University of Dar es Salaam(UDSM) Alumni - Special thread

Mimi nilikuwepo hapo 1972-75.

Nilihitimu na kutunukiwa BA in Janitorial and Bullshit science na baada ya hapo nikapangiwa kazi Nachingwea.
 
Mimi nlikuwa hapo 2006-2009 hadi namaliza chuo tuliwahi kugoma Mara kumi na moja...Mara maji hakuna, Mara boom limechelewa, Mara odong odwaa, kakatwa kugombea urais Wa chuo kiss mganda duhhhh.

2009huo mgomo ulinikuta,ambapo mkazi wa Hall II alipoteza maisha pale swimming pool,makaz ya Mkandala yaliharibiwa,na ndo hapo chuo kikaamua kuweka matenk makubwa mawili kila hall residence kama vile mabibo ,wakat huo wazir ea elim ni Maghembe.Ila pia ni kipindi hicho hicho na wahadhiri wa UDSM waligoma kwa siku kadhaa
 
Nilitiseka sana kutafuta kitabu Manitoba nilikua sijui utaratibu wa kuingilia mwenyewe kwenye kompyuta

Mkuu mimi library sijawahi ingia kusoma kabisa zaidi ya kufanyia ue tu ata utaratibu wake nilikua siujui 😝😝😝😝😝😝
 

Huo mgomo wa lecturers ndio uliongozwa na dr nyahoro nn alikua mtata sana huyu mzee katusumbua sana na kozi lake la foundation engineering second yr 😊😊😊
 
Mimi nilikuwepo hapo 1972-75.

Nilihitimu na kutunukiwa BA in Janitorial and Bullshit science na baada ya hapo nikapangiwa kazi Nachingwea.

Duuuh hiyo course nadhani currently haipo mkuu.......wewe ni nyani mzee😆😆😆😆
 
Huo mtindo ulikuwa zaidi pale hall 5 na hall two...

Daa miaka mitatu tumekula exile za kutosha saana.

Hahahaha umenikumbusha mbali sana mambo ya exile hata mabibo ilikuwepo sasa unapenyezewa tu text oya usije rum niko na shemeji yako tumepiga sana kambi chini ya vimbweta pale tukiwa exile😝😝😝😝
 

Kweli ulikua una haki ya kutoa machozi mkuu maana pale si mchezo wazee wamejaa roho mbaya tu, sisi department yetu mwanamke alikua mmoja tu nae ni secretary ila lecturers na TA 's wote wanaume wametutesa sana mkuu hii imepelekea graduates wengi kua na roho za kikauzu😎😎😎
 
Mkuu mimi library sijawahi ingia kusoma kabisa zaidi ya kufanyia ue tu ata utaratibu wake nilikua siujui 😝😝😝😝😝😝

Engineering wengi hawaingiagi libral labda wakiingia wanaenda kujisomea vitabu vyao wanavyoingia navyo wenyewe au soft copy...

But libral kuna usingizi balaaaa
 
Engineering wengi hawaingiagi libral labda wakiingia wanaenda kujisomea vitabu vyao wanavyoingia navyo wenyewe au soft copy...

But libral kuna usingizi balaaaa

Library kule kumetulia balaa usingizi nje nje😊😊😊😊
 
Reactions: itv
mkuu kama sijakosea ilikuwa 2008 na siyo 2009.
 
Haswaaaaa 100%
 
Sitakuja kusahau toka mwaka wa kwanza ckuwah Ku supp lakin mwaka wa Pili semester ya pil nilipata supplementary ya LL 2014, sikuweza kuichomoa hyo kozi na ikanibid ni carry mwaka wa tatu semester ya mwisho. Kilichonishtua ni kwamba sikuwah Ku supp sasa ile Ku supp Mara ya kwanza inakuwaje nashindwa kusapua mpaka naibeba hyo kozi mwaka wa tatu semester ya mwisho. Aisee mwaka wa tatu semester ya pil nimesoma kwa presha sana kutokana na hilo. Mwaka wa kwanza niliish hall 5 sasa mwaka wa pili na wa tatu nikawa naish msewe, changamoto za kwenda kusoma chuo usiku mm na jamaa zangu. Thanx God 2012 nilimalza fresh. Aisee Prof Said a Othman nusura anibakishe na hyo koz mwaka wa tatu, Cjui ingekuweje kushindwa Ku graduate kwa koz za arts wakat wazee wa koz ngumu wakivaa majoho.
 
Bila shaka wewe jamaa utakua LL.B....Tanchi stori ulipewa na kabudi....
 
kumbe ulikuwa COET, hahaha UDSM noma sana
 
Udsm, kweli ninepamis sana, nilikua hapo from 2008_2011, nilikua nakaa pale hall one kwa maseneta hahaha imagine kwa maseneta walikua wanakaa wanaume tu ila mimi jike peke yangu nlikua a room mitaa ile, yano niliachiwa room na boyfriend halafu yeye akahamia mabibo, weekend ndo akawa anakuja, tukaja kugombana sasa si nikamuachia room yake nikahamia zangu hall seven ambapo ndo ilikua room yangu niliyopangiwa

Later then he became my husband na tuna watoto wawili, sema yeye alikua mwaka wa nne sheria wakati mimi nipo first year,

Nakumbuka nlikua apenda sana kulala,kuna kipindi cha asubuhi nlikua nakichelewa kila siku mpaka lecturer akanikariri
 
Odong interpol walinrudisha kwao uganda baada ya ule mgomo uliosababisha chuo kufungwa, watu wengi walifukuzwa wengine walirudia miaka kama Antony machibya by then alikua rais wa daruso, ila odong jamani walimweka central almost wiki mbili kabla ya kumsafirisha,kuna siku mimi na best yangu tulienda kumsalimia odong central tuliwekwa kando tulihojiwa kama vile tumeenda kumtembelea gaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…