Arusha: Wafanyakazi 16 wa kiwanda cha kuchakata nyama wamlilia Rais Magufuli kutokana na kutimuliwa kazi kinyemela na kunyimwa stahiki zao

waziri2020

Member
May 31, 2019
46
125
Wafanyakazi 16 wa kiwanda cha kuchakata nyama cha jijini Arusha, (Arusha Meat )kilichopo chini ya jiji la Arusha, wamemlilia Rais John Magufuli awasaidie kurejeshwa kazini baada kufukuzwa kazi kinyemela bila kufuata taratibu na sheria za utumishi wa umma na kunyimwa stahili zao kwa miaka 4 sasa.

Baadhi ya wafanyakazi wamedai kuwa uongozi wa kiwanda umekuwa ukiwabambikia makosa ambayo hayana ukweli na wengine ambao ni wagonjwa kupewa barua za kusitishiwa mikataba wakiwa wamelazwa hospitalini kwa matibabu.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wengine huku akiangua kilio, Happy Ngowi ambaye alikuwa meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, alisema wanaomba Rais ambaye ni mtetezi wa wanyonge awasaidie kupata haki ya kurudishwa kazini pamoja na kulipwa stahili zao ili washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa nchi na pia kusaidia familia zao ambazo zinataabika kwa dhiki.

“Mimi nilipewa barua ya kuhamishwa Mwaka 2018 kutoka Arusha Meat kwenda jiji kama afisa mifugo, baada ya kulalamika nikapewa nyingine ya kurejeshwa na muda mfupi nikapewa barua ya kufukuzwa kwa madai ya uongo ya kujiongezea mshahara, sina uwezo huo wa kujiongezea mshahara wala daraja, juzi wamenifukuza kwenye nyumba nikiwa na kesi mahakamani, sina pa kuishi na watoto wanateseka”alisema.

Aidha amesema kwa Sasa amefukuzwa kwenye nyumba baada ya vitu vyake kutupwa nje kinyume na utarayibu

Mfanyakazi mwingine Fabian Kisingi ambaye alikuwa meneja mkuu alilalamika kuwa ameondolewa kazini kwa madai ya kushindwa kupanga majukumu kwa watumishi wa kiwanda ambapo alitakiwa kujieleza na alipofanya hivyo kwa barua lakini hakujibiwa, matokeo yake akapewa baraua ya kupumzishwa madaraka Mwaka 2018 na 2019 akafukuzwa kazi.

“Nilipewa barua mbili siku moja ya kujieleza bila kujibiwa nikapewa na kupumzishwa kazi, huu ni uonevu,naomba Rais aingilie kati kama tuna makosa ya kweli itabainika kama tunahaki itabainika, tuna watoto wanakwama kwenda shule kwa kukosa mahitaji ya familia, tulizuiliwa mishahara muda mrefu , hii ni nchi yetu sote tunaomba tuhukumiwe kwa haki sio uonevu”alisema Kisingi.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha alipotakiwa kuzungumdhia kashia hiyo alidai hawezi kuzungumza na asifuatwa fuatwe Kama kuku.

"Nimesema sitaki kuzungumzia Hilo suala na sitaki mnifuatefuate Kama kuku"alisema

Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Stephen Sulatan alipofuatwa na waandishi wa kujibu hoja hizo alijibu kuwa yeye si mwanasiasa na hayuko tayari kuzungumzia jambo hilo. “Mimi si Mwanasiasa ba siko tayari kuzungumzia jambo hilo kwani najua unanirekodi”alisema Sultan.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya kiwanda cha Arusha Meat Msafiri Sultan alipotakiwa kuzungumza na wanahabari alisema hawaruhusiwi kuzungumza chochote kwakuwa mzungumzaji ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha John Pima ambaye alipopigiwa simu hakupokea wala kujibu ujumbe wa maandishi wa simu ya mkononi.

Naye Meya wa jiji la Arusha Maximilian Iranghe alisema yeye ni mgeni bado hajajua lolote kuhusu Arusha meat na kuwataka waandishi kwenda kuzungumzan na uongozi wa kiwanda kwani wana mamlaka ya kuzungumza.

IMG_20210119_153049_964.jpg
View attachment 1683495 View attachment 1683498
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom