuo kuwakandamiza wawakilishi wa wanafunzi.

Wakieleza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walisema kwa kawaida kila mwanafunzi anayesoma chuo chochote huchangia pesa ya matibabu kwenye mfuko wa taifa wa bima NHIF ambayo kwa mwaka ni Tsh 50,400 na mchangiaji hupewa bima ambayo hugharamia matibabu yote kwa mwaka mmoja. Kinyume na hilo chuo kwa muda wote kimekuwa kikitoza Tsh 200,000/= ambapo mwanafunzi hupewa bima ya NHIF na pesa ambayo hubaki yaani 149,600/= haieleweki hufanya kazi gani. Kila wanafunzi wanapo uhoji uongozi wa chuo kupitia serikali za wanafunzi hujibiwa kuwa hiyo ni sera ya muda mrefu ya chuo ambayo haiwezi kubadilika (Long standing policy).

Kwenye suala la ada ,kabla mfumo wa serikali kubadilika kutoka kwenye utaratibu wa wanafunzi kupangiwa na serikali kwenda Vyuoni kupitia TCU kwenda utaratibu wa kuomba wenyewe chuoni, TCU ilitoa ada elekezi ambayo kwa mwaka mara ya mwisho ada elekezi ya Bugando inaonesha kuwa ni shilingi 3,700,000/= lakini chuo kimekuwa kikitoza kati ya shilingi 4,150,000/= hadi 4,300,000/= . Kwa ujumla chuo kimejiongezea pesa taslimu shilingi 600,000 ambayo ni karibia na nusu ya ada ya chuo cha muhimbili.

Kwenye mfumo wa bodi ya mikopo kuna utaratibu unaoonesha kwamba kila mnufaika wa bodi ya mikopo huwa anapewa fedha za kujikimu pamoja na fedha ya mahitaji maalumu ya kitivo ambapo kwa BUGANDO kila mwanafunzi hupewa Tsh 150,000/= na bodi ya mikopo.Pesa hiyo ambayo kawaida anapaswa kupewa mwanafunzi chuo kinachukua pesa hii kwa matumizi ya chuo na ilhali wanafunzi hupewa vifaa ambavyo wenyewe wanadai havina thamani sawa na kiasi cha pesa wanacho gharamiwa na bodi ya mikopo.

Pia kwenye utaratibu wa utawala wa Chuo cha BUGANDO mwanafunzi anapochelewa kulipa ada kwa wiki moja ya kufungua chuo semester ya kwanza ya masomo hutozwa kiasi cha ziada kama faini ya takribani Tsh 100,000/= hata kama amelipa ada lakini hajamaliza. Ikumbukwe kuwa mchango mkubwa wa da hutoka bodi ya mikopo kwahyo hata pale bodi ya mikopo inapokuwa imetoa kiasi cha pesa anachopewa mwanafunzi lakini bado mwanafunzi anatozwa faini hiyo ya laki moja. Utaratibu huu wa chuo kuwalipisha wanafunzi pesa ya faini wanapochelewa kulipa ada hujirudia pia semester ya pili ambapo mwanafunzi hulipishwa tena 100,000/= .Kwa mantiki hii kwa wale watoto wa masikini ambao ndio wengi hujikuta kila mwaka wanapata faini ya shilingi 200,000/=

Katika hatua za kufuatilia hizi kero wanafunzi kupitia serikali za wanafunzi miaka yote wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo lakini walikuwa wakijibiwa kuwa hamna kinachoweza kubadilika kwani maamuzi haya hufanyika kwenye University Council isiyo na uwakilishi wa wanafunzi hali iliyofanya wapeleke malalamiko yao Serikalini na mpaka naandika uzi huu chanzo chetu kimetaarifu kuwa serikali kupitia vyombo husika bado iko kimya.

