Ununuzi wa kiwanja Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ununuzi wa kiwanja Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Cassava, Feb 5, 2012.

 1. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Heshima kwenu wadau,

  Si watu wote wanaonunua viwanja mara tu vinapopimwa na manispaa husika, hii hutokana na kukosa pesa wakati huo, kutokuwa na habari au kuwa mbali wakati upimaji unapofanyika hivyo kutokutuma maombi. Kwa maana hiyo basi inapelekea kununua ki (vi)wanja kwa mtu aliyepimiwa na manispaa kwa bei ya juu kidogo.

  Sasa wadau wa mji kasoro bahari (MOROGORO) au wale wenye ufahamu wa mji huu, naomba kuhabarishwa ni njia ipi sahihi ambayo mtu hawezi kuingizwa mjini akinunua kiwanja kilichopimwa kwa mtu mwingine, hapa morogoro mjini. Manake viwanja huwa na migogoro sana, unaweza kuuziwa kiwanja walichokwisha uziwa watu wengine ikawa soo. Naomba kuelekezwa njia sahihui nisije lia manake pesa ya siku hizi imekuwa ngumu mno na kununua kiwanja ni kujibana.

  Nawasilisha.
   
Loading...