Underground Hip-Hop Tanzania ni chakula cha Ubongo

Mancobra

Member
May 31, 2021
53
125
Habari za wakati huu wakuu, mimi Ni mdau mkubwa wa game ya Hip Hop ya hapa Bong (mainstream na underground hip hop). Leo nataka tujadili kuhusu hip hop ya bongo especially, underground hip hop.

Underground hip-hop Ni aina ya rap inayofanywa na wasanii ambao wamejikita kuelezea matatizo yanayoikumba jamii. Aina hii ya rap ipo tofauti na mainstream rap kwa maana ya kwamba main stream rappers mara nying hujikita kwny kujisifia sana na kuongelea vitu ambavyo Ni entertainment sana mfano, kuwa na mademu wengi, kuonyesha pesa walizonazo, leo wamekula birian nyama, n.k.

Haya sasa turudi kwenye mada yetu, hapa Bongo underground rappers wapo wengi sana kuna akina Dizasta vina, manduka mc, Nacha, toxic fuvu, mbeya boy(chuma), stanza mobb, man cobra, n.k

Ukisikiliza nyimbo za hawa underground rappers utapata kitu ambacho ubongo utaanza kufanya kazi ya kutafakari jinsi maisha yalivyo na yanavyoendelea . Kupitia nyimbo za Hawa rappers utapata fursa ya kusikia matukio yaliyotokea/yanatokea, matatizo na changamoto kwny jamii na sometime njia za kutatua hizo changamoto. Mfano; ukisikiliza wimbo wa Dizasta vina wa kanisa kuna kitu utapata(kama bado Fanya wepes wa kutafuta), pia kuna ngoma ya Nacha; mdahalo, aah wapi na hodi hzo zote Ni chakula Cha ubongo.

Bila kuwachosha wadau wa hip hop, underground rappers Ni watunza mising ya hip hop yani nguzo za hip-hop.

Hivyo Basi wadau, hii rap inatakiwa ipate support kutoka kwa wadau ambao ni sisi wenyewe, tusupport kwa kununua album zao na kusubscribe youtube channel zao.

Kama tupo pamoja kwny kusupport harakat za kuwezesha underground rap, karibu utoe mchango wako jinsi Gani underground rap Ni chakula cha ubongo.

Karibuni kwa kutoa mawazo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom