Undani wa HLSSF ukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Undani wa HLSSF ukoje?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by gbrother, Sep 20, 2012.

 1. gbrother

  gbrother JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna taasisi iliyoanzishwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa chuo, inaitwa HIGHER LEARNING STUDENT SUPPORTING FUND, hivi inatambulika kisheria na iko chini ya nani? Naofia ya deci na kina malingumu yasijetokea then baadaye watu wakilia ndio tushituke.
  MSAADA WANAINTELLIJENSIA
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Hawa wanaweza wakawa ni matapeli 2!
   
 3. k

  kakamukubwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [h=2]MASWALI NA MAJIBU YAULIZWAYO MARA KWA MARA[/h] HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND (HLSSF).
  MFUKO WA KUSAIDIA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI.
  MASWALI NA MAJIBU YA MASWALA MBALIMBALI YANAYOIHUSU HLSSF.

  UTANGULIZI.
  Website: www.hlssf.org; e-mail: info@hlssf.org
  Contacts: +255 717 488 745/765 420 512.
  Telephone: +255-(0) 222183709.
  Fax: +255-(0)222183710.

  HLSSF ni NGO ambayo ilisajiriwa tarehe 30/10/2008 chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia na watoto.Ilipata usajiri namba 00NGO/00002621.

  SWALI: Je, HLSSF inatoa huduma gani kwa ujumla?
  JIBU: HLSSF inatoa huduma zifuatazo kwa kifupi;

  1. Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo.
  2. Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili.
  3. Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao.
  4. Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kisomi zaidi.Hii itafanikiwa kwa kuanzishwa kwa HLSSF ENTREPRENEURSHIP CLUBS kwenye vyuo mbalimbali nchini ambapo wanafunzi wanachama wa HLSSF watakutanishwa pamoja na kuweza kuandaa michanganuo bora.Hii michanganuo itatafutiwa mitaji na HLSSF ili kikundi husika cha wanafunzi waweze kuanzisha na kuendesha rasmi biashara yao.
  5. Kufanya utafiti juu ya matatizo mbalimbali yanayoikumba sekta ya elimu nchini;pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali juu ya uboreshaji wa sera husika.
  6. Kuendesha workshops,events na mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwapatia elimu pana zaidi wafanyabiashara na wanafunzi juu ya maswala ya ujasiriamali, uongozi wa biashara, upatikanaji na uboreshaji wa mitaji,risk management,changamoto za soko huria n.k
  7. Kutoa ushauri kwa wanafunzi wa sekondari na vyuoni juu ya namna ya kufanya uchaguzi sahihi wa michepuo ya kusoma pamoja na kozi muafaka za kusoma kulingana na changamoto za ajira za sasa.
  8. Kutoa msaada wa kufanya maombi ya vyuo kwa njia ya mtandao(TCU ONLINE APPLICATIONS) pamoja na kufanya maombi ya mkopo wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) kwa njia ya mtandao (HESLB LOANS ONLINE APPLICATIONS).
  SWALI: Je,Uanachama wa HLSSF unapatikanaje?
  JIBU: Uanachama wa HLSSF unapatikana kwa kufanya maombi ya uanachama.Maombi haya yanafanywa kwa kujaza fomu za uanachama kulingana na kundi lako husika;pia inabidi ulipe gharama ya uanachama kadiri ya kundi lako husika.Pia ambatanisha bank deposit slip ya malipo yako pamoja na fomu ya maombi iliyojazwa na kubandikwa picha na kuituma kwenye sanduku la posta la HLSSF au kuileta ofisini kwetu.

  SWALI: Uanachama wa HLSSF uko wa aina ngapi?
  JIBU: Uanachama wa HLSSF uko wa aina nne.Zifuatazo ni aina za uanachama:

  1. Uanachama wa mwanafunzi wa sekondari.
  2. Uanachama wa mwanafunzi wa chuo kikuu
  3. Uanachama wa mzazi/mlezi wa mtoto aliye mwanafunzi.
  4. Uanachama wa taasisi isiyo ya serikali,kampuni au chuo kikuu.

