Serikali yaombwa kuingilia kati unyanyasaji kiwanda cha SBC Tanzania, Uongozi wagoma kufafanua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Said Ibrahim Stawi alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), Tawi la SBC Tanzania (Kiwanda cha Pepsi), ambaye aliachishwa kazi kwa kile alichodai ni harakati zake za kupigania maslahi ya wafanyakazi kiwandani hapo amesimulia mambo mbalimbali aliyokutana nayo kazini.

Stawi hayuko peke yake kwenye orodha ya viongozi wa wafanyakazi waliofukuzwa kazi katika kiwanda hicho kilichopo eneo la Vingunguti, Dar es Salaam.

Siku chache kabla ya kufukuzwa kwake, aliyekuwa Katibu wake Lucas Emmanuel Dundo pia alifukuzwa kwa madai hayohayo ya kusimamia maslahi ya wafanyakazi kiwandani hapo.

The Chanzo ilishindwa kupata maelezo ya upande wa pili wa uongozi wa kiwanda baada ya uongozi huo kugoma kujibu maswali yetu mahususi. Hata hivyo, uongozi huo umesema kama kuna madai yoyote dhidi ya kampuni yawasilishwe kwa njia rasmi kwa ajili ya utatuzi.

MADHILA MENGI
Wakati wakiongea na The Chanzo nyumbani kwa Stawi mnamo Machi 18, 2022, huko Kiwalani, Dar es Salaam, viongozi hao wa wafanyakazi walieleza kwamba wafanyakazi kiwandani hapo wanapitia madhila mengi ambayo yameshindikana kutatuliwa kwani kila anayejitokeza kuyaibua uongozi wa kampuni unamfutia kazi.

Madhila haya ni pamoja na madai ya kufanyishwa kazi bila ya mikataba; watu kufanyishwa kazi kama vibarua kwa zaidi ya miaka 20; na tuhuma za rushwa ya ngono ambayo wahanga wakubwa ni wafanyakazi wanawake.

Mengine yanahusisha watu kufanyakazi miaka mingi bila ya kuwepo kwa nyongeza ya mishahara; pamoja madhila udhalilishaji mahala pa kazi kama vile kukaripiwa kwa makosa madogo madogo na hata ubaguzi wa rangi unaoelekezwa dhidi ya wazawa.

“Sababu mama ya kunifukuza kazi ni ile tabia yangu ya kusimama kwenye haki za wafanyakazi,” Stawi, ambaye amekuwa akifanyakazi na SBC Tanzania tangu mwaka 2009, anaieleza The Chanzo.

“Yaani kwamba wao mpango wao ni kudhulumu mfanyakazi katika maisha yao ya kila siku,” anaongeza Stawi, ambaye kazi yake ilikuwa ni mtunza vifaa. “Mimi mpango wangu ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kila mtu anapata stahiki zake kulingana na sheria inavyosema. Kwa hiyo kitendo hicho cha mimi kusimama katika misingi ya kisheria na wao kusimama kwenye upande wa dhuluma ndicho kinachopelekea leo nafukuzwa kazi.”



ATHARI ZA KUFUKUZWA KAZI
Stawi ameileza The Chanzo kwamba uamuzi wa kufukuzwa kazi umemuathiri sana, akidai kwamba uamuzi huo umechangia kumpoteza kaka yake lakini pia ulimzuia binti yake ashindwe kufanya mtihani wake.

Kaka yake huyo alikuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi na alikuwa akimtegemea Stawi kwa ajili ya kukidhi gharama za maisha na matibabu.

“Sasa juzi [Machi 16] baada ya kupata taarifa kwamba mimi nimefukuzwa kazi, nasikia alidondoka ghafla na umauti wake ukamkuta papo hapo,” anaeleza Stawi. “Kwa hiyo, jana [Machi 17] wamemzika saa nne asubuhi. Kwa hiyo, haya maana yake kwamba, kaka yangu asingekufa kama sio maamuzi waliyonifanyia Pepsi.”

