Unazungumzia CCM ipi?

Ukiona wazee wa chama wanatoka hadharani kujisifu juu ya yaliyomtokea mtangulizi,

Jua kuwa wameshagawana fito za nyumba Yao.
Lakini la kushangaza ni kwamba, pamoja na kugawana fito hizo bado wanaendelea kujenga nyumba ile ile waliyomo; iwe mbovu au imara, hayo hayawahusu wao, mradi manufaa yanawafikia wao.
 
Tanzania ni nchi yenye usiri mkubwa mno, na bahati mbaya sana wananchi wengi tuna kasumba ya kushindwa kusoma nyakati. Kuhusu kutokea wakina Sankara, tayari hilo lishafanyika mwaka 2021 sema kwasababu ya mihemko ya kisiasa wengi tulishindwa kulitazama katika mapana yake. Mwendazake alienda, wengine waliumia, wengine walifurahia.

Tatizo lipo sehemu moja tu, katika lugha za kiusalama nchini Tanzania, Raisi ni alama muhimu mno ya ustawi wa nchi. Awe mzuri au awe mbaya, ni lazima dola lifanye kazi ya ziada kumlinda hadi pale anapomaliza muda wake. Tulikubaliana kwamba ni miaka kumi kwa kila Raisi. Huu utaratibu uvunjwe tu kwasababu asilia, lakini kama ni sababu za kisiasa au mkono wa mtu, nchi ni lazima iingie kwenye matatizo. Inaweza isiwe leo au kesho, lakini lazima matokeo myaone tu.

Mzee Nyerere alitengeneza mfumo wa aina yake hapa nchini. Hadi kufika mwaka 1985 alifanyiwa majaribio mengi na watu waliotaka kuwa wakina Sankara, Rawlings na Gaddafi. Mara zote alipona, siyo kwasababu ya kuwa na mfumo wenye nguvu, ila kwasababu wengi ndani ya mfumo walifahamu madhara ambayo yangetokea endapo mtu kama Nyerere angeondolewa kiholela. Hata wale ambao walikuwa hawakubaliana na sera zake walifahamu vizuri madhara yake ukizingatia hali ya siasa za Afrika wakati huo. Dola ilifanya ilihakikisha mzee anakuwa salama, na mambo yalivyoenda kombo walimpa ushauri ang'atuke.

Baada ya kung'atuka ukajengeka utamaduni kwamba Raisi hawezi kugusika. Hivyo tutashika sharubu za watu wote lakini siyo za Raisi. Wengi akiwemo Mzee Nyerere hawakumkubali Mzee Mwinyi, lakini kuheshimu taratibu za nchi na kudumisha amani, ilikuwa ni lazima amalize muda wake akiwa salama. Alitoka Warioba na baraza zima lakini Mwinyi akabaki. Huu utaratibu ulienda hadi kwa Mzee Kikwete, ambaye mbali na kuwa na kashfa kibao za ufisadi, walitolewa kafara wengine lakini yeye dola lilimlinda.

Hata wale wasiomkubali Mzee Kikwete na kuyatambua madhaifu yake, walimlinda kwasababu ya utaratibu uliowekwa nchini, kwamba Raisi hagusiki. Hili wanasiasa, wanausalama na raia tunalifahamu vizuri. Hata Tundu Lissu wakati wa kashfa ya TEGETA ESCROW alisema dhahiri, kwamba Raisi akitolewa madarakani utatokea mtikisiko mkubwa nchini, hivyo tushughulike na hawa watu wa chini yake. Wanausalama wengi waliishia kumkomesha tu kwa kuvujisha taarifa za kinachoendelea Ikulu, lakini waliacha amalize salama.

Utaratibu ulienda vizuri, mpaka pale ulipoharibiwa mwaka 2021. Kuna madhara makubwa kwenye makosa yaliyofanyika mwaka 2021. Mfano mbaya mno umewekwa, A bad precedent, kwamba Raisi anaweza akatolewa madarakani kwa namna yoyote ile bila madhara kutokea. Kama mwendazake ambaye alilindwa kuliko maraisi wote aliondoka na hayajatokea madhara yoyote, nini kitazuia mwingine asitolewe endapo kundi fulani ndani ya chama tawala au taasisi za kiusalama litataka mtawala atoke ?

