Unyanyasaji wa polisi (FFU) wanaolinda Ikulu dhidi ya raia - 20/09/2011

Tatizo kubwa ni ELIMU ya wanausalama wetu,Wanachotakiwa kufanya kwa mtu ambaye ni mgeni AMA hajui Kama kuna katazo la namna ni kutoa elimu kwa mtu waliyemkamata na c wao kutoza faini ukikamatwa toa onyesha ushirikiano Kama watakuwa wagimu waombe upelekwe kituoni tatizo letu watanzania tunapenda shortcuts unataka kunegotiate na polisi ili iweje sheria c zipo?
 
Ni tatizo la wananchi kutojua haki zao, huyo kijana alitakiwa asitoe chochote na awe tayari kwenda kuandikishana offence polisi na angelipa faini hata kesho yake

wale walinzi wa ikulu ni wanyanyasaji sana lakini bahati mbaya hawajui sheria wala mipaka yao....
 
Ndiyo maana taifa la TZ linazidi kuangamia kwa ajili ya machukizo kwa MUNGU
 
Watanganyika wanataka haki ya kupita maeneo yasiyo ruhusiwa, hayo ndiyo yanayoleta rushwa, mimi namuona huyu kijana ndio chanzo cha rushwa na unyanyasaji, kwa nini kama yeye ni mgeni asitafute mwenyeji amuendeshe, kwanza vibao vile ni vikubwa mno hakuna jinsi mtu mzima akaacha kuviona. Wakati tunatupia lawama jeshi la polisi ni vyema tukaacha kuvunja sheria kwa makusudi kwani huu ndio mwanzo wa rushwa.
 
Wataishia kulinda mageti tu kama kufuli

Na frustrations ndo zinawasumbua sana polisi hao. kumbuka hata kipindi kile wanaacha malindo ya Bank city centre kule na kuanza kukamata magari yanayofanya makosa ya barabarani kama kupiga U-turn, No entry n.k
 
macho yao yote barabarani badala ya ikulu.angekubali fine akalipe kituoni wampe na risiti(GRR)<br />
Hawana tofauti na wanaolinda MAJENGO ya benki wakiona umepita no entry wanaacha lindo.ndo maana watu wanaiba pesa na kuwapita mlangoni na smg zao..poor intelligence
Mkuu unataka waangalie wapi mwenye Ikulu aishi hapo kila siku trip
 
walitakiwa wamuelimishe.wamezoea hao.chukua hatua nenda moja kwa moja karipoti kwa kamanda kova au saidi mwema wanajali matatizo.
 
Inabidi Elimu kubwa ya Uraia itolewa kwa watu wote..Nkimaanisha raia wa kawaida na wale wanaojihusisha na usalama wa Raia (Polisi). kushika kirungu haimaanishi kukitumia hata kama haistaili kutumiwa. Mimi huwa nawashangaa sana hawa polisi wetu. Tunawajua vizuri hali zao na hali za familia zao na kiukweli kazi wanayoifanya ndio inawaweka mjini sasa pale wanapo itumia vibaya na siku wakafukuzwa kazi itakuaje??? Hilo ndio wanapaswa kujiuliza kabla hawajaanza kukiuka misingi ya kazi yao
 
Mie walinikamata mchana kweupeee saa tisa mchana mwaka 2009, sikusimama ila nilipunguza mwendo kukwepa watoto waliokuwa wanafukuzana na kucheza barabarani kwenye karibu na ufukwe wa Agha Khan, wakawa wanakimbizana hadi barabarani!!!

Nilishtukia gari yao imesimama mbele yetu katikati ya barabara then wakashuka na kuja kuvamia gari yetu, waliniudhi zaidi walipofikia kiwango cha kufungua mlango wa abiria wa mbele na kumshusha wife ili mmoja wao akae pale ili kunitisha!!!

Nilijikuta nimeshuka na kukabiliana na askari aliyefanya kitendo hicho na nikataka twende kwa kamanda wao wanieleze kosa langu ni lipi na faini nilisema nitalipia huko. Kuna mmoja alikuwa ni kidogo ni mwelewa ambapo alihisi ama nafahamu sheria kwa hoja nilizokuwa natoa au alishahisi tatizo mbeleni kwani alilazimika kuwatuliza wenzie na kuniomba niendelee na safari (si kuomba msamaha).

Niliamua kujiondokea ili kuepusha mlolongo wa mambo usio na maana, kwanza ukiwaona tu unajua ni FFU ambao kazi yao ni malindo bank na nyumba za wakubwa hawana kipato cha zaidi kama wenzao askari wa kawaida au trafiki, so pale huwa wanaforce riziki!!!!
 
Ngoja nitume kijana akiwa na wire kesho halafu tuone hiyo shughuli!!
 
Kwa lipi? ninachokieleza mimi ni kile kilichokutana nacho na kushauri uwe serious katika kujieleza..............sio unajieleza huku unang'ata vidole na kujenga mazingira ya kutoa kitu kidogo..........Come on baby......Hata Mahakamani hakimu anaangalia jinsi unavyojieleza na uzito wa hoja zako ndipo sheria hufuata baada ya kuona kama una kosa au la...............Nasema tena acheni KULIALIA Jieleze............



Acha kujishebedua,,,,unahisi hao polisi waliokushika ndio waliomshika jamaaa,,,????au kabla yako walishapita wangapi??????inawezekana walishakamata weng na wakahisi wanaweza kukuachia,kwan maeneo mangap huwa watu wanajieleza na hawasikilizwi???,je polisi watu ambao imewaua hawajui kujieleza,,,,,,,SHUKURU MUNGU IT WAZ UR LUCKY
 
Back
Top Bottom