Unganeni kukikataa kikundi hiki kabla hakijakomaa zaidi ya hapa na kuwa kikundi cha hatari zaidi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Huu sasa ndio muelekeo kwenye Taifa moja katika Bara fulani ambako kuna chama fulani cha siasa sasa kimebaki chama siasa jina tu, ila kiuhalisia chama hicho kimegeuka kikundi cha watu wachache kilichokamata serikali (dola) katika nchi hiyo, na kinaweza fanya lolote pasipo hofu utadhani nchi hiyo haina sheria wala katiba.

Hivi sasa katika nchi hiyo, kikundi hiki cha watu wachache, kinaweza kufanya uhalifu wowote dhidi ya binadamu na bado kikapata utetezi mkubwa tu kutoka kwa watu mbalimbali na kinatumia "njaa" za watu katika Taifa hilo kama mtaji wa kupata ungwaji mkono/utetezi.

Kikundi hiki kinachojificha kupitia jina la chama cha siasa, kinaonekana kimeajiri vijana mitandaoni wenye kazi kubwa ya kutetea na ku-justify kila uovu unaofanywa na kikundi hiki dhidi ya binadamu wengine.

Kibaya zaidi, kikundi hiki kinatumia watu maarufu na wenye kuheshimika katika Jamii kama vile viongozi wa dini kutetea na kufunika maovu yao.

Kikundi hiki kimeweka mbele chama chao kuliko nchi, kimeweka mbele unyama kuliko utu, kimeweka mbele madaraka kuliko uongozi, kimeweka mbele fedha kuliko utu, kimeweka mbele dhuluma kuliko haki, kimeweka mbele ubinafsi kuliko utu, kimeweka mbele chuki kuliko upendo, kimeweka mbele amani kuliko haki, kimeweka mbele uongo na propaganda kuliko ukweli na uhalisia, kimeweka mbele kiburi kuliko unyenyekevu, n.k.

Kwa watu wa Taifa hilo, ni wakati sasa wa kuunganisha nguvu kukabiliana na kikundi hicho na wasitoe mwanya kikajimarisha zaidi kwani itafika hatua watakosa hata fursa ya kuelimishana kukipinga kwani hata access ya mitandao inaweza kuwa ni mtihani.

Samaki mkunje angali mbichi-Waswahili.
 
Mkuu hili siyo lile Taifa la Wadanganyika chini ya chama pendwa cha mafisadi (CCM)?
 
Ndiyo hivyo tena Hakuna Namna, Mchezo uliisha tarehe 28 Oct, 202.Kilichobaki ni only Kilio cha SAMAKI Machozi imekwenda na Maji "By Dr. Remmy Ongala''.
 
JIWE KUTOKA CHATO.
ameiweka CCM Yote na SELIKALI mfukoni Mwake atakalo taka anafanya.

Amevuruga uchaguzi ili awatawale vizuri WABUNGE NA MAWAZIRI WAMUABUDU YEYE KWA SABABU AMEWAPA UBUNGE WA BURE.
 
Back
Top Bottom