University of Dar es Salaam(UDSM) Alumni - Special thread

University of Dar es Salaam(UDSM) Alumni - Special thread

samuel faraj

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
1,326
Reaction score
1,269
Hii ni special thread wa ajili ya ex- Udsm students kushare moments mbali mbali tulizokutana nazo katika kipindi chetu cha masomo pale mlimani ziwe happy moments, sad moments etc.

Binafsi nilikua sijui history ya kikundi cha THE PUNCH, story za kina Nyerere kuchapa bakora.

Wanafunzi waliogoma enzi hizo, hebu tujiachie hapa kwa kuweka story mbali mbali tujifunze mambo mengi yaliyofanyika wayback tujifunze pia.

Mimi binafsi nilikuwepo pale tangu 2009-2013.

Ngoja ni share kidogo top 5 moments zangu na wengine mtiririke tuongeze siku.....

1. Nilitaka kuacha chuo week 1, 1st yr kisa ratiba ya vipindi nilichanganyikiwa kila kipindi kilicho kwenye ratiba nilikua naingia, brother mmoja ndo akanambia dogo hiyo ni ratiba ya college nzima akanisaidia kutick vipindi vyangu nikapata auheni (ushamba mzigo).

2. Tukiwa 2nd yr lecturers walikua aibu baada ya kwenda staff 8 kusimamia supplementary wanafunzi 5 wakafika wakajicheka wenyewe

3. Vituko vya dr.azafel fedha lwaitama alishawahi kuja darasani 2010 akatuambia jamani mwenzenu mwaka huu nakufa tukamuuliza kwanini akasema sheikh yahaya kasema mwaka huu wote tunaompinga jk tutakufa na mimi ni mmoja wao
Siku nyingine tena kaja kakuta ubao haujafutwa kaanza kuandika juu yake

4. Tukiwa 2nd yr ulitokea mgomo mkubwa wa kudai kuongezeka boom kutoka 5000-10000 kwa siku, sisi viongozi wa college yetu wakagoma wakasema wanataka walete official letter eti ili tujoin mgomo jamaa wakagoma matokeo yake wakaungana college zote kuja kutupiga college kwetu zilipigwa ngumi hatari matokeo yake tukafunga Mageti yote ya college yetu na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia ndani ya college kama hausiki ukikaidi kipigo cha haja kilikua kinatembezwa, tukaanzisha sasa ka mgomo ka kutaka mwenzetu mmoja aliekua amedisco arudishwe matokeo yake tukafukuzwa chuo kikafunga tulipo rudi wenzetu zaidi ya 100 walidisco kutokana na ratiba za mitihani tight

5. Kuingilia madirishani kwenye shuttle, purukushani zake zilikua si mchezo wale wa mabibo wanaelewa vizuri nishataka kupasua fuvu la kichwa siku moja baada ya kujigonga kwenye dirisha, mambo ya shuttlepori na kukomunika(kula mikate na chai pale boom linapokata).

Watu waliokua wanaongooza kwa kuoana na kufunga harusi enzi hizo ni waalimu kila siku mara vikao vya kitchen party, engagement mara sendoff.

School of Business: Hawa walikuwa wazee wa show off kuanzia wanaume kwa wanawake,
Law school wazee wa ma suti muda wote.

Engineering: Hawa ni desa boys non-complicators, very rough

Haya wazee wa zamani tiririkeni na nyinyi tufurahi...
 
Galadudu na @K4real walikuwa hapo miaka ya 2000...
 
Last edited by a moderator:
Mimi mwenzenu nili Disco!, sitaki kukumbuka!.

Pasco

Nakukumbuka ulikuwa na bodaboda yako ukitoka mabibo kwenda chuo unampa lifti yule mdada sijui ndo alikuwa shem
 
mdukuzi tupe na wewe ya kwako 😊😊😊
 
Last edited by a moderator:
mdukuzi tupe na wewe ya kwako 😊😊😊

Mi siku ya kwanza kupewa assignment mwalimu alisema anataka iwe kwenye soft copy yaan nusu darasa wakadhani soft copy ni makaratasi laini,mi nilikuwa nikifukuzia mzigo naualika hillpark lazima utaingia kingi tu,najifanya ndio viwanja vyangu kumbe wapi
 
Last edited by a moderator:
Mi siku ya kwanza kupewa assignment mwalimu alisema anataka iwe kwenye soft copy yaan nusu darasa wakadhani soft copy ni makaratasi laini,mi nilikuwa nikifukuzia mzigo naualika hillpark lazima utaingia kingi tu,najifanya ndio viwanja vyangu kumbe wapi

Hahahaha umenifanya nicheke kwa nguvu eti karatasi laini mlitisha sana wakuu
Hillpark ushuani palikua pazuri pa kukamatia watoto akitia maguu pale hachomoki 😊😊😊😊😊
 
Hahahaha umenifanya nicheke kwa nguvu eti karatasi laini mlitisha sana wakuu
Hillpark ushuani palikua pazuri pa kukamatia watoto akitia maguu pale hachomoki 😊😊😊😊😊

Maisha yanakwenda kasi sana ,
 
Maisha yanakwenda kasi sana ,

Hatari sana nakumbuka enzi izo tunaenda computers room wadau hawawezi ata kushika mouse wanainyanyua juu hawaweki chini😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom