Bila kusahau UDASA, sisi tulikuwa tunapaita YUDASA, ukipeleka mtoto wa kike pale lazima akuheshimu. Boom likikata unarudi zako manzese kula maandazi.
Mimi series nimezijulia Chuo, enzi hizo mnaenda kuangalia prison break chumbani kwa mshkj mwenye desktop. Computer zenyewe zilikuwa zimejaa tutorial tu a.k.a pilau (movie za ngono)
Watu tulikuwa tunachukulia boom dirishani karibu na ofisi za auxiliary police pembeni ya faculty of business siku hizi Ndio UDBS
Hivi siku hizi pepa za matriculation zipo? Ulikuwa huingii Chuo bila kufanya hizo pepa
Kuna mtu alikuwa anaitwa Pasiense Mlowe alikuwa anagombania uraisi wa DARUSO akichuana na Mganda anaitwa Odong Odwaa, huo mpambano asikwambie mtu ulikuwa kiboko. Utawala wanamtaka Pasiense wakati wanafunzi wanamtaka Odong. Pasiense alikuwa na Msemo wake mmoja "tofautisha Kati ya hamu na shauku"
Niachie hapo Ila UDSM is the best, pamoja na vioja vyote Ila nili enjoy maana Ndio kilikuwa Chuo cha ndoto zangu. Kusoma UD enzi hizo ni title mtaani.