Universe Ni Ndogo: No Light Years Between Planets Or Galaxies

Universe Ni Ndogo: No Light Years Between Planets Or Galaxies

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,395
Reaction score
1,439
Hi Guys!

Katika tafiti tulizokaririshwa na kuaminishwa, ni mengi tumeambiwa na wanasayansi wanaodai wametoka nje ya dunia. Mojawapo ya mambo tuliyoambiwa ni kwamba kuna miaka Billions Light years ndipo uvuke universe yetu.

Kama tunavyofahamu speed ya mwanga ni 3 × 10^8 m/s. Na ninaposema one Light year namaanisha usafiri kwa hiyo speed kwa mda wa mwaka mzima, huo umbali utakaoenda ndio tunasema one light year, nadhani unapata picha ni umbali kiasi gani itachukuwa kwa takribani 93 Billion light years ukubwa wa universe yetu, maana yake tangu uumbaji kuna sehemu mwanga haujafika bado unasafiri.

Telescope za NASA au SpaceX zimefanikiwa kuona maeneo mengi sana na ya many light years ndo ufike. Itakuwaje zenyewe zione hayo maeneo kwa mda mfupi wakati bado mwanga still unasafiri, na tunajua tangu uumbaji, piga ua garagaza hiyo miaka 93 Billion light years hatuna. Hapo ndipo nilipogundua kumbe Universe yetu ni ndogo sana. Au unawezekana speed of light ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri.

Pia nikatafakari nikaona kwamba mambo ya Time travel ni nadharia tu kwa mambo haya mawili yafuatayo.

1. Kama universe yetu ni ndogo basi hatutaweza kwenda future au past.

2. Kama speed of light ni kubwa kuliko tunavyodhani, basi Time Travel Mashine bado haijakidhi vigezo vya kutupeleka future au past.
 
Haya makolokolo huwa yanapunguza memory space kwenye ubongo wangu tu. Mke wangu aliniuliza time travel ni nini na inafanyaje kazi, nikamwambia niliona wamepost huko JF ila haieleweki sijui kama wengine wanaielewa.
 
Kumbe hata hujaelewa, zimeona hayo maeneo jinsi yalivyokuwa billions of years ago. Yani kile zilichokiona sasa ni cha hizo billion light years ago maana huo mwanga ulizofikia umetoka huko billions of light years ago.

According to physics universe had to be expanding or contracting at a speed of light. Einstein aligundua hili lakini akawa mwenyewe anapingana nalo, na kufanya formula yake ikubariane na upingaji wake, alaweka kitu kinaitwa cosomological constant which was a mistake ambapo baadae ilikundulika kuwa ni kweli ulimwengu unapanuka kwa kasi ya spidi ya mwanga, so mawazo ya Einstein yalikuwa sawa tu ila akajishtukia tu.
 
Kumbe hata hujaelewa, zimeona hayo maeneo jinsi yalivyokuwa billions of years ago. Yani kile zilichokiona sasa ni cha hizo billion light years ago maana huo mwanga ulizofikia umetoka huko billions of light years ago.

According to physics universal had to be expanding or contracting at a speed of light. Einstein aligundua hili lakini akawa mwenyewe anapingana nalo, na kufanya formula yake ikubariane na upingaji wake, alaweka kitu kinaitwa cosomological constant which was a mistake ambapo baadae ilikundulika kuwa ni kweli ulimwengu unapanuka kwa kasi ya spidi ya mwanga, so mawazo ya Einstein yalikuwa sawa tu ila akajishtukia tu.
Unapanuka kwa maana gani mkuu ?

Kwamba mwanzo ulimwengu ulikuwa kama puto alafu kadri siku zinavyokwenda ndo ulimwengu unapanuka kama vile ambavyo mtu anaouliza puto nalo kupanuka mkuu ama kupanuka kivipi ?
 
Haya makolokolo huwa yanapunguza memory space kwenye ubongo wangu tu. Mke wangu aliniuliza time travel ni nini na inafanyaje kazi, nikamwambia niliona wamepost huko JF ila haieleweki sijui kama wengine wanaielewa.
Yanaibua maswali mengi kuliko majibu. Kuyasoma na kuyazingatia Mambo ya unajimu ni kutafuta kichaa
 
Unapanuka kwa maana gani mkuu ?

Kwamba mwanzo ulimwengu ulikuwa kama puto alafu kadri siku zinavyokwenda ndo ulimwengu unapanuka kama vile ambavyo mtu anaouliza puto nalo kupanuka mkuu ama kupanuka kivipi ?
Ndiyo unapanuka kwa style hiyo tena kwa kasi ya mwanga
 
Ninachofahamu mimi ni kwamba mwanga husafiri katika mstari mnyoofu lakini niseme nuru yake/uangavu wake unamipaka/kikomo. Angalizo hakuna marefu yasiyo na ncha. Hao wanasayansi na hayo mavifaa yao wasituchanganye.
 
Nikisikia uwepo wa sayari nyingine zenye sifa tofauti na dunia tuishiyo naendelea kuchanganyikiwa.

Kama dunia ni sayari basi yake magimba mengine nane yaliyogunduliwa na wanasayansi kwenye mfumo wa jua yapatiwe jina tofauti na sayari.

Hatuwezi weka vitu vyenye sifa tofauti katika kundi moja.
Nini faida za moja kwa moja tunazozipata kutokana na kugundua mambo ya kwenye sayari nyingine?
Kwanini mataifa makubwa yana invest million dollars kwenye tafiti hizo?
 
Watakwambia ni mwanga kwanza unatakiwa ulifikie jicho ndo liweze kuona.
Hivi wakuu kwa anaejua spidi ya mwanga na spidi yakutazama kitu kwa macho inamaana spidi ya macho ni kasi kuliko ya macho...
 
Nikisikia uwepo wa sayari nyingine zenye sifa tofauti na dunia tuishiyo naendelea kuchanganyikiwa.

Kama dunia ni sayari basi yake magimba mengine nane yaliyogunduliwa na wanasayansi kwenye mfumo wa jua yapatiwe jina tofauti na sayari.

Hatuwezi weka vitu vyenye sifa tofauti katika kundi moja.
Kuna mwembe, kuna mpunga, kuna magimbi, kuna mchenza n.k, lakini yote ni mimea japo ina sifa tofauti lakini yote ni mimea tofauti yake ni kwamba kila mmoja una jina lake.
Hata sayari ni hivyo hivyo kuna sifa ya kitu kuwa sayari lakini kila sayari pia ina jina lake.
 
Unaelewaje nikikwambia huyu mbwa anakimbia kwa kasi ya gari? Au napo utaeuliza hilo gari linaenda wapi?
Masuala ya anga yanachanganya sana. Embu tufikirie kwa upana nje ya darasa kisha turejee kwa uchache darasani.
 
Back
Top Bottom