Unyama: Mtoto wa rafiki yangu amebakwa, wakamvunja na shingo

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
5,950
23,264
Ni Jambo la huzuni sana.

Jana tupo kazini mida ya saa nane mchana mara jamaa akapokea simu kutoka nyumbani,taarifa haikuwa nzuri Mara ghafla akaanza kulia. Tulipomuuliza nini tatizo akasema amepata taarifa mwanae ameng'atwa na nyoka porini kwa hiyo amekutwa amefariki. Ni binti wa kike anasoma darasa la tatu huko mkoani Mtwara.

Baada ya kupata taarifa hiyo mbaya tukafanya maandalizi,akasinidikizwa nyumbani ili akajiandae kwenda mkoani Mtwara kumzika mwanae.

Usiku saa 5 akanipigia simu kwamba walipopeleka mwili wa marehemu hospitali ya mkoa,ripoti ya daktari ilisema binti hakung'atwa na nyoka Kama walivyodhani,bali alibakwa Kisha akavyunjwa shingo na kutelekezwa porini.

Watu waliopeleka mwili hospitali walisema shingo ilikuwa imelegea sana kuliko kawaida. Na nadhani ripoti ya mchana ya kung'atwa na nyoka ilisambaa kwa sababu mwili uliokotwa porini, wakaamua kujiongeza kwa kudhani ni nyoka ndiye alimsababishia mauti binti mdogo.

Inasikitisha sana binti mdogo ambaye hawezi hata kujitetea kwa lolote unamfanyia ukatili na kumwondolea uhai,tena kwa kumvunja shingo..dah!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wa darasa la 3? Mbona haimake sense kwa mtu mzima kubaka mtoto mdogo kiasi hiki?

Sometime tunasema ni Imani za kushirikina, ila binafsi nasisitiza ile taarifa iliyosema kila penye watanzania wa5, mmoja ni kichaa, sio ya kuipuuzia.
 
Hii sasa imezidi, Yaani cha kushangaza hapo utaona hili linaishia ishia bila hatua kali, ila sasa ukiamua na wewe umvunje shingo mvunjaji ndio wanaibuka huko eti sheria mkononi, yaani hawana uchungu na wahanga wana uchungu na makatili wenzao.

Hapa ndio unaona uongozi upo kupiga tuu, watu wangeachwa waadabishane wenyewe kwa vikundi vya watu 10, anayezingua pakubwa anakatwa shingo chap.

Sio kundi kubwa lipo juu kijifanya anongoza kumbe, tumbo ndio lipo mbele.
 
Paedophiles wamejaaa kibaooo uraiani, na hawachelewi kuua.

RIP mtoto mzuri, poleee kwa Work mate wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa naonekana sina akili kwa mijitu mijinga kumpeleka mtoto wangu shule na kumrudisha.Eti nimuache ataongozana na wenzie!Haya ndiyo hunipa hofu.Tusiawaache watoto wasioweza kujitetea kwa mijahili ya dunia hii.
 
Pole na faraja ziende kwa baba na familia ya mtoto.
Binadamu tumekosa utu sana na hii inachangiwa na maadili mabovu na kukosa hofu ya mungu ndani yetu mtoto ukambake alafu ukatishe uhai dah inaumiza sana hakustahili adhabu hii hata kama ingekuaje
 
Usiku saa 5 akanipigia simu kwamba walipopeleka mwili wa marehemu hospitali ya mkoa,ripoti ya daktari ilisema binti hakung'atwa na nyoka Kama walivyodhani,bali alibakwa Kisha akavyunjwa shingo na kutelekezwa porini.
Polisi wakiwa makini watawakamata tu waliohusika, kutokana na DNA testing. Waangalie sehemu za kuchukua specimen kwenye mwili wa mtoto na kukagua eneo la tukio. Ila sasa, polisi wetu ni wazembe sijawahi kuona, sijui hata kama wanajua DNA testing maana yake nini
 
Tuwalinde sana watoto wetu dunia imekua sio sehemu salama kwao usimuachie mwanao mtu amlee uchungu wa mwana aujuae mzazi
 
Polisi wakiwa makini watawakamata tu waliohusika, kutokana na DNA testing. Waangalie sehemu za kuchukua specimen kwenye mwili wa mtoto na kukagua eneo la tukio. Ila sasa, polisi wetu ni wazembe sijawahi kuona, sijui hata kama wanajua DNA testing maana yake nini
DNA ni ngumu tyr watu wamemshika shika.
 
Back
Top Bottom