Leo Machi 8, 2023 ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Una ujumbe gani kwa Mwanamke?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,066
Machi 8 ya kila mwaka, #Wanawake duniani kote huungana katika Kuadhimisha Siku hii kwa kukutana na kujadiliana kuhusu Mafanikio yao katika Sekta mbalimbali, Changamoto wanazopitia, na Jinsi ya kukabiliana nazo

Kaulimbiu ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa kuwajumuisha Wanawake katika masuala ya #Teknolojia na #Uvumbuzi, ili kuwawezesha kuendelea kutimiza Ndoto zao katika nyanja mbalimbali.
==============

Tarehe 8 Machi kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ama Siku ya Wanawake Duniani. Katika siku hii, wanawake wanakutana na kujadiliana kuhusu mafanikio waliyopata katika sekta mbalimbali, changamoto wanazopitia, na jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo. Kauli mbiu ya Siku hii mwaka huu ni “Dijitali: Uvumbuzi na Teknolojia kwa Usawa wa Jinsia.”

Kwa kaulimbiu hii, tunaweza kuona umuhimu wa ujumuishi wa wanawake katika masuala ya teknolojia na uvumbuzi, ili kuwawezesha kuendelea kutimiza ndoto zao katika nyanja mbalimbali. Mara nyingi wanawake wamekumbwa na unyanyasaji katika sehemu za kazi, biashara, elimu, na hata ndani ya ndoa.

Ni wakati sasa kwa jamii kuungana kwa pamoja na kuhakikisha haki za mtoto wa kike na wanawake zinatimizwa, ni wakati sasa kwa wanawake na wasichana kupewa nafasi sawa na wanaume katika maeneo ya kazi, na ni wakati sasa kuona kuwa, mwanamke si kiumbe dhaifu asiyejiweza, bali kutambua kuwa, mwanamke na mtoto wa kike ni nguvu kubwa katika jamii, na anapopewa nafasi, anaweza kufanya mambo makubwa.

Hivyo basi, katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake leo hii tutazungumzia mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wanawake katika kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni siku chache kabla ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake, pia inajulikana kama IWD, ilianzia katika harakati za wafanyakazi na ikawa tukio la kila mwaka linalotambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Mbegu za siku hii zilipandwa mwaka wa 1908, wakati wanawake 15,000 waliandamana katika jiji la New York wakidai muda mfupi wa kazi, mishahara bora na haki ya kupiga kura.

Mwaka mmoja baadaye, Chama cha Kisoshalisti cha Marekani kilitangaza Siku ya Kitaifa ya Wanawake ya kwanza.

Wazo la kuifanya siku hii kuwa ya kimataifa lilitoka kwa mwanamke anayeitwa Clara Zetkin, mwanaharakati wa kikomunisti na mtetezi wa haki za wanawake.

Alipendekeza wazo hilo mnamo 1910 kwenye mkutano wa kimataifa wa wanawake wanaofanya kazi huko Copenhagen. Wanawake 100 waliokuwepo, kutoka nchi 17, walikubali kwa kauli moja pendekezo lake.

Iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1911, huko Austria, Denmark, Ujerumani na Uswizi. Miaka 100 iliadhimishwa mwaka 2011, hivyo mwaka huu tunaadhimisha Kitaalamu Siku ya 111 ya Kimataifa ya Wanawake.

Mambo yalirasimishwa mwaka 1975, Umoja wa Mataifa ulipoanza kuadhimisha siku hii. Mada ya kwanza iliyopitishwa na UN (mwaka 1996) ilikuwa "Kuadhimisha yaliyopita, kupanga kwa siku zijazo".

Siku ya Kimataifa ya Wanawake imekuwa siku ya kusherehekea jinsi wanawake walivyofikia katika jamii, siasa na uchumi, huku mizizi ya siku hiyo ikimaanisha migomo na maandamano yanafanywa ili kuongeza uelewa juu ya ukosefu wa usawa unaoendelea.

Kwanini tarehe 8 mwezi Machi

Wanaharakati walishiriki katika maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake huko Toluca, Mexico mwaka wa 2022

Wazo la Clara la kuunda Siku ya Kimataifa ya Wanawake haikuwa na tarehe maalum.

Ilirasimishwa tu wakati wa mgomo wa vita mnamo 1917, wakati wanawake wa Urusi walidai "mkate na amani". Siku nne baada ya mgomo kuanza, Tsar alilazimika kujiuzulu na Serikali ya Muda ikawapa wanawake haki ya kupiga kura.

Tarehe ya kuanza kwa mgomo wa wanawake, kulingana na kalenda ya Julian, ambayo ilitumiwa wakati huo nchini Urusi, ilikuwa Jumapili, Februari 23. Siku hii katika kalenda ya Gregorian ilikuwa Machi 8 na ni tarehe hii ambayo inaadhimishwa leo.
Kwa nini watu huvaa rangi ya zambarau?
Rangi ya zambarau mara nyingi huhusishwa na Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwani inaashiria "haki na utu".

Zambarau, kijani na nyeupe ni rangi za IWD, kulingana na tovuti ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

"Zambarau inaashiria haki na utu. Kijani kinaashiria matumaini. Nyeupe inawakilisha usafi, ingawa hii ni dhana yenye utata. Rangi hizi ziliundwa na Umoja wa Kijamii na Kisiasa wa Wanawake (WSPU) nchini Uingereza mnamo 1908".

UN WOMEN
 
 
Kama unaufeminist ndani yako basi umepoteza sifa ya kua mwanamke
 
Wajipambanie kiuchumi kwa namna yoyote ile ,hata kwa utapel wa mapenzi , maisha ni magumu mno na mahitaji yao ni mengi mno, hilo ltafanikiwa kwa sababu wajinga niwengi mno.
 
Waache kujiuza na wajitambue
Umeniwahi,inaonekana hili wanaona ni jambo la kawaida,wakati kudhalilishwa kwa mwanamke kunaanzia hapa,wapambane sana na hili,ili kuhakikisha hadhi ya mwanamke inakuwa juu na aweze kuheshimika,Kingine ni Porn,hizi ikiwezekana dunia nzima zipigwe marufuku,kuna udhalilishaji mkubwa sana wa mwanamke kwenye hivi vitu......
 
Back
Top Bottom