Watanzania wengi, hasa wale wa kwenye vyombo vya usalama ambako mara zote watu aina ya Sankara na Rawlings hutokea huko wameshakula A Forbidden Fruit, hivyo macho yao ya kutambua mema na mabaya yamefunguka. Aheri wangeendelea kuaminishwa kwamba Raisi hagusiki, na akigusika yanaweza kutokea madhara. Kinyume chake wameoneshwa kwamba hakuna ambaye hagusiki hapa nchini. Siku za mbeleni, wanaweza wasiwe hawa mnaowaita Sukuga-Gang, bali genge jingine kabisa ambalo litazua taharuki kubwa, chama tawala ndivyo kilivyo.

Katika mahojiano na wahaini wa mwaka 1982, walikiri kuogopa madhara ambayo yangetokea kwa serikali yao endapo Mzee Nyerere angekutwa na jambo baya, kuuwawa au kutolewa madarakani. Katika taarifa zao wanasema kwamba Tanzania ingevamiwa na nchi jirani kama Msumbuji, Angola na Uganda ambazo maraisi wake walikuwa ni wafuasi kindakindaki wa Mzee Nyerere. Walikuja na mkakati kwamba pindi wamepindua nchi, basi kuidhibiti Msumbijia wangeanzisha mahusiano na magaidi ya Renamo na kuidhibiti Angola wangeanzisha mahusiano na UNITA. Haya yangetokea Tanzania isingetawalika.

Kule dola la Roma, kuna kipindi walipitia majanga kwa zaidi ya miaka 50, The Third Century Crisis. Kipindi hiki hakuna mfalme ndani ya dola la Rumi aliyefanikiwa kukaa kwenye kiti zaidi ya miaka saba bila kuuwawa au kupinduliwa na wanajeshi wake. Mambo yalianza kimzaha mzaha baada ya wanajeshi na majasusi kumuua mfalme Severus Alexander na kumuweka mtu mwingine. Wanajeshi na majasusi baada ya kuona kwamba wanaweza kumtoa mfalme ambaye alikuwa anachukuliwa kama mungu mtu, huu ndiyo ukawa utamaduni wao mpya kwa miaka zaidi ya hamsini.

Msihangaike na upinzani, chama tawala kimegawanyika kuliko wakati wowote ule. Huku ndiko upinzani utaanzia. Kuna watu wanaviziana na endapo kundi linalotawala leo hii litafanya makosa kidogo tu, basi tunaweza kuongelea mengine. Baada ya mwendazake lilifanyika jaribio kubwa ambalo halikufanikiwa. Huu ni ushahidi tosha kwamba nyumba imegawanyika, ndiyo maana inatumika nguvu kubwa mno kumsifia mtawala wa sasa huku tukimchafua mtawala wa zamani.
 
Hapana.
Nilijua hunielewi ninaandika nini na inawezekana ukawa hunielewi kwa haya niliyoandika hapa.

Tuliyoshindwa kuelewana kati yetu huko nyuma yako wazi kabisa. Usidhani nimebadili msimamo juu yake. sasa.

Ni kwamba sikuelewi kwakuwa unaandika mambo magumu sana, au huna tabia ya kueleweka?
 
CCM kimekuwa chama chenye milengo mbalimbali (rangi nyingi), na kwa maoni yangu hii ni sababu mojawapo inayofanya vyama vya upinzani wapate taabu sana kukikabiri barabara chama hiki na kukiondoa kwenye madaraka.

Ni hoja yangu kwamba, ni ndani ya CCM hiyo hiyo kwa kuwa na makundi mbalimbali, yenye milengo mbalimbali kiasi kwamba hivi vyama vya upinzani vilivyoko nje ya chama hicho, mahitaji yao (wenzao wenye milengo kama wao) tayari wamo ndani ya CCM.