Ili kutatua changamoto hizi ,mwaka huu wanafunzi walifanya baraza la chuo ambapo waliamua kwa pamoja kumtaka makamu mkuu wa chuo apelike malamiko yao kwenye Baraza kuu la Chuo (University council). Katika kikao hicho wanafunzi walitoa dukuduku zao na makamu mkuu wa chuo kuzipeleka kwenye Council na pia kumtaka asisitizie kuhusu suala la uwakilishi wa wanafunzi katika University council.

Baada ya kikao cha Baraza la chuo maamuzi yaliyotolewa ni kuwapunguzia wanafunzi hela ya matibabu kutoka 200,000/= hadi 100,000= na kuwa na mwakilishi mmoja wa wanafunzi katika baraza la chuo. Lakini pia wale viongozi wawakilishi wa wanafunzi kupitia serikali ya wanafunzi walipewa mashitaka wakituhumiwa kuwashawishi wanafunzi kudai madai yao ambapo mpaka hivi naandika uzi huu viongozi wa wanafunzi BUGANDO wako hatarini kufukuzwa chuo.

Kwa haraka mpaka sasa ukijumlisha pesa inayofanyiwa ubadhirifu na watawala wa chuo hicho kwa wastani ni Zaidi ya 1,000,000/= kwa mwanafunzi mmoja na ukizidisha idadi ya wanafunzi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2500 hela hiyo inafikia zaid ya billion 2 kwa mwaka (yaani 600,000/= kama ongezeko la ada, 149,600/= ongezeko la pesa ya matibabu, 200,000 ya pesa ya faini pamoja na 150,000/=kama pesa maalumu ya vitivo).

Ufisadi huu unatisha sana ukizingatia hali duni ya maisha ya sasa hivi na ni aibu kubwa kwa serikali kufumbia macho suala hili linalowaacha watoto wetu wakiteseka. Ikumbukwe kuwa hawa ndio wataalamu wa afya wanaoandaliwa kwa ajili ya Taifa la kesho kwahiyo wanaponyanyaswa kwa namna yoyote ile baadaye tunakuja kupata wataalamu wa afya wasio wazalendo.

NAWASILISHA.

=======

UPDATES:

Viongozi wa wanafunzi wa Chuo wafukuzwa. Zaidi soma=>News Alert: - Viongozi wa Serikali ya Wanachuo na Wanachuo wa Chuo Kikuu Bugando Wafukuzwa Chuo!
Thanks so much sir for bringing this out in the light,i dont think that the regime or gava dont know, they must know coz we have TIS, whos work is to know such issues and inform the gorverment, but looking at your statement, this is purely a LEGAL ISSUE, someone MUST be held accoutable and answer charges before a court of law, why for instance charge 200,000 for health while its 51,000 by law,and i think catholic head must be aware of this, but tz has became so corrupt such that we dont even care for students from poor parents and yet this is a church college, reminds me of why the ex head of anglican church was kicked out of office, reason he leased churchs property at a cost of 2.7 us $ ,and thats a lot of money consdering that tz is a very poor country, churches my brother nowdays are much worse than CORPORATIONS, its better to deal with apple, amazon or google than some churches. be blessed and once again thanks for your info
 
kam
Sidhan kama wao ni baba aisee hivi unaujua uchungu wa baba
kama wanaijua kazi yao lazima wawe na uchungu na wanafunzi...hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na wakuu wa mshahara pia!
 
Hapa bado wahadhiri vitombi waliosemwa na mbunge aliyechukua jimbo la mamake
 
Hapa bado wahadhiri vitombi waliosemwa na mbunge aliyechukua jimbo la mamake
 
JE KAA NIWAFISADI WAKUBWA HAO WAKATOLIKI NA WANAKUWA WALAGAI HATA KUYAYASA WATOTO WA MASIKINI NI WATOTO YATIMA WATAWEZA, naona wewe una akili ndogo sana kwa hili wazo wako,pls elewa mambo kabla ya kucomment, have a great day
Sasa umeandika nini ndugu yangu? yaani hata kusoma inakuwa kero, tulia andika then pitia ndo upost.
 