  SWALI: Ada za uanachama ziko vipi? Je, zinalipwa mara ngapi?
  JIBU: Ada za uanachama ni kama ifuatavyo:

  1. Ada ya uanachama wa mwanafunzi wa sekondari na mwanafunzi wa chuo ni Tsh.10,000.
  2. Ada ya uanachama wa mzazi/mlezi wa mtoto aliye mwanafunzi ni Tsh.50,000.
  3. Ada ya uanachama wa taasisi isiyo ya serikali,kampuni au chuo kikuu ni Tsh.100,000.

  ADA hizi zinalipwa mara moja tu;pale ambapo mwanachama anajiunga na HLSSF.

  SWALI: Kuna michango ya mwanachama au la?Kama ipo,Je ni ya aina gani?
  JIBU: Ndio kuna michango ya wanachama ya aina mbili.Michango hii ni kama ifuatavyo:
  1.Michango ya mwisho wa mwaka.Michango hii inategemeana na aina ya uanachama kama ifuatavyo:

  • Mwanafunzi wa sekondari atalipa Tsh.20,000.
  • Mwanafunzi wa chuo atalipa Tsh.30,000.
  • Mzazi au mlezi wa wanafunzi atalipa Tsh.80,000.
  • Taasisi ya serikali,kampuni au chuo kikuu kitalipa Tsh.200,000.
  NB: Hii ndio michango itakayo mtabulisha mwanachama husika kuwa ni "active member of HLSSF".
  2.Michango ya kila mwezi .Hii ni michango itakayofanyika kila mwezi kwa kiwango kitachoafikiwa na muhusika.Hii ni michango itakayofanywa na wazazi au walezi wa wanafunzi wa sekondari au chuo kwa lengo la kuwawezesha watoto wao kulipa gharama muhimu za chuo kwa miaka ijayo.Kulingana na makubaliano HLSSF itamuongezea mwanachama kiasi cha pesa kulingana na michango yake ya kila mwezi pamoja na mda wa kuchangia pindi tu atakapo taka kupata pesa hizo kwa ajili ya kusomesha mwanae.Mahesabu ya kiasi cha nyongeza kitakavyopatikana ni kama ifuatavyo(ORDINARY ANNUITY REFERENCE):

  Ordinary annuity ni michango inayofanyika kila mwisho wa mwezi.Kuna aina mbili za mahesabu;yale ya kutafuta thamani ya michango kwa kipindi kijacho ambayo imewekezwa kila mwisho wa mwezi.Kupitia haya mahesabu ndo itawezekana kukokotoa kiasi cha pesa kama ongezeko la faida/support atakayoongezewa mwanachama kulingana na riba itakayokuwa imepangwa.
  [TABLE="width: 60%"]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]
  C = Cash flow per period(michango ya kila mwezi)
  i = interest rate (riba ya mchango)
  n = number of payments (idadi ya michango kwa mwezi)

  FV ordinary annuity: thamani ya pesa ya baadae ya ordinary annuity.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Kama unataka kuelewa kwa kina juu ya taaluma ya annuities soma hapa chini:

  What Are Annuities?
  Annuities are essentially series of fixed payments required from you or paid to you at a specified frequency over the course of a fixed period of time. The most common payment frequencies are yearly (once a year), semi-annually (twice a year), quarterly (four times a year) and monthly (once a month). There are two basic types of annuities: ordinary annuities and annuities due.


  • Ordinary Annuity: Payments are required at the end of each period. For example, straight bonds usually pay coupon payments at the end of every six months until the bond's maturity date.
  • Annuity Due: Payments are required at the beginning of each period. Rent is an example of annuity due. You are usually required to pay rent when you first move in at the beginning of the month, and then on the first of each month thereafter.
  • [​IMG]
  • C = Cash flow per period(michango ya kila mwezi)
   i = interest rate (riba ya mchango kwa mwezi)
   n = number of payments (idadi ya michango)
  • FV ordinary annuity: thamani ya pesa ya baadae ya annuity due.Annuity due ni michango ya pesa inayofanywa kila mwanzo wa mwezi.Kanuni iliyo hapo juu ndio inayotumika katika kupata thamani ya baadae kwa kipindi maalumu kijacho inayofanywa kila mwanzo wa mwezi.