Kwa hiyo, kwa chama kama CHADEMA, walipata taabu sana toka kwa kundi lililo upande wa Magufuli, huku wenzao waliomo ndani ya chama hicho, kutokana na muundo wa chama, hawakuweza kuinua kidole na kuwatetea CHADEMA.
Baada ya Magufuli kuondoka, kama alivyoondoka, na kundi lililokuwa limenyamaza likiwa upande wa akina Samia, sasa ndio wanaotawala anga. Kundi hili ni kundi lenye misimamo inayokubaliana karibu kwa kila kitu na CHADEMA, kasoro kuwaachia washike serikali. CHADEMA imejikuta haina wigo wa kumkabiri Samia, ambaye naye hatumii njia zilezile za kuwakandamiza kama alizotumia Magufuli.

Kwa hali hii, ni ajenda gani wanayoweza kuishika na kumkabiri nayo Samia? Ukandamizaji hakuna, Katiba Mpya, inazungumzika, Tume Huru, hili tutalifanyia kazi. Sasa CHADEMA imebaki na kitu gani kuwapelekea wananchi wawaunge mkono!

Mbowe kautazama ukweli huu, na kuamua kama alivyo amua ni nini chama chake kifanye.

Wakati huo huo, huko ndani ya CCM vikelele vya kundi la Magufuli linatafutiwa dawa. Kamati Kuu na Kamati mhimu zinasukwa upya kuondoa takataka za Magufuli huko. Hawa wanaopiga kelele pembeni, wakati wakiwa ndani ya chama, wengi wanatupiwa minofu, na wale ambao ni sugu kama akina Polex2, akina Bashiru, akina Kalamaganda wote wamekwishawekwa pembeni.

Hiyo ndiyo CCM, ambayo, kwa rangi zake mabalimbali na uwezo wa kujigeuza kila mara, imeapa" kutawala nchi hii milele"! Kweli?

Kama vyama vyote vya upinzani tayari wanayo makundi yao ndani ya CCM, yako wapi tena matumaini ya waTanzania?

Kwa mwendo huu huu, kuna siku tutajikuta akina Thomas Sankara wakiibuka bila ya kutegemewa. Hilo ndilo litakaloiondoa CCM na makundi yake yote, ndani na nje ya chama.

Sikuhariri chochote, naomba usinilaumu kwa makosa ya uandishi.
Bandiko linaeleweka. Dirisha la kuitikisa CCM baada ya kuondoka kwa Magufuli lilikuwa mwaka 2021 na kidogo 2022. Kwa kuruhusu wajipange upya na kurudi kwenye "comfortability" waliyofikia sasa, ni ngumu tena wale pro-Magufuli ndani ya CCM kuleta madhara ya kisiasa.

Hawa pro-Magu wataendelea kuchokonelewa na kutekenywa mara kwa mara ili kuangalia kama bado kuna masalia yaliyobaki yanayoweza kuibuka wakati usiotegemewa ila mtazamo wa CHADEMA kuhusu Magufuli na siasa zake unaipa CCM nafasi nzuri zaidi ya kupambana nao hao pro-Magu.

Kwa kumalizia ACT pia ni chama kitakachokuja kuisaidia sana CCM na naamini kilianzishwa kimkakati. Wakati CCM imeamua kukumbatia siasa za kibepari, ACT itatumika kama waendelezaji na watetezi wa sera za kijamaa zinazoachwa na CCM. Hii inafunga nafasi na uwezekano wa mtu mwingine kuja kuzitumia sera hizo kuiumiza CCM katika uwanja wa siasa.
 
CCMM ni DINI kama dini zingine,

Pia ni Kinyonga wa KIJANI na Manjano.

Tunakoelekea itatekwa na Aliye juu na itajipa umbo la Dini na kuja kuanzisha system yake ya kipekee duniani.