Chuo cha KANISA hicho.
Full kunyonya.
Chuo cha Kikatoliki,na waziri MKATOLIKI wacha jamaa watambe.
Huwa njiuliza hawa jamaa wa awam ya V wanaweza kujivunia nini?Mbona mambo yapo worse zaidi ya JK?
 
kuna ulazima kusoma hapo tu...????? nazani kuna kile kipengele kuwa ada itapanda hata bila wanafunzi kupewa dhamana ya kujadiri na uongozi... na hili ni kwa vyuo vyote... na vingine wanasema kuwa pesa utakayo lipa kwa ada na application hazirudishwi...

yani hivi vyote pia wavielewe wanafunzi... Serikali pia ilisema haita ingilia shule binafsi ktk kupanga ada... nazani ndio mpaka chuo ili wanafunzi muende vyuo vya serikali... hivyo sizani kama utasikia tamko hapa ila kutakuwa na kicheko kutoka kwa mamlaka...

wakitaka na mkitaka serikali hiingilie kati nazani... ni kuundwa na mamlaka au sheria ya ku regulate hizo malipo ya vyuo na mashule na ruzuku watoe pia... kwa taasisi zote za serikali na binafsi ili ziweze jiendesha vizuri kama ilivyo katika taasisi za kiafya...
Chuo kama UDSM wewe kama ulianza na ada ya laki,atakayekuja hata akipangiwa laki 6 wewe uliyeanza na laki utaendelea na LAKI YAKO.
Hata ada za M PESA zina taratibu zake.
 
Kanisa Katoliki halijaribiwi na migomo na mobilization ya aina yotote.......

Elimu kwao ni huduma na sio biashara....Wanauwezo wa kufunga hicho chuo na kukigeuza kituo kikubwa cha kulea watoto yatima...
Kama wangekuwa na uwezo wangeshusha bei
 
Thanks so much sir for bringing this out in the light,i dont think that the regime or gava dont know, they must know coz we have TIS, whos work is to know such issues and inform the gorverment, but looking at your statement, this is purely a LEGAL ISSUE, someone MUST be held accoutable and answer charges before a court of law, why for instance charge 200,000 for health while its 51,000 by law,and i think catholic head must be aware of this, but tz has became so corrupt such that we dont even care for students from poor parents and yet this is a church college, reminds me of why the ex head of anglican church was kicked out of office, reason he leased churchs property at a cost of 2.7 us $ ,and thats a lot of money consdering that tz is a very poor country, churches my brother nowdays are much worse than CORPORATIONS, its better to deal with apple, amazon or google than some churches. be blessed and once again thanks for your info
Mkuu ungeandika Kiswahili fasaha ungeeleweka zaidi kuliko ulivyokoroga humu. Uzuri watanzania tunajuana wengi ‘Kiinglish’ kimekata kona. Wakati mwingne badilika.
 
Usiwe blinded na udini kwa vitu simple to comprehend kama hiki. Sababu za vijana kufukuzwa ni kuhoji kwa nini kwenye medical capitation wanakuwa overcharged na hata kama uko tayari kwenye system ya bima bado unalazimishwa kulipa!! Does it bring sense? Kingine pale unapokuwa hujakamilisha ada hata kama ni laki mbili pungufu wanakataa kukusajili na ikipita week hujasajiliwa wanakupenalize Tsh. 100,000! Yaani wanakataa kukusajili ili waje wakupenalize baadaye!
Leo viongozi wenu wanafiki wameishia kuandika nyaraka kuelezea hali ya mambo nchini na wakati mwingine directly au indirectly huiokosoa serikali wakati kwenye taasisi zao kumejaa ufisadi na wao wakiwa front line, au ndio kusema nyani halioni kundule?
Mkuu nimekupenda bure. Huyo jamaa huwa ni fara sana. Ana mahaba ya kimbwambwa. Bila shaka hata mleta mada ni mkristo. Huwa hataki kabisa taasisi zenye mafungamano na Katoliki zikosolewe. Sijui tulirogwa na nani majitu meusi. Ni msenge sana.
 
