Unyanyasaji wa Kijinsia - Leo Siku ya Kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyanyasaji wa Kijinsia - Leo Siku ya Kimataifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MAMMAMIA, Nov 25, 2011.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Leo ni Siku ya Kimataifa ya Unyanyasaji wa Kijinsia, mkazo ukiwa katika unyanyasaji wa wanawake majumbani. Inakadiriwa kuwa kila siku zaidi ya wanawake milioni 8 wanakumbwa na tatizo hili kwa namna moja au nyengine, ikiwemo kupigwa, kutukanwa, kubakwa na hata kuuawa. Ninawaomba Watanzania wenzangu tuwachane na tabia hii chafu.

  Kwa mwanaume, kwa nini umnyanyase mwenzako, mtu ambaye mko pamoja kwa mapenzi? Kumtesa si mapenzi. Kwa wmanamke, usikubali kunyanyaswa iwe kwa kisingizio chochote kile. Kumbukuka wewe ni binadadamu unayestahiki kuheshimiwa.

  Kwa wanaume na wanawake, tukumbuke kuwa tunaponyanyasa au kunyanyaswa, hili linawapa picha mbaya watoto wetu. Mvulana anayemwona baba anamnyanyasa mama, ataona unyanyasaji ni jambo la kawaida, na yeye akikuwa atafanya hivyo hivyo. Msichana anayeona mama ananyanyaswa, atalichukulia jambo hilo ni la kawaida, akikua na kunyanyaswa ataona aibu kushitaki manyanyaso anayoyapata kwa vyombo husika.

  Tuiadhimishe siku hii kwa kwa kauli mbiu hii - Piga ngoma, usipige mwanamke!
   
Loading...