Mungu ataweka madhabahu yake hapa na tutakuwa msaada wa mataifa mengi.

Tusubiri.
 
"Mwaka 2021 na 2022", hii ilikuwa ni miaka ya "Kazi Iendelee". Kesi za akina Mbowe zikipamba moto huku zikichagizwa kwamba "washiriki wenzake tayari walishafikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo".

Hapana, hiyo miaka miwili haikuwa wakati ambapo pangeibuka upinzani ndani ya CCM, kwa sababu dereva mkuu alikuwa bado akitafuta njia ya kusawazisha na kuzima hilo kundi la upande wa Magufuli.
Hawa tayari wamekwisha dhibitiwa, ndani ya chama hakuna tena mwenye kufurukuta. Kumbuka, hoja ya mada ni kuwa, lengo kuu la haya makundi mbalimbali yaliyomo ndani ya CCM ni kufaidika wao, na siyo lazima kufaidika kwa taifa kwanza.
Kwa maana hiyo ni kwamba, masalia ya Magufuli yatakayokuwemo ndani ya CCM, sasa ni wakati wao kula kimya kimya ndani ya chama, siyo kula kwa kupiga kelele nyingi. Kundi la Samia ndani ya CCM chini ya Magufuli, ulisikia wakipiga kelele yoyote ile huku wakifaidika chini ya Magufuli?

Huo ndio muundo wa CCM ulivyo sasa hivi.

ACT Wazalendo? Ndani ya CCM? Sioni wanavyoweza kujipambanua. Sana sana hawa ni wa kumezwa tu na kuridhika na watakachotupiwa wakitafune.
 
Bandiko linaeleweka. Dirisha la kuitikisa CCM baada ya kuondoka kwa Magufuli lilikuwa mwaka 2021 na kidogo 2022. Kwa kuruhusu wajipange upya na kurudi kwenye "comfortability" waliyofikia sasa, ni ngumu tena wale pro-Magufuli ndani ya CCM kuleta madhara ya kisiasa.

Hawa pro-Magu wataendelea kuchokonelewa na kutekenywa mara kwa mara ili kuangalia kama bado kuna masalia yaliyobaki yanayoweza kuibuka wakati usiotegemewa ila mtazamo wa CHADEMA kuhusu Magufuli na siasa zake unaipa CCM nafasi nzuri zaidi ya kupambana nao hao pro-Magu.

Kwa kumalizia ACT pia ni chama kitakachokuja kuisaidia sana CCM na naamini kilianzishwa kimkakati. Wakati CCM imeamua kukumbatia siasa za kibepari, ACT itatumika kama waendelezaji na watetezi wa sera za kijamaa zinazoachwa na CCM. Hii inafunga nafasi na uwezekano wa mtu mwingine kuja kuzitumia sera hizo kuiumiza CCM katika uwanja wa siasa.
Usijidanganye alichotengeneza mwanadamu ni rahisi kukiharibu.
 
CCMM ni DINI kama dini zingine,

Pia ni Kinyonga wa KIJANI na Manjano.

Tunakoelekea itatekwa na Aliye juu na itajipa umbo la Dini na kuja kuanzisha system yake ya kipekee duniani.

Mungu ataweka madhabahu yake hapa na tutakuwa msaada wa mataifa mengi.

Tusubiri.
Tusubiri Hilo mpaka lini?
 
Andiko lako lingekamilika kama lingeonyesha mchango wa dola katika kuendelea kuiweka CCM mamlakani, CCM ni chama dola kuondolewa kwake kunahitaji mabadiliko makubwa katoka dola zaidi ya ubora wa chama pinzani tu.
CCM kimekuwa chama chenye milengo mbalimbali (rangi nyingi), na kwa maoni yangu hii ni sababu mojawapo inayofanya vyama vya upinzani wapate taabu sana kukikabiri barabara chama hiki na kukiondoa kwenye madaraka.