Mkuu ungeandika Kiswahili fasaha ungeeleweka zaidi kuliko ulivyokoroga humu. Uzuri watanzania tunajuana wengi ‘Kiinglish’ kimekata kona. Wakati mwingne badilika.
Aisee mkuu bora umemkosoa wewe. Sisi wengine angekula na tusi kwanza. His English is far worse than average.
 
Mtoa Mada Bugando ni Saut, mimi nimesoma Saut Mwanza! Haya madai ya Bugando ni sawa na mambo yaliyokua yanafanyika Saut...

Nakumbuka tulikua tunalipa Tshs 100,000 kila mwaka kama emergency, Hii pesa sijui ilikia inaenda wapi!! Ukichelewa kulipa Ada na Administration Fee unapigwa penalty ya LAKI MOJA!!
Utaratibu wa udokozi walianzisha Fr John Chacha, mwanasheria uchwara wa chuo,na Mwizi mwenzake Sister mmoja mkerewe jina limenitoka!! Wakatoliki ni wezi,na wanatumia ubabe,ukidai haki yako unafukuzwa mchana kweupe!!!
 
- Ubadhirifu wa fedha za wanafunzi masikini unaokadiriwa kuwa Zaidi ya billion 2.
- Wanafunzi hulipishwa Tsh 200,000/= ya matibabu ya Bima ya NHIF huku gharama za bima ni Tsh 50,400/=
- Ada hupandishwa kiholela, TCU na wizara kimya
- Uwakilishi wa wanafunzi wapigwa stop na utawala wa chuo
- Wanafunzi watozwa michango ya nyongeza Tsh 100,000 kila muhula
- Viongozi wa wanafunzi na wanafunzi hatarini kufukuzwa chuo

Huku hali ya sintofahamu ikiendelea kutawala ndani ya chuo kikuu cha UDSM kwa serikali ya wanafunzi,kwingineko ndani ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba CUHAS –BUGANDO yanaenddelea mambo ya kusikitisha sana katika taaluma ya Eimu ya Juu na Afya kwa ujumla. Kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vilivyoweza kuthibitishwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho walioonekana kukerwa na tabia ya uongozi wa chuo kukandamiza haki zao na kujipatia pesa kwa njia za magumashi walieleza kwa undani masaibu wanayoyapata.

Imeelezwa kuwa kwa kipindi chote wamekuwa na “KERO ZA KUDUMU” walizozitaja kama Upandishwaji wa ada kiholela, Utozaji wa pesa za matibabu ya NHIF Zaidi ya ile inayohitajika, Ukosefu wa uwakilishi wa wanafunzi katika vikao vya maamuzi, na Tabia ya utawala wa chuo kuwakandamiza wawakilishi wa wanafunzi.

Wakieleza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walisema kwa kawaida kila mwanafunzi anayesoma chuo chochote huchangia pesa ya matibabu kwenye mfuko wa taifa wa bima NHIF ambayo kwa mwaka ni Tsh 50,400 na mchangiaji hupewa bima ambayo hugharamia matibabu yote kwa mwaka mmoja. Kinyume na hilo chuo kwa muda wote kimekuwa kikitoza Tsh 200,000/= ambapo mwanafunzi hupewa bima ya NHIF na pesa ambayo hubaki yaani 149,600/= haieleweki hufanya kazi gani. Kila wanafunzi wanapo uhoji uongozi wa chuo kupitia serikali za wanafunzi hujibiwa kuwa hiyo ni sera ya muda mrefu ya chuo ambayo haiwezi kubadilika (Long standing policy).