Stawi pia alipaswa kusafiri kwenda Songea ambako binti yake anasoma ili kutatua sintofahamu iliyokuwa imeibuka baina ya binti yake na uongozi wa chuo kuhusiana na suala la ada. Lakini kutokana na kilichotokea, na kulazimika kupigania ajira yake, alishindwa kufanya hivyo.

“Matokeo yake Jumatatu [Machi 14] wameanza mitihani, mtoto hakuingia kwenye mitihani,” anaeleza Stawi. “Hivi ninavyozungumza [binti yangu] hakufanya mitihani ya stashahada kutokana na jambo hili.”

Kupigania haki kumenigharimu
Kwa upande wake, Dundo anasema kwamba hali ya maisha imekuwa ngumu sana kwa upande wake tangu afukuzwe kazi, ukizingatia ana familia inayomtegemea, ikiwa ni mke na watoto wawili.

“Nilijitoa mhanga kwa ajili ya kuwatetea watu lakini mimi imekuja kunigharimu,” anaeleza Dundo kwa masikitiko. “Naona kama [ni] ushujaa lakini kihali ya maslahi imeniathiri.”

SBC TANZANIA WAULIZWA, MAJIBU YAO NI HAYA…
Foti Gwebe ni Msemaji wa Kampuni ya SBC Tanzania ambaye baada ya kutafutwa kutoa maelezo kuhusiana na shutuma zilizoelekezwa dhidi ya kampuni alisema:

“Wanajua utaratibu wa kampuni. Kama wanaona wananyanyaswa ofisini kuna utaratibu wakufuata, wafuate huo utaratibu.”

Gwebe aligoma kujibu maswali mahususi kutoka The Chanzo.

Stawi na Dundo kwa pamoja wameeleza kwamba Ofisi ya Kamishna wa Kazi inaelewa madhila wanayopitia wafanyakazi wenzao wa SBC Tanzania na licha ya kutoa maelekezo kwamba hatua za kuboresha ustawi wa wafanyakazi zichukuliwe maagizo hayo yamepita bila utekelezaji.

The Chanzo iliitafuta Ofisi ya Kamishna wa Kazi ili kujiridhisha kama madai haya ni ya kweli lakini ilishindikana kupata maelezo baada ya afisa anayehusika kuomba muda zaidi na kuturudia lakini mpaka wa kuandika habari hii hakuwa amefanya hivyo.

WAFANYAKAZI WASIKAE KIMYA
“Kiukweli, [wito wangu] kwa wafanyakazi [ni kwamba] hawatakiwi kukaa kimya kwa sababu hali hii itakuwa ni endelevu; itakuwa ni hali ya kurithishwa,” anashauri Dundo. “Na kwa Serikali [ni] kuweza kupita mara kwa mara na kuona vitu gani vinavyoendelea [kwenye maeneo ya kazi].”

Mbali na kuwataka wafanyakazi wenzake wasikate tamaa katika kudai haki na stahiki zao, Stawi pia alikuwa na haya ya kusema kuhusu mamlaka zinazohusika na kusimamia masilahi ya wafanyakazi nchini:

“Serikali mimi nailamu sana,” alisema Stawi. “Serikali imechangia mimi kufika hapa nilipofika. Kwa sababu siamini kwamba ipo Serikali duniani inayoshindwa kuchukua maamuzi dhidi ya mwananchi wake, au taasisi iliyo ndani ya nchi yake, inapofanya makosa. Serikali ijiangalie. Serikali ipo haja ya kupata meno ya kusimamia hivi vitu.”

Dundo na Stawi wameahidi kupigania haki zao kwa kuanzia katika Mahakama ya Kazi na ikishindikana kupata haki zao hapo wataendelea kwenda mahakama zingine za juu.