Ni hoja yangu kwamba, ni ndani ya CCM hiyo hiyo kwa kuwa na makundi mbalimbali, yenye milengo mbalimbali kiasi kwamba hivi vyama vya upinzani vilivyoko nje ya chama hicho, mahitaji yao (wenzao wenye milengo kama wao) tayari wamo ndani ya CCM.

Kwa hiyo, kwa chama kama CHADEMA, walipata taabu sana toka kwa kundi lililo upande wa Magufuli, huku wenzao waliomo ndani ya chama hicho, kutokana na muundo wa chama, hawakuweza kuinua kidole na kuwatetea CHADEMA.
Baada ya Magufuli kuondoka, kama alivyoondoka, na kundi lililokuwa limenyamaza likiwa upande wa akina Samia, sasa ndio wanaotawala anga. Kundi hili ni kundi lenye misimamo inayokubaliana karibu kwa kila kitu na CHADEMA, kasoro kuwaachia washike serikali. CHADEMA imejikuta haina wigo wa kumkabiri Samia, ambaye naye hatumii njia zilezile za kuwakandamiza kama alizotumia Magufuli.

Kwa hali hii, ni ajenda gani wanayoweza kuishika na kumkabiri nayo Samia? Ukandamizaji hakuna, Katiba Mpya, inazungumzika, Tume Huru, hili tutalifanyia kazi. Sasa CHADEMA imebaki na kitu gani kuwapelekea wananchi wawaunge mkono!

Mbowe kautazama ukweli huu, na kuamua kama alivyo amua ni nini chama chake kifanye.

Wakati huo huo, huko ndani ya CCM vikelele vya kundi la Magufuli linatafutiwa dawa. Kamati Kuu na Kamati mhimu zinasukwa upya kuondoa takataka za Magufuli huko. Hawa wanaopiga kelele pembeni, wakati wakiwa ndani ya chama, wengi wanatupiwa minofu, na wale ambao ni sugu kama akina Polex2, akina Bashiru, akina Kalamaganda wote wamekwishawekwa pembeni.

Hiyo ndiyo CCM, ambayo, kwa rangi zake mabalimbali na uwezo wa kujigeuza kila mara, imeapa" kutawala nchi hii milele"! Kweli?

Kama vyama vyote vya upinzani tayari wanayo makundi yao ndani ya CCM, yako wapi tena matumaini ya waTanzania?

Kwa mwendo huu huu, kuna siku tutajikuta akina Thomas Sankara wakiibuka bila ya kutegemewa. Hilo ndilo litakaloiondoa CCM na makundi yake yote, ndani na nje ya chama.

Sikuhariri chochote, naomba usinilaumu kwa makosa ya uandishi.
 
Andiko lako lingekamilika kama lingeonyesha mchango wa dola katika kuendelea kuiweka CCM mamlakani, CCM ni chama dola kuondolewa kwake kunahitaji mabadiliko makubwa katoka dola zaidi ya ubora wa chama pinzani tu.
Hili ni wazo mkuu 'Yoda', sasa najaribu kuwaza,.... Hii "Dola" kwani ni nani? Inayo tofauti yoyote na CCM?
Viongozi wote walioko huko, wanapomaliza kazi zao huko, au hata kabla huwa hawashiki nyadhifa mbalimbali serikalini na hata ndani ya chama?

Sasa jaribu kuunganisha uhusiano huo na hoja ninayoitetea kwenye mada hii kuhusu CCM kuwa muunganiko wa makundi yenye maslahi tofauti tofauti, mengine yakiwa nje ya chama hicho, lakini yakiwa na washirika wao ndani ya chama chenyewe!

Kwa hiyo swali linabaki ni lile lile. CCM itaondolewaje madarakani wakati ikiwa na sura zote hizi zinazounganishwa na maslahi ya kila kundi ndani ya chama. Kila kundi kunufaika kwake ni uwepo wa CCM, hata hiyo "dola" unayoisema wewe. Nje ya CCM makundi haya hayana kitu, kwa hiyo uwepo wa CCM ndiyo nyenzo yao kuu, na hawawezi kamwe kuivuruga ndani kwa ndani.

