mtotomtamuu
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 602
- 1,464
Ndiyo bei niliyopewa na muuza duka muda mfupi uliopita,, kutoka 1200 hadi 1600 hii hali sio nzuri.
Habari wanajf. Leo nimeamua kuzungumzia hili suala la kupanda kwa bei ya unga wa mahindi au sembe, sasa hivi unga wa sembe bei yake kwa kilo 50 imefikia 64000 wakati kilo 25 imefikia 32000 kwenye maduka ya rejareja imefikia kwa kilo wanauza 1500 hadi 1600 wakati hapo awali ilikuwa 1200.
Serikali pia inatakiwa kuliangalia suala hili mapema kwakuwa kwenye bajeti waliahidi mazao ya nafaka yatashuka bei kwa kupewa ruzuku.
Pia unga wa mahindi kwa kiasi kikubwa ndio mkombozi wa watu wa chini hata hali ikiwa ngumu mtu akishindwa kula ugali basi atakunywa uji.
Naomba kuwasilisha.