Source: The Chanzo


Pia Soma - TAKUKURU na Uhamiaji, Mchunguzeni Jitendra Shechwat wa Kiwanda cha Pepsi(SBC LTD). Anatuhumiwa kwa Rushwa na Unyanyasaji
 
Watanzania wacha kupiga kelele na kulalamika ukitegemea watu wengine wakupiganie, fanyeni maandamano hapo kiwandani, funga uzalishaji hapo hawa ni lazima wapelekewe moto ndio lugha wanayoielewa, sio kukimbilia kwenye social media kulalama,chomeni tairi hapo getini na malori yote ya pepsi yanayosambaza bidhaa hiyo ni target halali ni this battle
 
Watanzania wacha kupiga kelele na kulalamika ukitegemea watu wengine wakupiganie, fanyeni maandamano hapo kiwandani, funga uzalishaji hapo hawa ni lazima wapelekewe moto ndio lugha wanayoielewa, sio kukimbilia kwenye social media kulalama,chomeni tairi hapo getini na malori yote ya pepsi yanayosambaza bidhaa hiyo ni target halali ni this battle
Sio rahisi hivyo_Labda uwe hujawahi fanya kazi sekta binafsi

Huko unaweza kufanya migomo kama usemavyo na muitikio wao ukawa mzuri tu kwamba watafanyia kazi malalamiko yenu kwakuwa tu mmewashinikiza kwa nguvu ya dola

Kisha wakishaboresha kile mlicholalamikia inafuata hatua ya kupunguza wale wote waliotokeza kadhia hiyo mdogomdogo, ili isijirudie tena

Sasa kama una mpango wa kuwa Yesu kwa wafanyakazi wenzako sio mbaya

Na yawezekana ndio yaliyomkuta ndugu yetu huyo
 
Naomba kuuliza

Hivi serikali yetu ina kitengo cha wakaguzi wanaopaswa kutembelea sekta binafsi kujua hali za wafanyakazi.?

Maana hali zinasikitisha sana
Wapo lakini wakifika wanapewa bahasha na kuishia kughushi ripoti kamili.

Hapo wa kulaumiwa hasa wala sio wahindi bali ni wazawa wenzetu wanaopewa uongozi na wahindi na wao kujifanya sio wazawa tena, kupelekea kukandamiza wenzao.

Pia wakaguzi wa serikali na vyama vya wafanyakazi, hawa mara nyingi ndio wanakuwa wakandamizaji wakuu wa wale wanaopaswa kutetea. Hata kukiwa na malalamiko, wanachukua hongo na kutelekeza wale wanaolalamika.
 
Wapo lakini wakifika wanapewa bahasha na kuishia kughushi ripoti kamili.

Hapo wa kulaumiwa hasa wala sio wahindi bali ni wazawa wenzetu wanaopewa uongozi na wahindi na wao kujifanya sio wazawa tena, kupelekea kukandamiza wenzao. Pia wakaguzi wa serikali na vyama vya wafanyakazi, hawa mara nyingi ndio wanakuwa wakandamizaji wakuu wa wale wanaopaswa kutetewa. Hata kukiwa na malalamiko, wanachukua hongo na kutelekeza wale wanaolalamika.
Kabisa

Hawa vibisa wenye rangi nyeusi tiii.! kama mipingo na laana zao

Ndio wanaowafundisha wageni kuwa wanyonyaji na wanyanyasaji wa wazawa

Lakini hii laana mpaka iishe, itachukua mda kama hakutakuwa na uongozi thabiti
 
Naomba kuuliza

Hivi serikali yetu ina kitengo cha wakaguzi wanaopaswa kutembelea sekta binafsi kujua hali za wafanyakazi.?

Maana hali zinasikitisha sana
Sijui kama ulipata jibu la swali lako hili. Inasikitisha sana.
 
Hali kama hii zipo sana makampuni binafsi lakini wazawa hatuna ujasiri kwa sababu ya kulinda ajira zetu. Unaweza kuwa na uthubutu wa kupaza sauti mwishoni ukabaki mwenyewe..
 
Dawa yao ni kuacha kazi tu
Haya mambo ndio yalikuwaga kipindi cha shule,unaanzisha harakati fulani wenzio wapo nyuma yako,likitokea la kukutokea unajiona jasiri wenzio wanakusifia ule muda wa shule ile unaondoka ukiwa pekeyako njiani unajiona boya tu,
 
Wahindi ndio walivyo, wana deal na mwongoza movie kisha wanamu isolate halafu kazi inaendelea kama kawaida. Kwenye viwanda vya kanjbhai hivyo vyama vya wafanyakazi ni kama mapambo tu havina effects yoyote.
 
Back
Top Bottom