Ahmet
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 1,537
- 3,404
Habari za muda huu wapendwa, natumai Kila mtu ni mzima.
Acha leo niwaonyeshe uzuri wa mkoa wa Lindi, mkoa uliopo kusini mwa Tanzania. Watu wengi hasa kutoka kasikazini, magharibi au hata Kanda ya kati wanaweza wasiufahamu vizuri mkoa huu. Si ajabu mtu akakuambia hajui kama Lindi ni mkoa. Baadhi wanadhani ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Mtwara.
Mkoa wa Lindi ni watatu kwa ukubwa Tanzania kwani una kilomita za mraba 66040. Ukubwa wa mkoa huu ni asilimia 7.1 ya ukubwa wa Tanzania. Mkoa huu mkubwa umejawa rasilimali na vivutio vingi vyenye kustaajabisha na kupendeza machoni mwa wengi.
Basi bila kupoteza muda acha niwatembeze katika baadhi ya sehemu ambazo ni za kuvutia zipatikanazo mkoani Lindi.
1. Tendaguru formation, hapa ndipo yalipogunduliwa mabaki ya mjusi mkubwa ambayo yalichukuliwa na wajerumani (Dinosaurs). Picha ya chini ni mabaki ya mjusi huyo huko nchini Urejumani.
2. Magofu ya kilwa na Historia yake, dola ya Mrima, Kilwa ilikuwa na fedha yake. Magofu haya ni yenye kupendeza na huvutia watu mbalimbali kuja kuyatazma.
3. Selous game reserve, ni pori kubwa mno na wanyamwa wengi wapo hapa.
4. Fukwe za bahari ya Lindi, ni zenye kuvutia kwelikweli. Fukwe hizi zimepambwa na mchanga mweupe na miti mingi ya minazi pembezoni.
5. Cradle of Majimaji, mnara wa Nandete Kilwa ndio mahali ambapo Vita vikubwa kabisa vya Majimaji vilianza
6. Mazao Kama korosho, ufuta, miogo, mtama na vyakula vya bahari kama pweza, ngisi, uduvi n.k. vinapatikana kwa wingi mkoani Lindi.
7. Visiwa vizuri vyenye maajabu na Historia nzuri. Mkoa wa Lindi una visiwa vingi vinavyopatikana katika bahari ya Hindi, Sanje ya Kati, Songo mnara, Songo songo, Fanjove private island, Kilwa kisiwani ni baadhi tu kati ya visiwa vilivyopo mkoani Lindi.
8. Uwepo wa gesi asilia chini ya bahari, gesi iliyogunduliwa karibu na pwani ya manispaa ya Lindi inatajwa kuwa ndio nyingi zaidi kuliko ile ya Mtwara. Gesi asilia pia inapatikana katika wilaya ya Kilwa ambayo inachangia megawatt nyingi katika grid ya taifa.
Hakika Lindi ni pazuri, karibu Lindi.