Ndipo nilipoangukia kwa akina Sankara.

Lakini si lazima iwe hivyo. Inawezekana kabisa kukazuka chama ambacho viongozi wake ni maslahi ya nchi tu basi, wasioshawishika na haya ya kujinufaisha wenyewe kwanza. Hili linawezekana kabisa na ninaamini waTanzania wataunga mkono juhudi za viongozi hao.
Kama Magufuli, na mapungufu yote yale, kaweza kuwakoga nyoyo sehemu kubwa ya nchi, haiwezekani wenye dhamira ya mioyo ya kuwatumikia wananchi wasiungwe mkono.

"Dola" kupambana na wananchi waliodhamiria kuweka mabadiliko, tunajua ni nani huwa ni mshindi mara zote.
 
Tanzania ni nchi yenye usiri mkubwa mno, na bahati mbaya sana wananchi wengi tuna kasumba ya kushindwa kusoma nyakati. Kuhusu kutokea wakina Sankara, tayari hilo lishafanyika mwaka 2021 sema kwasababu ya mihemko ya kisiasa wengi tulishindwa kulitazama katika mapana yake. Mwendazake alienda, wengine waliumia, wengine walifurahia.

Tatizo lipo sehemu moja tu, katika lugha za kiusalama nchini Tanzania, Raisi ni alama muhimu mno ya ustawi wa nchi. Awe mzuri au awe mbaya, ni lazima dola lifanye kazi ya ziada kumlinda hadi pale anapomaliza muda wake. Tulikubaliana kwamba ni miaka kumi kwa kila Raisi. Huu utaratibu uvunjwe tu kwasababu asilia, lakini kama ni sababu za kisiasa au mkono wa mtu, nchi ni lazima iingie kwenye matatizo. Inaweza isiwe leo au kesho, lakini lazima matokeo myaone tu.

Mzee Nyerere alitengeneza mfumo wa aina yake hapa nchini. Hadi kufika mwaka 1985 alifanyiwa majaribio mengi na watu waliotaka kuwa wakina Sankara, Rawlings na Gaddafi. Mara zote alipona, siyo kwasababu ya kuwa na mfumo wenye nguvu, ila kwasababu wengi ndani ya mfumo walifahamu madhara ambayo yangetokea endapo mtu kama Nyerere angeondolewa kiholela. Hata wale ambao walikuwa hawakubaliana na sera zake walifahamu vizuri madhara yake ukizingatia hali ya siasa za Afrika wakati huo. Dola ilihakikisha mzee anakuwa salama, na mambo yalivyoenda kombo walimpa ushauri ang'atuke.

Baada ya kung'atuka ukajengeka utamaduni kwamba Raisi hawezi kugusika. Hivyo tutashika sharubu za watu wote lakini siyo za Raisi. Wengi akiwemo Mzee Nyerere hawakumkubali Mzee Mwinyi, lakini kuheshimu taratibu za nchi na kudumisha amani, ilikuwa ni lazima amalize muda wake akiwa salama. Alitoka Warioba na baraza zima lakini Mwinyi akabaki. Huu utaratibu ulienda hadi kwa Mzee Kikwete, ambaye mbali na kuwa na kashfa kibao za ufisadi, walitolewa kafara wengine lakini yeye dola lilimlinda.

Hata wale wasiomkubali Mzee Kikwete na kuyatambua madhaifu yake, walimlinda kwasababu ya utaratibu uliowekwa nchini, kwamba Raisi hagusiki. Hili wanasiasa, wanausalama na raia tunalifahamu vizuri. Hata Tundu Lissu wakati wa kashfa ya TEGETA ESCROW alisema dhahiri, kwamba Raisi akitolewa madarakani utatokea mtikisiko mkubwa nchini, hivyo tushughulike na hawa watu wa chini yake. Wanausalama wengi waliishia kumkomesha tu kwa kuvujisha taarifa za kinachoendelea Ikulu, lakini waliacha amalize salama.

