Ungekuwa ni wewe mdada ungefanyeje.

Ungekuwa ni wewe mdada ungefanyeje.

lucz

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2013
Posts
218
Reaction score
41
Habari zenu wana MMU. Nilikuwa na bf kwa bahati nzuri nina ujauzito wake.Nilipomwambia alinipa hela niitoe mimi sikuitoa nikakaa kama miezi miwili nikamwambia mimba sikuitoa kwa sababu naogopa kufa. Akasema atatoa matunzo nikijifungua na kudhibitisha mtoto ni damu yake ila kwa sasa hata changia chochote. Ungekuwa ni wewe ungefanyeje. Majibu ya kejeli sitapenda.
 
...ningekua ni wewe ningesubiri ,,,
 
Nachompendea MUNGU atatoa mtt kafanana nae hadi aone hayaa,na atamuhudumia mara atapomuonaa,jipe moyo mkuu wa uvumilivuuu utayashinda,pole
 
Nitaitunza mimba mpaka nitakapojifungua...akitaka kutoa matunzo kama alivyosema haya asipotoa pia yote heri...

Kama makosa yameshafanyika basi songa mbele na maisha yako Mungu ni mwema..
 
Hongera kwanza kwa kutokutoa mimba pia jitunze tu mpaka pale utakapoweza kuthibitisha kuwa ni wake na Mungu yupo
 
Eiyer ni sawa kwenye uzinzi lkn bora hajaitoa,kwan mtt hana kosaa azaliwe tu,kwani kosa lishatendeka hakuna jinsi na naamin kama ametubu ashasamehewa
 
Lakin si ulikubali kumwachia kitu......... Hakuna jinsi kubali kuubeba mzigo wako peke yako
 
Kauli aliyo itoa inaonesha hakuamini kabisaaa, hapo inawezeka na mmoja wenu ni kicheche.

Any way, ulikubalije kumpa zawadi ya mtoto wakati hakuamini ?
Kifupi mwenzio hakutaka kitokee kilicho tokea maana alitaka ale tu.
Kwa vile amekuambia hivyo, huna jinsi inabidi usubirie tu.
Kuhudumia ujauzito kazi kweli maana kuna mengi mama mjamzito ana-sacrifice kwaajili ya mtoto.
Komaa mwenyewe na hata usiwaze kusema ukijifungua atalea mtoto huyo maana ametoa kauli ya ki-play boy.
 
Ningekuwa mie nngelea mimba yangu peke yangu na nikishajifungua naendelea kumlea na kumtunza mwanangu peke yangu, halafu huyo mwanaume ole wake ajilete!
 
Eiyer ni sawa kwenye uzinzi lkn bora hajaitoa,kwan mtt hana kosaa azaliwe tu,kwani kosa lishatendeka hakuna jinsi na naamin kama ametubu ashasamehewa

Bado Mungu hahusiki ...!!!!!!
 
Ningekuwa mie nngelea mimba yangu peke yangu na nikishajifungua naendelea kumlea na kumtunza mwanangu peke yangu, halafu huyo mwanaume ole wake ajilete!

Ushauri wako nimeupenda nitaamua hivo.
 
Kauli aliyo itoa inaonesha hakuamini kabisaaa, hapo inawezeka na mmoja wenu ni kicheche.

Any way, ulikubalije kumpa zawadi ya mtoto wakati hakuamini ?
Kifupi mwenzio hakutaka kitokee kilicho tokea maana alitaka ale tu.
Kwa vile amekuambia hivyo, huna jinsi inabidi usubirie tu.
Kuhudumia ujauzito kazi kweli maana kuna mengi mama mjamzito ana-sacrifice kwaajili ya mtoto.
Komaa mwenyewe na hata usiwaze kusema ukijifungua atalea mtoto huyo maana ametoa kauli ya ki-play boy.

Tulitumia kinga kwa bahati nzuri imetokea hivo.
 
Ningekuwa mimi nafanya yangu.
Nalea mimba, after kujifungua nalea mtoto wala hata taarifa hapati!

Btw, ulishawahi kuyasaliti mahusiano yenu?
 
Tunza hiyo mimba na uzae,,,,, kwa sasa fanya kazi kwa bidii usave hela ya kukusaidia wakati wa kujifungua...............
Huyo kichaaa mwache kichaa chake kikipoa atarudi.
 
Back
Top Bottom