  SWALI: Je,Mwanachama atapata faida gani kutoka HLSSF?
  JIBU: Faida(Benefits) zinatofautiana kulingana na aina ya uanachama na viwango vya michango.Makundi ya benefits ni kama ifuatavyo:

  • Mwanachama active; mwanafunzi wa sekondari atapewa kipaumbele katika kupata mkopo wa masomo kutoka HLSSF pindi aingiapo chuo;pia atapata fursa ya kupewa scholarship ya kusoma ndani na nje ya nchi.
  • Mwanachama active; mwanafunzi wa chuo atapewa kipaumbele katika kupata mkopo wa masomo kutoka HLSSF, kupata fursa ya kutafutiwa ajira;pamoja na support za kupata pesa za mtaji kwa wale watakaotaka kujiajiri.
  • Mwanachama active; mzazi au mlezi wa mtoto aliye mwanafunzi atampa fursa nzuri kwa mwanae kupata msaada mkubwa wa kulipiwa gharama za masomo ya chuo.
  • Mwanachama active,kampuni/taasisi isiyo ya serikali au chuo kikuu atapata fursa ya kufanya projects na HLSSF pamoja na kuwa partner na HLSSF katika mambo muhimu ya jamii kwa ujumla.

  SWALI:Kuna namna ngapi za uanachama?
  JIBU: Kuna aina mbili za uanachama.Uanachama wa mtu aliye active na ule wa mtu asiye active.Hivyo basi kuna active members and passive members.Active members ni wale ambao wanalipa michango ya mwaka na wanashiriki katika mipango,vikao na shughuli mbalimbali zilizopangwa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa malengo ya HLSSF.Passive member ni yule mwanachama wa HLSSF ambaye bado halipi pesa za michango ya mwisho ya mwaka,hashiriki katika shughuli maalumu atakazo pangiwa na uongozi wa HLSSF.

  SWALI:Ni vigezo gani vinaangaliwa kwa ajili ya kupewa mkopo?
  JIBU: Vigezo/Sifa hizi ni:

  • Uwe raia wa Tanzania.
  • Uwe mwanachama wa HLSSF.
  • Uwe umefanya maombi ya mkopo pamoja na kuambatanisha nakala zote zilizotajwa kwenye fomu.
  • Bandika picha yako kwenye fomu za uanachama na fomu za mkopo.
  • Lipa Sh.10,000 kwa ajili ya ada ya uanachama;pia lipa Sh.20,000 kwa ajili ya maombi ya mkopo.Malipo yote yafanyike kwenye akaunti zilizotajwa kwenye fomu husika.Hakikisha unaambatanisha original deposit slip ya malipo yako kwenye fomu husika.
  • Mkopo utatolewa kwa wale tu watakao kuwa na ushahidi wa kwamba wamepata udahili katika chuo chochote nchini kinachotambulika kisheria kwamba kinatoa elimu ya juu.
  • Tuma maombi yako kwa njia ya EMS au posta kwa:
  MKURUGENZI MKUU,
  HIGHER LEARNING STUDENTS SUPPORTING FUND,
  UHURU STREET-KARIAKOO AREA,
  P.O BOX 41866,
  DAR ES SALAAM.

  • Hakikisha umejaza maelezo yote muhimu yaliyoulizwa kwenye fomu kwa kuwa yatatumika kufanya tathmini ya kupewa mkopo.
  • Kipaumbele ni kuwapa mkopo wale ambao hawatapewa mkopo na bodi ya mkopo ya serikali (HESLB).
  • Wale wanaotaka kusoma diploma,digrii ya kwanza watapewa kipaumbele katika mkopo huu.
  • Wale wanaotaka kusoma digrii ya pili,na PHD watafanyiwa mpango wa kupata scholarship za ndani na nje ya nchi.Wachache watapewa mkopo wa HLSSF.
  • Wafanyakazi;hususani wa serikali nao wanashauriwa kuomba mkopo kwa kuwa wao wanadhamana ya mshahara kupitia salary slip.
  • Kwa kipindi kijacho wale watoto wa wanachama wa HLSSF kupitia EDUCATION INSURANCE SYTEM ya HLSSF watapewa kipaumbele katika kupata mkopo wa HLSSF kwa kuwa watakuwa wanadhamana ya michango yao ndani ya mfuko wa HLSSF.
  • Kwa mwaka huu wa masomo 2012/2013; mwisho wa maombi ya mkopo wa HLSSF ni tarehe 30/10/2012.
  SWALI: Ofisi za HLSSF zinapatikana wapi?
  JIBU: Ofisi za HLSSF zinapatikana kwenye mtaa wa UHURU karibu na makutano ya barabara ya Lumumba na Uhuru; jengo linatazamana karibu na kituo cha kujaza mafuta GAPCO. Jengo linaitwa CALIST TOWER, PLOT NO 16, BLOCK 75, ghorofa ya TISA (9[SUP]th[/SUP] FLOOR). Office secretary wetu anaitwa DEVOTHA KILEO; namba yake ya simu ni +255 714 366 281. Endapo hautamkuta ofisini wasiliana nae kwa simu yake ili aweze kuja kuwahudumia.
  Telephone: +255-(0) 222183709.
  Fax: +255-(0)222183710.


  SWALI:Mikopo itatolewa lini?
  JIBU:Mikopo itatolewa baada ya vyuo mbalimbali nchini kutangaza wale waliopata udahili katika vyuo husika.Pia baada ya bodi ya mikopo ya HESLB kutoa list ya wale waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika bodi hiyo(HESLB).

  SWALI:Je,maombi ya uanachama wa HLSSF yana mwisho/deadline?
  JIBU: Maombi ya uanachama wa HLSSF hayana mwisho;yanafanyika wakati wowote wa kazi katika kipindi chote cha mwaka.

  SWALI:Nini umuhimu wa uanachama wa mwanafunzi wa sekondari ndani ya HLSSF?
  JIBU:Mwanafunzi wa sekondari anatakiwa kuwa mwanachama wa HLSSF ili aweze kutoa taarifa zake mapema juu ya masomo yake katika ngazi ya sekondari.Taarifa hizi zitatumiwa na HLSSF ili kuandaa mchakato wa kutafuta scholarship kwa ajili ya hawa wanafunzi pindi wamalizapo kidato cha sita.Pia itatoa fursa kwa hawa wanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kupata mkopo wa HLSSF pamoja na kusaidiwa katika kupewa ushauri wa kozi za kusoma vyuo vikuu,pamoja na kufanya maombi ya udahili TCU kwa njia ya mtandao;pia kupata msaada wa maelekezo juu ya namna ya kuomba mkopo wa HESLB kwa njia ya mtandao.
  SWALI: Fomu za uanachama na zile za maombi ya mkopo zinapatikana wapi?
  JIBU: Fomu za mkopo na zile za uanachama zinapatikana kwenye tovuti yetu ya www.hlssf.org. ziko kwenye homepage ya tovuti au kwenye kipengele cha admission au kile cha download application form.

  SWALI:Wanafunzi walio vyuoni(continuing students) wajaze fomu gani za maombi ya mkopo?
  JIBU:Wanafunzi walio vyuoni wanatakiwa kujaza fomu zilizoandikwa kwenye tovuti yetu kama "HLSSF LOAN FORM FOR MATURE ENTRY".

  SWALI:Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na wanajiandaa kuingia vyuoni wanatakiwa kujaza fomu gani za maombi ya mkopo?
  JIBU: Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na wanajiandaa kuingia vyuoni wanatakiwa kujaza fomu zilizoandikwa kwenye mtandao wetu kama "APPLICATIONS OF LOANS FOR UNDERGRADUATE STUDIES OF 2012/2013.

  SWALI:Je,wanafunzi wanaoomba udahili kupitia mature entry program;pamoja na wale walioingia vyuoni kupitia mature entry program wajaze fomu gani?
  JIBU:Wanafunzi wanaoomba udahili kupitia mature entry program pamoja na wale walioingia vyuoni kupitia mature entry program wanatakiwa wajaze fomu za maombi ya maombi ya mkopo inayoitwa kwenye tovuti yetu "LOAN FORM FOR MATURE ENTRY".