Utaratibu ulienda vizuri, mpaka pale ulipoharibiwa mwaka 2021. Kuna madhara makubwa kwenye makosa yaliyofanyika mwaka 2021. Mfano mbaya mno umewekwa, A bad precedent, kwamba Raisi anaweza akatolewa madarakani kwa namna yoyote ile bila madhara kutokea. Kama mwendazake ambaye alilindwa kuliko maraisi wote aliondoka na hayajatokea madhara yoyote, nini kitazuia mwingine asitolewe endapo kundi fulani ndani ya chama tawala au taasisi za kiusalama litataka mtawala atoke ?

Watanzania wengi, hasa wale wa kwenye vyombo vya usalama ambako mara zote watu aina ya Sankara na Rawlings hutokea huko wameshakula A Forbidden Fruit, hivyo macho yao ya kutambua mema na mabaya yamefunguka. Aheri wangeendelea kuaminishwa kwamba Raisi hagusiki, na akigusika yanaweza kutokea madhara. Kinyume chake wameoneshwa kwamba hakuna ambaye hagusiki hapa nchini. Siku za mbeleni, wanaweza wasiwe hawa mnaowaita Sukuma-Gang, bali genge jingine kabisa ambalo litazua taharuki kubwa, chama tawala ndivyo kilivyo.

Katika mahojiano na wahaini wa mwaka 1982, walikiri kuogopa madhara ambayo yangetokea kwa serikali yao endapo Mzee Nyerere angekutwa na jambo baya, kuuwawa au kutolewa madarakani. Katika taarifa zao wanasema kwamba Tanzania ingevamiwa na nchi jirani kama Msumbuji, Angola na Uganda ambazo maraisi wake walikuwa ni wafuasi kindakindaki wa Mzee Nyerere. Walikuja na mkakati kwamba pindi wamepindua nchi, basi kuidhibiti Msumbiji wangeanzisha mahusiano na magaidi ya Renamo na kuidhibiti Angola wangeanzisha mahusiano na UNITA. Haya yangetokea Tanzania isingetawalika.

Kule dola la Roma, kuna kipindi walipitia majanga kwa zaidi ya miaka 50, A Third Century Crisis. Kipindi hiki hakuna mfalme ndani ya dola la Rumi aliyefanikiwa kukaa kwenye kiti zaidi ya miaka saba bila kuuwawa au kupinduliwa na wanajeshi wake. Mambo yalianza kimzaha mzaha baada ya wanajeshi na majasusi kumuua mfalme Severus Alexander na kumuweka mtu mwingine. Wanajeshi na majasusi baada ya kuona kwamba wanaweza kumtoa mfalme ambaye alikuwa anachukuliwa kama mungu mtu, huu ndiyo ukawa utamaduni wao mpya kwa miaka zaidi ya hamsini.

Msihangaike na upinzani, chama tawala kimegawanyika kuliko wakati wowote ule. Huku ndiko upinzani utaanzia. Kuna watu wanaviziana na endapo kundi linalotawala leo hii litafanya makosa kidogo tu, basi tunaweza kuongelea mengine. Baada ya mwendazake lilifanyika jaribio kubwa ambalo halikufanikiwa. Huu ni ushahidi tosha kwamba nyumba imegawanyika, ndiyo maana inatumika nguvu kubwa mno kumsifia mtawala wa sasa huku tukimchafua mtawala wa zamani.
Akili kubwa sana,
 
Much respect to you, ww Si mvuja JASHO kama wengine, umeandika kama mtu mwenye uhakika wa kula.

Kwa uchambuzi wako murua,

Njia pekee ni Dola kuhakikisha inapatikana KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ikikosekana hiyo, basi inabidi turudi misri tu, hamna namna.

Bila mijeledi,chakula hakijaingia kinywani Bado.
Umesoma vzr na kumwelewa?, rudia tena kusoma ili uelewe halafu ndio uchangie
 
Back
Top Bottom