Kwenye suala la ada ,kabla mfumo wa serikali kubadilika kutoka kwenye utaratibu wa wanafunzi kupangiwa na serikali kwenda Vyuoni kupitia TCU kwenda utaratibu wa kuomba wenyewe chuoni, TCU ilitoa ada elekezi ambayo kwa mwaka mara ya mwisho ada elekezi ya Bugando inaonesha kuwa ni shilingi 3,700,000/= lakini chuo kimekuwa kikitoza kati ya shilingi 4,150,000/= hadi 4,300,000/= . Kwa ujumla chuo kimejiongezea pesa taslimu shilingi 600,000 ambayo ni karibia na nusu ya ada ya chuo cha muhimbili.

Kwenye mfumo wa bodi ya mikopo kuna utaratibu unaoonesha kwamba kila mnufaika wa bodi ya mikopo huwa anapewa fedha za kujikimu pamoja na fedha ya mahitaji maalumu ya kitivo ambapo kwa BUGANDO kila mwanafunzi hupewa Tsh 150,000/= na bodi ya mikopo.Pesa hiyo ambayo kawaida anapaswa kupewa mwanafunzi chuo kinachukua pesa hii kwa matumizi ya chuo na ilhali wanafunzi hupewa vifaa ambavyo wenyewe wanadai havina thamani sawa na kiasi cha pesa wanacho gharamiwa na bodi ya mikopo.

Pia kwenye utaratibu wa utawala wa Chuo cha BUGANDO mwanafunzi anapochelewa kulipa ada kwa wiki moja ya kufungua chuo semester ya kwanza ya masomo hutozwa kiasi cha ziada kama faini ya takribani Tsh 100,000/= hata kama amelipa ada lakini hajamaliza. Ikumbukwe kuwa mchango mkubwa wa da hutoka bodi ya mikopo kwahyo hata pale bodi ya mikopo inapokuwa imetoa kiasi cha pesa anachopewa mwanafunzi lakini bado mwanafunzi anatozwa faini hiyo ya laki moja. Utaratibu huu wa chuo kuwalipisha wanafunzi pesa ya faini wanapochelewa kulipa ada hujirudia pia semester ya pili ambapo mwanafunzi hulipishwa tena 100,000/= .Kwa mantiki hii kwa wale watoto wa masikini ambao ndio wengi hujikuta kila mwaka wanapata faini ya shilingi 200,000/=

Katika hatua za kufuatilia hizi kero wanafunzi kupitia serikali za wanafunzi miaka yote wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo lakini walikuwa wakijibiwa kuwa hamna kinachoweza kubadilika kwani maamuzi haya hufanyika kwenye University Council isiyo na uwakilishi wa wanafunzi hali iliyofanya wapeleke malalamiko yao Serikalini na mpaka naandika uzi huu chanzo chetu kimetaarifu kuwa serikali kupitia vyombo husika bado iko kimya.

Ili kutatua changamoto hizi ,mwaka huu wanafunzi walifanya baraza la chuo ambapo waliamua kwa pamoja kumtaka makamu mkuu wa chuo apelike malamiko yao kwenye Baraza kuu la Chuo (University council). Katika kikao hicho wanafunzi walitoa dukuduku zao na makamu mkuu wa chuo kuzipeleka kwenye Council na pia kumtaka asisitizie kuhusu suala la uwakilishi wa wanafunzi katika University council.

Baada ya kikao cha Baraza la chuo maamuzi yaliyotolewa ni kuwapunguzia wanafunzi hela ya matibabu kutoka 200,000/= hadi 100,000= na kuwa na mwakilishi mmoja wa wanafunzi katika baraza la chuo. Lakini pia wale viongozi wawakilishi wa wanafunzi kupitia serikali ya wanafunzi walipewa mashitaka wakituhumiwa kuwashawishi wanafunzi kudai madai yao ambapo mpaka hivi naandika uzi huu viongozi wa wanafunzi BUGANDO wako hatarini kufukuzwa chuo.

Kwa haraka mpaka sasa ukijumlisha pesa inayofanyiwa ubadhirifu na watawala wa chuo hicho kwa wastani ni Zaidi ya 1,000,000/= kwa mwanafunzi mmoja na ukizidisha idadi ya wanafunzi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2500 hela hiyo inafikia zaid ya billion 2 kwa mwaka (yaani 600,000/= kama ongezeko la ada, 149,600/= ongezeko la pesa ya matibabu, 200,000 ya pesa ya faini pamoja na 150,000/=kama pesa maalumu ya vitivo).

Ufisadi huu unatisha sana ukizingatia hali duni ya maisha ya sasa hivi na ni aibu kubwa kwa serikali kufumbia macho suala hili linalowaacha watoto wetu wakiteseka. Ikumbukwe kuwa hawa ndio wataalamu wa afya wanaoandaliwa kwa ajili ya Taifa la kesho kwahiyo wanaponyanyaswa kwa namna yoyote ile baadaye tunakuja kupata wataalamu wa afya wasio wazalendo.

NAWASILISHA.

=======

UPDATES:

Viongozi wa wanafunzi wa Chuo wafukuzwa. Zaidi soma=>News Alert: - Viongozi wa Serikali ya Wanachuo na Wanachuo wa Chuo Kikuu Bugando Wafukuzwa Chuo!

Gharama za uendeshaji ziko juu sana.
Hivi vyuo havipokei ruzuku ya serikali kujiendesha, watu wanavyochelewa kulipa ada ndio chuo kinavyoshindwa kulipia huduma mbali mbali. Kwa hiyo lazima uwekwe utaratibu kuhimiza ulipaji ada mapema.

Masomo ya afya ni gharama. Kama vyuo vya binafsi vinavyotoa diploma tu za utabibu ada ni zaidi ya million NNE unategemea nini level ya MD?.

Hilo LA fedha ya bima linazungumzika kwani huduma ya bima kwa wanafunzi kwa 50400 halina muda mrefu sana na chuo kimekuwapo kabla ya hapo, walishajiwekea utaratibu. Kumbuka kwenye shule na vyuo hivi, michango ya namna hii huwa ni kwa lengo LA kuboost sehemu nyingine.
 
Mkuu ungeandika Kiswahili fasaha ungeeleweka zaidi kuliko ulivyokoroga humu. Uzuri watanzania tunajuana wengi ‘Kiinglish’ kimekata kona. Wakati mwingne badilika.
HAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA sawa mkuu, nitajitahiji niwe naandika swahili, ila swahili kwangu ngumu kidogo, lakini asante na barikiwa sana
 
Gharama za uendeshaji ziko juu sana.
Hivi vyuo havipokei ruzuku ya serikali kujiendesha, watu wanavyochelewa kulipa ada ndio chuo kinavyoshindwa kulipia huduma mbali mbali. Kwa hiyo lazima uwekwe utaratibu kuhimiza ulipaji ada mapema.

Masomo ya afya ni gharama. Kama vyuo vya binafsi vinavyotoa diploma tu za utabibu ada ni zaidi ya million NNE unategemea nini level ya MD?.

Hilo LA fedha ya bima linazungumzika kwani huduma ya bima kwa wanafunzi kwa 50400 halina muda mrefu sana na chuo kimekuwapo kabla ya hapo, walishajiwekea utaratibu. Kumbuka kwenye shule na vyuo hivi, michango ya namna hii huwa ni kwa lengo LA kuboost sehemu nyingine.
Ni kweli gharama za uendeshaji ziko juu. Je, hiyo ndiyo iwe sababu ya kuwaumiza wanafunzi. Na hii ya kukataa kumsajili mwanafunzi hata kama amelipa laki saba na nusu kapungukiwa laki mbili, unakataa kumsajili halafu baada ya wiki moja unampenalize laki moja kama late registration fee wewe unaona ni sawa kwa taasisi ya kanisa katoliki linalojinasinasibu kwamba kwao elimu ni huduma na si biashara! Ninaunga mkono serikali kuwashighulikia hawa jamaa coz ni wanafiki wako busy na nyaraka wakati wao wenyewe mafisadi kwenye taasisi zao
 
Back
Top Bottom