SoC02 Unyanyasaji au Uonevu wa Kimtandao (Cyberbullying) umekuwa tatizo kubwa kwenye Jamii yetu

Stories of Change - 2022 Competition

Edward mbaga

New Member
Apr 1, 2019
3
2
Unyanyasaji wa kijinsia ni dhana pana sana ambayo ina ainanyingi sana ambazo kwa namna moja au nyingine zina muathiri mwanaume au mvulana Pamoja na mwanamke au msichana katika jamii zetu na kuna aina tofauti tofauti za unyanyasaji wa kijinsia ambazo ni ; Unyanyasaji wa kingono, Unyanyasaji wa kimwili, Unyanyasaji wa kihisia nakisaikolojia Pamoja na Unyanyasaji wa kijamii au kiuchumi.

Unyanyasaji wa kihisia na kisaikolojia ndio nguzo kwenyechapisho hili nahii ni kutokana na ukuaji wa sayansi nateknolojia hivyo kuibua matumizi makubwa ya mitandao yakijamii katika jamii zetu kwa nyakati hizi, pia unyanyasaji waaina hii unajumuisha unyanyasaji kwa kutumia maneno hivomoja kwa moja huathiri mtu husika kihisia na kisaikolojia , katika jamii yetu ya Tanzania tuna mifano Dhahiri kabisakwani wasanii wengi wamekua wakipitia masuala hayakupitia mitandao ya kijamii mifano mzuri ni msanii wamaigizo aitwaye Wema Isack Sepetu ambaye alipitia aina hiiya unyanyasaji.

Lakini swali kubwa ni kwamba kwanini wanawake ndiyohuwa wanazungumziwa Zaidi kwenye aina hii ya unyanyasajikuliko wanaume? kwani pia kuna baadhi ya wasanii wakiumeambao pia walipitia aina hii ya unyanyasaji lakini jambo hilohalikuchukuliwa kwa uzito kama lilivyo kwa wanawakemfano wa msanii huyo wa kiume ni JACKIE ambayealifaamika kwa jina la Bongo spiderman ambaye alipitia ainahii ya unyanyasaji lakini suala hili halikupewa uzito kama ule wa Wema Isack Sepetu.

Hivyo kuna namna katika jamii zetu kuna kutokuwa nauwiano katika kuyapa uzito masuala ya unyanyasaji wakijinsia kwa njia mbali mbali hasa huu unyanyasaji wa kihisiana kisaikolojia kwani mwanaume na mwanamke wote wahisia na wanaweza kuharibika kisaikolojia pia lakini kunaTatizo moja kubwa ambalo linachangia kutokuwa na usawa nauzingatiaji mkubwa katika unyanyasaji wa kihisia nakisaikolojia hasa kupitia mitandao ya kijamii ni kuwa hapaTanzania hakuna sheria ya moja kwa moja ya kuhukumu mtuambaye anatekeleza unyanyasaji au kuomewa mitandaonihivyo matukio kama haya yanakuwa na athari nyingi sanakwa watumiaji.

UNICEF walikuja na masuala kadhaa ambayokwa namnamoja au nyingine yangeweza kusaidia Wazazi wengi kuelewakuhusu suala la kuonewa au kunyanyaswa mtandaoni“cyberbullying” hivyo katika kuadhimisha siku ya mitandaosalama ilikuja na mbinu kadhaa za kuelimishanamna yakupambana na hali hizo hususani kwa Watoto hivyo UNICEF walitoa jumla ya mambo nane (8) ambayo Watoto wanayopaswa kujua kutambua ni kuwa ;

1. Uonevu wa Mtandao ni nini ?
2. Je, unawezaje kutofautisha kati mzaha na uonevu wamitandaoni ?
3. Yapi ni madhara ya uonevu mitandaoni ?
4. Nizungumze na nani iwapo nikifanyiwa uonevumtandaoni
5. Kusanya Ushahidi wa uonevu ili kukomesha inahitajikakutambuliwa na kuripotiwa
6. Jinsi ya kumsaidia Rafiki yake aliye onewa mtandaoni
7. Je , kuna adhabu ya uonevu mtandaoni ?
8. Nyenzo za mtandaoni za kuzuia unyanyasaji na uonevukwa Watoto au vijana

Hivyo hayo ni mambo kadhaa ambayo yangewasaidia wazazina Watoto ili kuepukana na uonevu na unyanyasaji katikamitandao ambayo yalitolewa na UNICEF.

Lakini bado hakuna sheria ya moja kwa moja ambayoinawahukumu moja kwa moja watuhumiwa wa unyanyasajiwa kimtandao ingawa Mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Wametoa adhabu kwa wale ambao watakuwa wamefanyamakosa hayo ya kimtandao ni kuwa mtu anayefanyaunyanyasaji mtandaoni, Atapigwa faini isiyopungua MilioniTano(5) au kifungo kisichopungua miaka mitatu (3) au vyotekwa Pamoja.
Nini madhara ya uonevu au unyanyasaji mtandaoni“cyberbullying” ?

Madhara ni mengi ambayo yanatokana na Unyanyasaji huuwa kimtandao kihisia na kisaikolojia ambayo kwa namnamoja au nyingine yanasababisha madhara makubwa kwa watuambao ndio wahanga wa hayo unyanyasaji huo. Yafuatayo nibaadhi ya madhara yatokanayo na unyanyasaji wa kimtandao;

• Kusongwa na mawazo na huzuni
Hii ni kutoka na mhanga wa jambo husika kukaa nakufikiria jinsi jamii ilivyochukulia mara baada yakukutana na aina hiyo ya unyanyasaji mara nyinginewatu huamua kufanya mambo yasiyopendeza kama vile unywaji pombe kupita kiasi.
• Kujilaumu na kujihukumu
• Kutengwa
Hii ni kutokana na jinsi jamii ilivyoona juu ya mhangaambaye amefanyiwa unyanyasaji huo hivyo watu wajamii husika kumtenga mtu wa namna hiyo.

• Mawazo na vitendo vya kujinyonga
Kutokana na kutojiamini wahanga wa unyanyasaji huuhuwa wanakuwa na msongo mkubwa wa mawazo nahupelekea kujidhuru hata kufikia hatua ya kujinyongakwani huona hakuna haja ya kuendelea kuishi.

Nini kifanyike ili kuepukana na madhara ya uonevu au unyanyasaji mtandaoni “cyberbullying” ?
Kama kuna madhara ya unyanyasaji huu pia kuna mambo ambayotukifanya kama jamii yanaweza kufanyika ilikuepukana na madhara haya ya unyanyasaji katika mitandao. Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kusaidia katikakupunguza visa na kuondoa kabisa unyanyasaji na uonevumitandaoni;

• Kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao yakijamii ili kuepukana na aina hii ya unyanyasaji kwanikwa kufanya hivyo itapunguza visa vingi vya uonevu au unyanyasaji mitandaoni.
• Kuwekwa kwa sera mbali mbali ambazo zitakuwa namaslahi mazuri juu utumizi wa mitandao ya kijamii.
• Uwepo uzito katika jamii zetu juu ya kuhukumu masualahaya ya uonevu mitandaoni
• Sheria zilizowekwa juu ya kudhibiti masuala haya yauonevu na unyanyasaji mitandaoni zizingatiwe ipasavyo.

Kwa njia hizo na nyingine nyingi zinaweza kusaidiakupunguza ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kimitandaokatika jamii zetu kwa kiwango kikubwa sana .
 
Back
Top Bottom