Wachumi wanaweza kutusaidia hapa, hivi inakuaje hapa? Nchi yetu inasifika sana kwa uzalishaji wa nafaka ya mahindi ukanda huu wa Afrika mashariki kuliko hata mchele, lakini bei ya kilo moja tu ya unga wa mahindi inakimbizana na bei ya kilo ya mchele.
Kinachonishangaza ni kitu kimoja, mzunguko wa pesa sio mzuri lakini pamoja na upatikanaji wa pesa kua mgumu lakini bado thamani ya shilingi haijapanda zaidi inashuka. Sasa kuna uhusiano gani kati ya kupanda kwa thamani ya shilingi na kuadimika kwa shilingi? Kuadimika kwa shilingi kunaweza kua suluhisho la kushuku kwa thamani yake?