  SWALI:Je,kuna riba kiasi gani inayotozwa kwenye mkopo wa HLSSF?
  JIBU: HLSSF haitozi riba ya aina yoyote ila inatambua ongezeko la thamani ya mkopo wa HLSSF itakayotokana na kushuka kwa thamani ya pesa ya Tanzania;shilling,mabadiliko ya kiuchumi pamoja na changamoto la soko la fedha la kimataifa.Hivyo basi,kutakuwa na mahesabu ya thamani ya mkopo utakaorudishwa kama ifuatavyo:
  So, the following will be the calculation for future value of the loan for one who
  wants to obtain loan from HLSSF.


  Future Value of Loan = Lo + Lo *r *t Whereby: t: number of years taken to repay the loan. r: annual estimated financial markets fluctuation rate. Lo: This is the amount of loan presently borrowed. Future value of loan: This is the value amount of loan to be repaid after t years period. For example: If a student receives a Tsh.2 million loan from HLSSF in the academic year 2012/2013; he/she takes two years to start repaying the loan; while the estimated annual market fluctuation rate is 8%; then the following student will have to pay the following loan after two years. See the calculation below: Lo: Tsh.2,000,000. r: 8% t: 2 years Future Value of loan to be paid after 2 years is = 2,000,000 + 2,000,000*8%*2 = 2,000,000+ 4,000,000*0.08 = 2,000,000 + 320,000. = Tsh.2,320,000. For those who will receive HLSSF loan in the academic year 2012/2013. NOTE: We don't have interest rates. We have just recognition of market Fluctuation cost as described above.So, just take into consideration of the formula above. Repayment of loan. The repayment of loan will be done on monthly basis. The calculation for the amount is as follows. Amount to be repaid = 10% * monthly basic salary. For example: Consider the example of the loan taken by a student in the above question. This student will start paying the loan after 2 years and the Future value of the loan to be repaid is already calculated as shown above. Suppose after 2 years, this student obtains work that gives him a salary of Tsh.700,000 per month.Then,the following will be the calculation for the monthly loan repayment. Amount to be repaid monthly = 10% * 700,000 = 0.01 * 700,000 = Tsh.70,000. Since the total value of loan to be repaid is Tsh.2,320,000.Then, it will take the following months to be repaid = 2,320,000/70,000 = 33 months. NOTE: A 10% salary loan repayment rate is a minimal rate.Thus, others will be charged by actual figures or rates above 10% according to the agreements that will be made by the two parties; that is HLSSF and loan beneficiary. .

  SWALI:Je,mkopo utabidi urejeshwe kwa muda gani?
  JIBU: Kwa yeyote atayechukua mkopo wa HLSSF anabidi ndani ya miaka kumi awe amerudisha mkopo wote.Hii itategemea na makato ya mwezi pamoja na kiasi cha mkopo unaobidi kurejeshwa.

  SWALI: HLSSF itaweza kujiendesha kwa namna gani kwa kipindi kirefu?
  JIBU: HLSSF imebainisha vyanzo vingi vya mapato.Chanzo cha kwanza ni pesa za waanzilishi,pili ni pesa za wahisani,wafadhili na makampuni ya ndani na nje ya nchi,tatu ni pesa za wanachama wetu ambao watawekeza ndani ya HLSSF;pesa hizi zitawekezwa vizuri na zitazaa faida kubwa ambayo itawekezwa zaidi na nyingine kutolewa kama msaada na mkopo kwa watoto wa wanachama wa HLSSF.Pia kutakuwa na vyanzo vingine va pesa za miradi mbalimbali inayoendeshwa na HLSSF ambayo itakuwa inazalisha faida kubwa.
  Chanzo kikubwa cha pesa za kuendesha HLSSF ili iweze kuwa endelevu katika kutoa huduma zake ni ile program ya BIMA YA ELIMU YA JUU ambayo itatumika kukusanya michango ya wanachama wenye mikataba na HLSSF.Michango hii itawekezwa rasmi katika fursa nyeti zenye uwezo wa kuzalisha faida kubwa katika muda muafaka.
   
Loading...