Unaombwa utoe ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo ya elimu ya Juu nchini ili hatimaye:
a. Migomo isiyo ya lazima isitokee
b. Elimu ya Juu inapatikana kwa kila atakaye
c. Familia zinaweza kumudu elimu ya juu
d. Elimu ya Juu inakuwa ni ya kiwango cha juu katika ubora wake na kuandaa wanafunzi katika ushindani wa soko la ajira la kimataifa.
e. Kuwaandaa wanafunzi kuwa watafiti na kuchangia utaalamu wao katika mabadiliko ya jamii yetu.
f. Kujenga nidhamu ya kisomi nchini.
NB: Yawezekana kuna kaubaguzi ka aina fulani hapa kwa kufocus kwenye elimu ya juu tu. Mniwie radhi.
Ngoja tuangalie haya yafuatayo:
(a) Elimu ya chuo kikuu ni ngumu na hasa katika mazingira ya hapa kwetu ambapo wanafunzi wanakuwa wanakabiliwa na ukweli kuwa wakifeli mitihani yao watafukuzwa na kupata fedheha kutoka kwa jamii yao. Kwa hiyo wanafunzi wengi walioko chuo kikuu huwa hawahitaji bughudha za aina yoyote kusudi waelekeze nguvu zao katika masomo. Hata hivyo wakishavurugwa kidogo tu, basi huwa hawawezi kabisa kugawanya muda wao kati ya kukabiliana na bugudha hizo na vile vile kufuatilia masomo yao. Huanza kwa kupuuza bugudha zile na kuendeleza nguvu zao kwenye masomo hadi pale inapoonekana kuwa bugudha zile hazitaondoka ndipo huamua kuweka masomo pembeni ili wakabiliane na budhudha zile kwanza. Sasa hicho ndicho chanzo cha migomo. Kumbuka kuwa vijana wale ni watu waliokomaa kiakili na wanasoma kozi tofauti tofauti huku wakitoka kwenye background tofauti vile vile. Wakishakubaliana jambo basi ujue jambo lile lina ukweli fulani na ni muhimu kwa viongozi kulichukulia jambo hilo kwa uzito unaostahili bila kutumia njia za mkato mkato.
(b) Serikali itambue kuwa elimu ya juu ni ya lazima kwa kila raia aiwezae. Katika bajeti ya serikali kuwe na kipaumbele kwenye elimu na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima. Mpaka sasa hivi Tanzania ina uwezo mkubwa sana wa kutoa elimu ya juu bure kwa raia wake wote ila tu haijapanga na kutumia raslimali zake vizuri. Mimi niliwahi kusoma na wanafunzi wa kutoka Botswana wakiwa wanalipiwa na serikali yao kuliko skolaship niliyokuwa nimepewa na wajerumani. Tunaweza kufanya ya Botswana bila wasi wasi kama viongozi wetu wataamua: Kupanga ni Kuchagua.
(b,c) Kumpa elimu ya juu kila aitakaye si jambo rahisi sana bila kuangalia uwezo wake. Nadhani tunachotakiwa hapa ni kuweka viwango vya elimu ya juu itakayolipiwa na serikali na ile ambayo kila mtu atajilipia binafsi. Mimi nadhani kwanza tunahitaji kuimarisha elimu ya sekondari na baraza la mitihani ili wanafunzi wote wamalizao form 6 wawe na nafasi sawa mbele uchaguzi wa kuingia chuo kikuu. Uvujaji wa mitihani na tofauti za mazingira ya masomo baina ya shule na shule huwafanya baadhi ya wanafunzi wawe "at a disadvantage" hata kama wana uwezo mzuri sana kimasomo. Baada ya kuwa ni standard nzuri huko sekondari, serikali iweke skolaship za kushindania na viwango vya kuzipata. Kwa mfano kuwe na skolaship za Engineering, Medicine, Law, Science, na specialization nyingine na viwango vyake vijulikane wazi wazi. Wanafunzi wa fom 6 waambiwe tangu huko form six kuwa washindanie skolaship hizo kutegemea na viwango vya pass zao za mitihani; viwango vyenyewe viwe reasonable siyo vile vya kukaangana. Kwa hiyo mwanafunzi anayeshindwa kufikia viwango vitakiwavyo kwenye skolaship zile aridhike kuwa hakufikia kiwango. Skolaship hizo ziwe zinalipia gharama zote za mwanafunzi siyo tena kudai michango kutoka kwa wazazi.
(c) Kwa wale ambao watashindwa kufikia viwango vya skolaship kwa margin ndogo wapewe second chance ama kwa kutakiwa warudie mitihani au wachukue mikopo ya elimu isiyokuwa na riba; na kuwe na utaratibu wa kuhakikisha kuwa mikopo hiyo inalipwa kweli.
(d,e, f) Viongozi wa taasisi za elimu ya juu wasiwe wanateuliwa na rais, badala yake wawe wanapatikana kwa search process. Kama CEO wa TANROADS alipatakana kwa search process basi hata viongozi wa vyuo vikuu wawe wanapatikana kwa njia hiyo. Hii itawafanya wawe more academic kuliko kuwa political. Kwa sasa wanafunzi wakiipinga serikali ya Kikwete, basi Mkuu wa chuo atachukua hatua ya kuwanyamazisha kwa nguvu akiogopa kuwa kikwete anaweza kung'oa kibarua chake hata kama wanafunzi wale wako sahihi. Ni muhimu wakumbuke kuwa Chuo kikuu kinaundwa na Wahadhiri, Wanafunzi, na Vyumba vya madarasa. Vitu vinginevyo vilivyoko chuo kikuu ni kwa ajili ya kusaidia Wahadhiri na Wanafunzi wakutanapo kwenye Vyumba vya Madarasa yao waweze kupanuana maarifa kwa ufanisi zaidi. Kwa sasa inaonekana kama vile Chuo Kikuu ni Viongozi!!